Matumaini ya mashabiki wa
Uruguay kuwa mshambulizi wa Liverpool ya Uingereza ataiongoza timu yao
katika kombe la dunia yameingia ati ati baada ya mshambulizi huyo bora
katika ligi kuu ya Uingereza kufanyiwa upasuaji wa dharura wa goti lake
mapema leo.
Suarez aliyeisaidia Uruguay kumaliza katika
nafasi ya nne katika kombe la dunia ya mwaka wa 2010 iliyokuwa huko
Afrika Kusini alitarajiwa kushiriki katika safu ya mashambulizi lakini
upasuaji huu unamaanisha hatoweza kushiriki katika maandalizi kwa jumla
ya majuma matatu hivi.Kulingana na ripoti za magazeti nchini Uruaguay mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 27 aligundua jumatano kuwa alikuwa na jeraha la goti na akalazimika kufanyiwa upasuaji wa kisasa kwa haraka kuambatana na ushauri wa muuguzi mkuu wa timu hiyo ya taifa.
Kulingana na daktari huyo mfumo uliotumika kwa operesheni hiyo ''arthroscopy'' itamruhusu Suarez kupata nafuu kwa takriban siku 15-20 na hivyo huenda akarejea kabla ya kuanza kwa kipute hicho cha fainali ya kombe la dunia .
Uruguay imeratibiwa kufungua kampeini yake dhidi ya Costa Rica mjini Fortaleza mnamo Juni 14
No comments:
Post a Comment