Saturday, May 31, 2014

GARI ALILOPATANALO AJALI DIIRECTOR GEORGE TYSON SAA NNE KABLA YA TUKIO

 
Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.

Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.

Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.



 



Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.



 
CHANZO DJ CHOKA 

Thursday, May 29, 2014

WATUHUMIWA WA MILIPUKO ARUSHA WAFIKISHWA MAHAKAMANI



                                    Watuhumiwa wakipelekwa polisi


Mmoja wa watuhumiwa hao akipakiwa kwenye Gari la Polisi tayari kwa Kupelekwa Mahakamani kusikiliza kesi yao.

WATU 17 wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu Mkazi jijini Arusha, kujibu mashitaka 16 yakiwemo ya kuua kwa kutumia bomu,kutesa binadamu na kusajili vijana na kuwapeleka nje ya nchi kufanya ugaidi.

Watu hao walifikishwa mahakamani hapo leo na kusomemewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siama ambapo hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na kile kilichoelezwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kutenda tukio hilo Aprili 13,katika nyumba ya kulala wageni na baa ya Arusha Night Park iliyopo Mianzini jijini hapa,ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi juni 11 mwaka huu kwa mtuhumiwa namba moja na namba nne na watuhumiwa wengine waliobaki kesi yao itatajwa tena juni 12

Katika tukio hilo la mlipuko huo wa bomu watu 14 walijeruhiwa vibaya katika maeneo mbalimbali ya miili yao hali iliyopelekea mmoja wa majeruhi hao aliyefahamika kwa jina la Sudi Ramadhani mkazi wa Kaloleni jijini hapa kufariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru.
Kwa hisani ya Mtaa kwa Mtaa Blog

Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya Polisi Arusha,kabla ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani,Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai nchini (DCI) Isaya Mngulu amesema kuwa mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo, polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama walianza upelelezi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Ameongeza kuwa pia siku hiyo hiyo ya tukio hilo la mlipuko wa bomu katika baa ya Arusha Night Park muda mfupi baadae bomu lingine la aina ileile liligundulika kutegwa katika baa ya Washington ya jijini hapa ambapo bomu hilo liliondolewa katika eneo hilo bila kuleta madhara .
"Aidha baadhi ya watuhumiwa hawa pia walibainika kuwa na mikakati ya mashambulizaya namna hiikatika maeneo mengine na sehemu mbalimbali hapa nchini ambazo ni taasisi za Serikali na sehemu zenye mikusanyiko ya watu,ambapo pia wanajihusisha na uandaaji wa vijana kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini na kuwapeleka nchi za nje ili kujiunga na makundi ya kiuhalifu"alisema Mkurugenzi huyo wa Mashitaka nchini.
Mkurugenzi huyo amesema kwamba upelelezi wa matukio haya bado unaendelea ili kuwakamata watiliwa shaka wenginewaliobaki katika matukio ya milipuko ya mabomu katika Kanisa Katoliki Olasitna uwanja wa Soweto yaliyotokea mwaka jana jijini hapa na sehemu nyingine nchini.

Ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa lengo la kuwafichua wahalifu wa ndani na nje wa matukio haya ya kihalifuna matukio mengine kwa lengo la kuvuruga amani na utulivu wa nchi.

DIMOND AFANYA KOLABO MPYA NA INYANYA,DAVIDO MJINI LONDON


Screen Shot 2014-05-27 at 1.31.14 AM 
Wiki iliyopita Diamond Platnumz alikua London Uingereza kwa ajili ya kufanya show lakini pia vilevile kufanya video ya wimbo wake aliofanya na msanii Iyanya wa Nigeria.
Exclusive interview na meneja Babtale ambae anasimamia kazi za Diamond sasa hivi ambapo amesema kutokana na kupiga hatua kwa Diamond na kuingia kwenye levo za kimataifa, imebidi waanze kufanya video za kiwango hicho cha kimataifa lakini haimaanishi kwamba ndio Platnumz hatofanya tena video Tanzania’
Namkariri Tale akisema ‘video tuliyofanya na Iyanya Uingereza ni kwa sababu tulikua tunamuhitaji Director MoE Musa ambae anaishi na kufanya kazi zake Uingereza ndio maana tukasafiri mpaka huko, kuna video ambayo tutafanya Nigeria tukishatoka Ghana na pia ikitokea kwamba tunatakiwa kufanya video Tanzania tutafanya hivyo’
Screen Shot 2014-05-29 at 2.28.04 AM Mmetumia kiasi gani cha pesa kufanya hii video Uingereza?
Bab Tale: ‘kiukweli tunaumia, tunaumia kwa sababu kumlipa Moe Musa na kupata kila kitu kama kwenye hii video ya juzi tumemlipa Moe peke yake dola elfu 25 ambazo zinagonga mpaka milioni 40 za Kitanzania, bado usisahau tumewatoa kina Iyanya Nigeria kwa hela yetu kuwaleta London, kuwalipia nauli ya business class kwenye ndege na hoteli hawawezi kulala hoteli mbaya kama sisi watoto wa Manzese’
Kwenye sentensi nyingine, Babtale ameithibitishia kwamba Diamond atasikika tena kwenye kolabo nyingine na Davido itakayowahusisha pia Tiwa Savage wa Nigeria na Mafikizolo wa South Africa ikiwa ni kampeni ya kituo kimoja kikubwa cha TV Afrika

LAPF YAMKANA KUMDAI MBOWE PIA YAWAKANA KUWASAIDIA MSIGWA NA MBILINYI


Mbowe, Hawa ghasia na Peter Msigwa
SIKU chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa Tawala za Mikoa (Tamisemi), Hawa Ghasia, kusema kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amekopa kiasi cha sh bilioni moja kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Eliud Sanga, amekanusha.

LAPF pia imekana kuwasaidia fedha au vifaa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Iringa Mjini, Peter Msigwa, kama ilivyosemwa bungeni. Juzi, Ghasia alisema kuwa Mbowe anadaiwa sh bilioni moja na LAPF na ametumiwa waraka wa kumkamata ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waziri huyo alisema si kosa kwa wabunge kupewa fedha na LAPF, lakini ni kosa kwa mbunge kutorejesha fedha alizokopeshwa.

Kauli ya LAPF
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Sanga, alibainisha kuwa LAPF haijawahi kumkopesha Mbowe sh bilioni moja, na kwamba mfuko huo hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo.
“Mfuko wa LAPF hauna utaratibu wa kukopesha mtu mmoja, hivyo hakuna mikopo ya aina hiyo na wanachofanya ni kutoa mikopo ya wanachama wake kupitia vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) na mikopo ya nyumba kwa wanachama wanaokaribia kustaafu,” alieleza Sanga.
Alisema shughuli kuu za mfuko huo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango, uwekezaji na kulipa mafao. “Ieleweke kuwa ingawa waheshimiwa wabunge au mtu au taasisi yoyote hazuiliwi kuomba msaada wa kijamii, Mbilinyi na Msigwa hawajawahi kuwasilisha maombi na hawajawahi kupewa msaada wowote na LAPF.

Tuesday, May 27, 2014

WAMACHINGA WAMUUA ASKARI JIJINI DAR ES SALAAM


Marehemu Stephano Benjamin Komba (36) ambaye aliyekuwa na cheo cha sajenti.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana wanaodaiwa ni Wamachinga wamemuua askari mmoja wa Jiji la Dar es Salaam kwa kumpiga na stuli kichwani wakati akitimiza majukumu yake.



Akizungumza na waandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa kuuaga mwili huo, Mkuu wa Oparesheni Manispaa ya Ilala, Charles Wambura alimtaja marehemu kwa jina la Stephano Benjamin Komba (36) aliyekuwa na cheo cha sajenti.



Mke wa marehemu Stephano Benjamin Komba (mwenye kilemba cheupe).

Alisema tukio hilo lilijiri Mei 16, mwaka huu, saa 7.30 mchana kwenye Mtaa wa Raha Kariakoo.
“Marehemu alikuwa na askari wengine walikamata baadhi ya bidhaa za Wamachinga kwa lengo la kuwaondoa lakini ghafla walivamiwa na kundi la wafanyabiashara hao ambapo Sajenti Komba akapigwa kichwani kwa stuli hali iliyomfanya apoteze fahamu kwa kuvuja damu nyingi.

“Askari walipambana na hao Wamachinga na kufanikiwa kumuokoa Sajenti Komba lakini akiwa na hali mbaya.

Mke wa Marehemu Stephano Benjamin (katikati) akisaidiwa na jamaa wa karibu msibani kumuaga marehemu mume wake.

“Walimkimbiza Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo walimpeleka Muhimbili ambapo alifariki dunia saa 2:00 usiku,” alisema Wambura.
Mwili wa marehemu uliagwa Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mbagala na kusafirishwa kwao Songea, mkoani Ruvuma kwa mazishi.

Wambura aliongeza kuwa, hakufurahishwa na kitendo hicho cha Wamachinga kuchukua sheria mkononi.Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutii sheria bila shuruti.

MASTAA BONGO MUVI WAMLILIA RECHO

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akilia kwa uchungu.

Huzuni tele ikiwa imetawala wasanii waliokuwa viwanja ya Leaders.

Bi. Mwenda akilia kwa uchungu.

Mume wa Rachel aitwaye Saguda akiwa na majonzi.

Mwigizaji Johari akiwa na huzuni.

Steve akizungumza na wanachama wa Bongo Muvi, viwanja vya Leaders.

Bongo Muvi wakijadili cha kufanya.

Wasanii wakipanga utaratibu wa msiba wa mwenzao.

Wasanii wa Bongo Muvi wakiwa Muhimbili baada ya kupata habari za kifo cha mwenzao.
MASTAA wa Bongo Muvi wamemlilia msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' aliyefariki jana saa mbili usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar baada ya kujifungua ambapo mtoto wake alifariki muda mfupi na baadaye yeye akafariki.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve ‘Nyerere’, mwili wa Rachel utasafirishwa kwenda kwao Songea kwa ajili ya maziko. Habari nyingine za msiba zitatolewa wakati wowote na mtandao huu mara tu zinapopatikana.
GREDIT GPL

KUONDOA SHILINGI NI MCHEZO WA KUIGIZA!

@Mwanamabadiliko
KATIKA hili bunge la bajeti linaloendelea sasa hivi, pamoja na kwamba limekosa mvuto kutoka kwa jamii ya watanzania, kuna mambo matatu nimeyagundua. Kwanza, huu utaratibu wa kuondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri ni kama mchezo wa kuigiza kwa kuwa wabunge wanaoshika hizo shilingi hatimaye huziachia na vifungu vya ovyo vya bajeti hupitishwa.
 
Pili, kwa mara ya kwanza katika historia ya bunge hili nimeshuhudia wabunge wa CCM wakiondoa shilingi kwenye mshahara wa waziri wa chama chao. Nadhani ni muendelezo ule ule wa kuleta mzaha na kuwakoga wananchi wanaowatazama ili waone kwamba wana uchungu na maendeleo yao wakati si kweli. 

Lakini pia wanafanya hivyo ili kufuata mkumbo wa wabunge wa UKAWA ambao tangu mwanzo walitahadharisha kushika shilingi za mishahara ya mawaziri ambao wameshindwa kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Kinachowaponza wabunge wa UKAWA ni uchache wao kwani hata kama wakishika shilingi, mwisho wa siku wabunge wa CCM watapiga kura za Ndiyooooooooooooooo ili kuwaokoa mawaziri wao wa CCM.
 
Tatu, nimegundua kwamba mle bungeni kuna wabunge wa CCM ambao wao kazi yao kubwa wanayoijua ni kusema NDIYOOOOOOOOOOO kwa sauti kubwa ili vifungu vya bajeti, hata vile vibovu, vipite bila kupingwa. Kundi hili huwa halichangii chochote bungeni. Wakishaingia bungeni wakasaini kwenye kitabu cha posho, hukaa mezani na kusubiri kugonga meza. 

Hili ni suala la kustaajabisha sana kwani wabunge hawa wametumwa na wananchi waende kuwawakilisha lakini wamegeuka kuwa wachumia tumbo na watetezi wa ukandamizaji wa serikali dhidi ya wananchi. 

Na kwa kuwa moja ya kazi ya wabunge ni kuibana serikali iwahudumie wananchi, wabunge hawa wa CCM ni wasaliti wa wapiga kura wao na hawafai kurejeshwa bungeni tena msimu ujao. Inasikitisha sana kuona kwamba wabunge hawa wa CCM wapo bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wananchi badala ya kuwatetea!

MH; BENARD MEMBE WAASI WA M23 WALITOKA RWANDA


Waasi wa M23
Tanzania kwa mara ya Kwanza imesema inayo uhakika kuwa waasi wa M23 walioondolewa nchini Jamuhuri ya Kongo ni ni raia Rwanda.Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Benard Membe ameliambia Bunge la Tanzania kuwa anao uhakika kuwa waasi M23 walitokea nchini Rwanda.
Hii ni Mara kwanza kwa Tanzania kukiri hadharani kuwa inao uhakika kuwa waasi hao ni raia wa Rwanda.
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimepeleka majeshi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo kwa kushirikiana na yale ya umoja wa Mataifa yaliwaondoa waasi hao DRC

Benard Membe Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania
Matamshi hayo ya Waziri huyo aliyatoa wakati alipokuwa akiwasilisha hotuba ya Bajeti ya Wizara yake ambapo pia alikiri kuwa bado uhusiano wa Tanzania na Rwanda sio mzuri.
Hata hivyo upande wa Upinzani mlishambulia Waziri huyo wa Mambo ya nje Benard Membe wakidai kwamba Waziri huyo anachochea kuvurugika kwa uhusiano wa Watanzania na Rwanda kwa kuhisi kuwa M23 ni Wanyarwanda nahata kutaka achukuliwe adhabu kali.
Mbali na tuhuma hizo Waziri Membe alizidi kusisitiza kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda akisema hiyo ni ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Mbali na waziri baadhi ya wabunge wanamuunga mkono waziri Membe kuwa waasi wa M23 ni raia wa Rwanda wao.
Matamshi haya Waziri wa Tanzania kuhusu M23 bado haijulikana ni kwa namna gani utaathiri uhusiano wa Tanzania na Rwanda kama utakuwepo huenda ukajulikana hapo baadae

Monday, May 26, 2014

UCHAGUZI MALAWI WAZIDI KUWA KITENDAWILI.

 
Rais Joyce Banda awali alitaka matokeo ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali 

Uchaguzi mkuu wa Malawi umeendelea kubeba sura mpya ya sarakasi za mapingamizi ya kisheria, baada ya mahakama kuu ya Lilongwe kuamuru Tume ya uchaguzi nchini humo iendelee na mipango ya kazi zake bila kuingiliwa na mamlaka yeyote.
Uamuzi huo umetokana na ombi la chama cha Malawi Congress MCP kutaka mahakama hiyo izuwie amri ya Mahakama kuu ya Blantyre iliyo iamuru tume ya uchaguzi kuhesabu kura na kumtangaza mshindi ndani ya siku 8, likiwa ni ombi la chama cha DPP.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza aliye mjini Lilongwe anasema kuwa uamuzi huo sasa una maana kwamba MCP imeshinda kesi ambapo pamoja na mambo mengine wanataka kazi ya kuhesabu kura ianze upya nchi nzima jambo ambalo ndiyo maamuzi ya tume na vyama vyote vya siasa isipokuwa DPP.
Tume ya uchaguzi inakutana mjini Blantyre na itatoa taarifa baadaye kuhusu uamuzi uliochukuliwa na Mahakama Kuu hii leo.
Huku ikijulikana wazi kuwa kinachosubiriwa sasa ni ama kurudiwa kuhesabu kura za maeneo yenye mgogoro au kura zote za nchi nzima.
'DPP waja juu'
Jumamosi mchana tume ya uchaguzi kwa pamoja na vyama vya siasa walikubaliana kurudia kuhesabu kura zote kutokana na kugundulika makosa mengi katika baadhi ya maeneo, huku DPP ikigomea hatua hiyo na kuamua kwenda mahakama kuu mjini Blantyre kuzuia mpango huo ikitaka zihesabiwe zile tu zinazotiliwa mashaka.
Jaji Lloyd Muhara wa mahakama hiyo alikubaliana na ombi la DPP jambo ambalo pia likazua upya mgogoro wa kisheria ambapo vyama vingine vikaungana kwa pamoja na wagombea binafsi kupeleka zuio kwenye mahakama kuu ya Lilongwe chini ya kundi la wanasheria zaidi ya 12 wa chama cha MCP.
'Wizi wa kura'
Vijana kwa wakongwe wote walijitokeza kushiriki uchaguzi huo ambao wadadis wanasema umegeuka sarakasi
Uchaguzi wa Malawi umekumbwa na wimbi la mivutano miongoni mwa vyama vikuu vya siasa vilivyo simamisha wagombea urais wa nchi hiyo.
Dalili za kujitokeza kwa matatizo zilianza mapema siku mbili baada ya uchaguzi ambapo baadhi ya vyama kikiwemo chama tawala Peoples Party cha Rais Dr Joyce Banda walilalamika kuwa kuna mchezo mchafu umefanyika katika shughuli nzima ya upigaji kura.
Siku chache zilizopita Rais Banda alitoa amari ya kuufuta uchaguzi huo na kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 kwa madai ya wizi na ulaghai uliokumba uchaguzi, lakini Mahakama kuu ilisema hana mamlaka hayo.
Siku mbili baadaye tume ya uchaguzi MEC chini ya mwenyekiti wake Jaji Mackson Mbendera, ikatangaza kuwa ni kweli imegundua ubadhirifu katika baadhi ya maeneo na hivyo lazima kura zote zihesabiwe upya.
Kufikia sasa haijajulikana nini itakuwa hatma ya kura zilizopigwa na wananchi zaidi milioni saba wa nchi hiyo huku vyama vya DPP na MCP kila kimoja kikidai kuwa kilielekea kushinda uchaguzi huo

RAIA WA MISRI WACHAGUA RAISI MPYA


Mabango yanayotangaza uwaniaji wa aliyekuwa Mkuu wa jeshi la Misri, Abdel Fatah al-Sisi, kama Rais

Raia wa Misri wanapiga kura kwa muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama.
Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .
Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.
Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi

UMESHASIKIA HII!!! "TUZO ZA WATU" HAPA TANZANIA!! PIGA KURA SASA


tuzo 2

Tuzo za Watu ni tuzo mpya Tanzania zinazoendeshawa na Bongo 5 Media Group ambapo mwaka huu imeweka vipengele vya kushindanisha 11na kila kipengere kuna washindani 5. Utaratibu ni kwamba kura zitapigwa kuwapata washiriki 3 kila kipengele na ndio watakaoshandanishwa siku ya mwisho na wale wengine 2 wataalikwa kama wageni wa heshima siku ya kutoa tuzo hizo.

Vipengele na wasanii/stars wanaoshindanishwa ni hivi hapa

1.MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
1. Vanessa Mdee – Choice FM
2. Millard Ayo – Clouds FM
3. Hamis Mandi aka B12 – Clouds FM
4. Mariam Kitosi – Times FM
5.Ergon Elly – Mbeya Highlands FM

2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
1. The Hitlist – Choice FM
2. Xxl – Clouds FM
3. Amplifaya – Clouds FM
4. Hatua Tatu – Times FM
5. Power Breakfast- Clouds FM

3. MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
1. Salama Jabir – EATV
2. Sam Misago – EATV
3. Zamaradi Mketema- Clouds TV
4. Salim Kikeke – BBC Swahili
5. Gondwin Gondwe – ITV

4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
1. Friday Night Live – EATV
2. Mkasi – EATV
3. Planet Bongo – EATV
4. Uswazi – EATV
5. Take One – Clouds TV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
1. Juma Kaseja – Yanga
2. Mrisho Ngassa – Yanga
3. Mbwana Samatta – TP Mazembe
4. Ramadhan Singano – Simba SC
5. Francis Cheka
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
1. Nisher
2. Adam Juma
3. Nick Dizzo
4. Mecky Kaloka
5. Jerry Mushala
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
1. My Number – Diamond
2. Jikubali – Ben Pol
3. Mirror – Baby
4. Love Me – Izzo Bizness f/ Barnaba & Shaa
5. Muziki Gani – Nay wa Mitego f/ Diamond

8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
1. Amani ya Moyo – Feza Kessy
2. Closer – Vanessa Mdee
3. Sugua Gaga – Shaa
4. Yahaya – Lady Jaydee
5. Nakomaa na JIJI – Shilole

9. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Elizabeth ‘Lulu’ Michael
2. Jacqueline Wolper
3. Shamsa Ford
4. Irene Uwoya
5. Wastara Juma

10. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
1. Jacob Stephen aka JB
2. King Majuto
3. Vincent ‘Ray’ Kigosi
4. Hemedy Suleiman
5. Salim ‘Gabo’ Ahmed

11. FILAMU INAYOPENDWA
1. Foolish Age – Elizabeth Michael
2. Bado Natafuta – Salim Ahmed, Shamsa Ford
3. Shikamoo Mzee – JB, Shamsa Ford, Majuto
4. Ndoa Yangu – Kanumba, Wolper
5. Zawadi Yangu – JB, Irene Uwoya

Kupiga kura katika Tuzo za Watu bonya hii link http://tuzozetu.com/vote/
Ili kupata ufafanuzi wa kina na jinsi ya kupiga kura kwa kutumia simu bofya hapa http://www.bongo5.com/tuzo-za-watu-zazinduliwa-rasmi-wasanii-wa-muziki-filamu-na-watangazaji-wa-radio-na-tv-kutuzwa-02-2014/

Sunday, May 25, 2014

KILL TOUR YAFANA SANA MJINI MOSHI


k20Ni show ambayo ilifanyika kwenye uwanja wa Ushirika Moshi Kilimanjaro na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu wa nguvu wanaosupport bongofleva kuona list ya wakali akiwemo Ommy Dimpoz, Ney wa Mitego, Profesa Jay, WEUSI, Ay na FA,
 Prof Jay  ,Kavishe na Wadau wengine.
 Weusi  wakiamsha amsha kwenye stage....
 G-Nako ..


 Mwana Fa..
 Hevy weight Mc..
 Dimpoz kwa poz..Mzee wa tupogo..

 Weusi ,Ay, Prof jay..


 Crown ilikiwa imejaa vibaya..

k1Picha naShafiq 

Saturday, May 24, 2014

LEO NI REAL MATRID AU ATLETICO MATRID KUSHINDA KOMBE LA UEFA

Ronaldo na Bale kuchuana dhidi ya Atletico Madrid

Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo na mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani Gareth Bale watakuwepo katika timu ya Real Madrid itakayochuana na Atletico Madrid katika fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa jumamosi hii.
Ronaldo, 29, alikuwa amekosa kucheza mechi mbili akiuguza jereha sawa na mshambulizi Gareth Bale, 24, ambaye hakushiriki katika mazoezi siku ya jumanne.
Wawili hao kwa ushirikiano wamiefungia Real Madrid mabao 68 msimu huu.
Kocha Carlo Ancelotti, ambaye anapania kuwa mkufunzi wa pili katika historia ya mchuano huu kuwahi kushinda taji la ubingwa barani Ulaya mara tatu amethibitisha kuwa nyota hao wawili wakali kwa mashambuli watakuwepo
Ronaldo atacheza dhidi ya Atletico Madrid

Lisbon huku akiongezea kuwa anasubiri ithibati ya muuguzi wa timu kuhakiki kuwepo kwa mlinzi Pepe na mshambulizi Karim Benzema.
Benzema alijeruhiwa Real ilipoibana Espanyol 3-1 huku Pepe akisalia kwenye bench kwa zaidi ya majuma mawili sasa.
Real Madrid inapania kutawazwa mabingwa wa Uropa iwapo watawalaza washindi wapya wa ligi kuu ya Uhispania Atletico Madrid mbali na kusitisha ukame wa miaka 12 wa kombe hilo lenye umaarufu barani Uropa.

RAISI ZUMA AAPISHWA KWA MUHULA WA PILI.

Rais Jacob Zuma
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameapishwa kwa muhula wa pili wa uongozi.
Maelfu ya wafuasi, wakipepea bendera za taifa, walishangilia ndege za jeshi za Afrika Kusini zilipopita juu ya uwanja wa sherehe.
Viongozi wa nchi 20 walikuwako katika sherehe hiyo.
Katika hotuba yake ya kutawazwa Rais Zuma aliahidi kuwa serikali yake itakuza uchumi na nafasi za ajira.
Chama chake cha ANC kilishinda uchaguzi awali mwezi huu ambapo kilipata kura zaidi ya asili-mia-60.
Hii ni mara ya tano kwa chama cha ANC kushinda katika uchaguzi na kimeongoza nchi tangu utawala wa ubaguzi wa rangi kumalizika.

LOUS SUAREZ KUTOCHEZA KOMBE LA DUNIA BRAZILI 2014


Hofu iwapo Suarez atacheza Brazil
Matumaini ya mashabiki wa Uruguay kuwa mshambulizi wa Liverpool ya Uingereza ataiongoza timu yao katika kombe la dunia yameingia ati ati baada ya mshambulizi huyo bora katika ligi kuu ya Uingereza kufanyiwa upasuaji wa dharura wa goti lake mapema leo.
Suarez aliyeisaidia Uruguay kumaliza katika nafasi ya nne katika kombe la dunia ya mwaka wa 2010 iliyokuwa huko Afrika Kusini alitarajiwa kushiriki katika safu ya mashambulizi lakini upasuaji huu unamaanisha hatoweza kushiriki katika maandalizi kwa jumla ya majuma matatu hivi.
Kulingana na ripoti za magazeti nchini Uruaguay mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 27 aligundua jumatano kuwa alikuwa na jeraha la goti na akalazimika kufanyiwa upasuaji wa kisasa kwa haraka kuambatana na ushauri wa muuguzi mkuu wa timu hiyo ya taifa.
Kulingana na daktari huyo mfumo uliotumika kwa operesheni hiyo ''arthroscopy'' itamruhusu Suarez kupata nafuu kwa takriban siku 15-20 na hivyo huenda akarejea kabla ya kuanza kwa kipute hicho cha fainali ya kombe la dunia .

Hofu iwapo Suarez atacheza Brazil
Shirikisho la soka nchini humo imetoa taarifa kwa vyombo vya habari huko Montevideo ikisema kuwa wanamtarajia nyota huyo wa Uruguay kurejea mapema .
Uruguay imeratibiwa kufungua kampeini yake dhidi ya Costa Rica mjini Fortaleza mnamo Juni 14

UCHAGUZI WA MALAWI UMEFUTWA NA JOYCE BANDA HATOGOMBEA TENA


Screen Shot 2014-05-24 at 3.49.25 PM 
Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.

Wednesday, May 21, 2014

NI MIAKA 18 TANGU KUZAMA KWA MV BUKOBA NDUGU NA JAMAA WAWAKUMBUKA KWA KUWAOMBEA.





Baba mzazi wa flaviana pamoja na wadogo zake


Tanzania leo tumewakumbuka ndugu zetu ambao walipoteza maisha kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni mama mzazi wa mwanamitindo Flaviana Matata pamoja na mtoto wa mjomba wake ambao walikua safarini.

Leo Flaviana Matata akiwa na Ambwene Yesaya ‘Ay’ na baadhi ya wasanii wengine wa Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa dini waliungana na Watanzania waliopata nafasi kuhudhuria ibada iliyofanyika kwenye makaburi yaliyopo eneo la Igoma Jijini Mwanza.












































Nyaisa Simango ni Mmoja wa walionusurika na ajali ya Mv Bukoba