Wednesday, April 30, 2014

BASI LA HOOD LAWAKA MOTO LIKIWA SAFARINI KUTOKA ARUSHA KWENDA ARUSHA


   
Imeripotiwa watu 55 waliokuwa ndani ya basi la kampuni ya Hood wakisafiri kutoka Mbeya kwenda Arusha wamenusurika kufa baada ya basi hilo kushika moto na kuteketea kabisa katika kijiji cha Kilolele, Chalinze mkoani Pwani.
Katika ajali hiyo abiria 40 walijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao na kukimbizwa katika Hospitali ya mkoa ya Morogoro kwa matibabu

HAYA NDO MAMBO ANAYO FANYA MWANAUME KAMA MSICHANA ANAFAA KUOA

Hizi ndo marks (majibu) ya kupata ndoa mapema..........hii inawahusu hadi wale walio kwenye uchumba chronic/sugu
Hamna haja ya kunywa mchina uongeze makalio,wala kuenda kwa sangoma upate ndoa ndani ya siku 3 ,ukiona miaka mvua za masika zinakukatikia hujaitwa Mrs somebody habari.

Hii hapa > Mambo ambayo mwanaume anafanya kukutest kama wewe msichana unafaa kuwa mke wake:
1. Ukienda kwake ukutane na vyombo vichafu na nguo chafu zimejazana usidhani ni mvivu, ni kamtihani anakupa. 

2. Ukiingia kwake ukaona anampigia simu yule dada wa usafi anayekujaga mara moja kwa wiki aje afanye usafi alipwe usidhani eti anajali kihivyo. Anakutest aone kama utasema "Acha baby, ntakufulia mpenzi wangu".

3. Ukikuta kwake amefanya shopping ya vyakula vya kupika kama unga, mchele, na vingine halafu akakwambia mwende ule mgahawa fulani mkapate dinner usidhani eti ana hela kibao ya kutumia! Anakutest aone kama utamwambia mbaki kwake mpike mle. Uko chumba cha mtihani!

4. Siku kakuahidi kukutoa out halafu unafika kwake unakuta kajikunyata kama mgonjwa anakwambia mama ake kapiga simu anaumwa anaomba atumiwe hela. Halafu anakwambia hela aliyo nayo na ukipiga mahesabu unaona ni kama ile ya kutumia mkiwa out. Anakuomba ushauri afanyaje. Wewe unamwambia "Baby twende out, suala la mama nina uhakika kaka zako na dada zako watalishughulikia, atawapigia". Woiyeeee! My sista hapo umejimaliza!!

5. Ukimtembelea kwake ukakuta anapika na kufanya usafi wewe Umekaa tu unaangalia muvi halafu ukitaka umsaidie anakwambia endelea kuangalia muvi karibu anamaliza na wewe kweli ukarudi ukakaa kuendelea na muvi yako! Siku zako zinahesabika!!

6. Ulishawahi kumwambia mpenzi wako aende kwenye ibada? Alipokataa ulimsisitizia? My sister, hata walevi wanapenda wanawake ambao wanawasisitiza kwenda kwenye ibada. Sio tule wale kila siku wanashinda baa na club.

7. Mara ngapi huwa unamkumbusha kuwapigia simu wazazi au ndugu zake kuwajulia hali mkiwa wote? Angalao akupe na simu na wewe uwasalimie? Huo ni mtihani mwingine huwa mnafeli sana.

8. Jifunze pia kusisitiza kujitunza kabla ya ndoa. Sio kila saa ukimtembelea ni kujiachia tu. Inaleta adabu na inawafanya mkazanie kufikia lengo kubwa la maisha.
9. Jaribu ukiwa unaenda kwake uwe unaenda na tuvitu kama nyanya, vitunguu, n.k. Hivyo vyote huwa wanaume ni shida kununua mara nyingi.

10. Wakati mwingine nenda kwake hata na CD za dini mpelekee msikilize. Sio kila ukifika kwake wewe ni rege, Eminem, Lil Wayne na kina nani sijui. Ukiwa hivyo hataona tofauti kati yako na wale macho juu anakutana nao club kila wikiendi.

11. Jenga na tabia ya kumnunulia tuzawadi tudogo tudogo. Sometimes unakuja na boksa au kavesti au kadodoranti. Hiyo kwa wanaume inaonyesha unaweza kujipa majukumu na kuyasimamia. Marks hizo.

KWA WALE WOTE WENYE VITAMBI HIZI NI AINA 6 ZA VITAMBI.



1. Kitambi Mvurugo -- hiki kitambi kimekaa kama O.
Kinapatikana kwa kula sana kitimoto.

2. Kitambi Mchuchumio -- hiki kitambi kimekaa kama
herufi D. Kinatokana na kula sana michemsho na bia za
ofa.

3. Kitambi Mbonyeo -- Akivua shati kitovu hakionekani.
Hiki wanacho wala rushwa. Ila akisimamishwa kazi
kinaisha.

4. Kitambi Mtepeto -- Ni kitambi cha wastani ambacho
ukivaa nguo pana
hakionekani. kinasababishwa na kula mno viporo.

5. Kitambi Mfumanio: hiki mtu anakuwa hana pesa ila
kitambi ni kutokana na minyoo na utapiamlo wa ukubwani.

6. Kitambi Mtunguo: Hiki wanacho sana wadada. Kina
umbo la yai. Hiki kwa 'diet' hakitoki labda Kwa Maombi tu.

Tuesday, April 29, 2014

DENI LA TAIFA LAFIKIA TRILION 40 IMF YAIONYA SERIKALI


 Jengo la benki kuu.
Jumapili iliyopita Gazeti dada la The Citizen liliandika habari ya kushtua katika ukurasa wa mbele, likielezea wasiwasi wa wataalamu na mabingwa kadhaa wa masuala ya uchumi kuwa, Tanzania inakabiliwa na janga kubwa la mzigo wa madeni iwapo Serikali haitapunguza kasi ya mikopo isiyokuwa na tija katika kuinua uchumi.
Onyo la wataalamu hao linatukumbusha jinsi janga la Deni la Taifa lilivyoligharimu Taifa kiuchumi katika miaka ya 90, ambapo karibu rasilimali zote ambazo Serikali ingezitumia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na pia kuziwekeza katika huduma muhimu za kijamii zilielekezwa katika kulipa madeni. Ni aibu na ukweli ulio mchungu kwamba ilipofika mwaka 2006, Deni la Taifa lilikuwa asilimia 70 ya Pato la Taifa, ingawa msamaha wa madeni ulipunguza kiwango hicho hadi asilimia 21 mwaka uliofuata.
Hata hivyo, kilichoendelea baada ya pale ni uthibitisho kwamba Serikali haikupata fundisho kutokana na janga hilo, kwani ilizidisha kasi ya kukopa kiasi kwamba Deni la Taifa hivi sasa linakadiriwa kuwa kati ya asilimia 40 na 50 ya Pato la Taifa, ambalo linakadiriwa kuwa Sh50 trilioni. Ni vigumu kuamini kwamba Deni la Taifa limekua kwa kasi ya kutisha kutoka Sh10 trilioni mwaka 2005 hadi Sh27 trilioni mwishoni mwa mwaka uliopita.
Kama baadhi ya wataalamu wa masuala ya uchumi wanavyohadharisha, suala hapa siyo Serikali kukopa, bali ni kwamba mikopo hiyo inayokadiriwa kuwa Sh2 trilioni kila mwaka inachukuliwa kufanya kitu gani? Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), zinaonyesha kwamba Deni la Taifa lilipaa kwa Tsh5 trilioni kati ya Januari na Oktoba mwaka uliopita.
Mtaalamu mmoja wa uchumi ametukumbusha jinsi miaka ya 70 Serikali ilivyokopa Sh96 bilioni kuanzisha Kiwanda cha Viatu Morogoro, lengo likiwa kuuza viatu nchini Italia. Kutokana na kufilisika kilibinafsishwa miaka ya 90 na hivi sasa majengo yake yamegeuzwa kuwa ghala, huku deni la uanzishwaji wa kiwanda hicho likiwa limelipwa kupitia kodi za wananchi. Mfano mwingine ni bajeti ya Sh122.4 bilioni ya kusambaza pembejeo za ruzuku kwa wakulima kwa mwaka 2011/12, ambapo Tsh89 bilioni zilikuwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imefichua uvundo na ufisadi mkubwa katika mfumo mzima wa pembejeo za ruzuku. Kwa hiyo, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inakutana leo kupokea na kujadili ripoti hiyo. Kwa mfano, katika Kijiji cha Lunyala, wilayani Nkasi, mkoani Rukwa asilimia 70 ya wananchi walioorodheshwa kupata mbolea walikuwa bandia, huku Benki ya Dunia ikikaririwa ikisema asilimia 60 ya Bajeti ya pembejeo za ruzuku ililiwa na mafisadi.
Kinachosikitisha ni kwamba Deni la Taifa litalipwa na wananchi wote ingawa waliofaidika nalo ni mafisadi na viongozi wachache walio serikalini na mashirika ya umma. Lakini kinachosikitisha zaidi ni tabia ya Serikali kuendelea kukopa kwa lengo la kuendeleza matanuzi na matumizi makubwa yasiyo ya lazima.
Mfano mzuri ni ziara fupi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki, ambapo aliongozana na ujumbe mkubwa kupita kiasi na magari ya kifahari ya Serikali yasiyopungua 30. Sisi tunadhani unahitajika mjadala mpana wa kitaifa kuhusu Deni la Taifa.
CHANZO; MWANANCHI.

ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA, KATA YA KAWE DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.

Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.

Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.

Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo

Mlezi wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo

 
Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014



Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis akimwelekeza jambo, Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Vincent Masawe wakati wa mkutano huo

Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Masawe akishukuru kwa kupewa ukamanda huo. Kushoto ni Sadifa akimsikiliza

Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe, Dar es Salaam, Aisha Kitundu (katikati) akiwa na Wasanii wa Kikundi cha TOT, Malkia wa Mipasho Nchini, Khadija Kopana na Jane Komba wakati wa mkutano huo

Viajana wa Kikosi kazi cha UVCCM Kata ya Kawe wakipozi kwa picha maalum ya kumbukumbu wakati wa mkutano huo.

Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare

 
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akiwa na viongozi wa Chipukizi, Nimka Lameck (Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa) na Maleo Motelo (Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni) baada ya uzinduzi wa Tawi UVCCM la Kawe, Mnarani, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma akizindua Tawi la UVCCM, Kawe Mnarani, DSar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.

Kamanda wa UVCCM Kawe, akitoa mchango wa sh. 200,000 kwa Ktb wa tawi la UVCCM Mnarani, Mlangala Zacharia kwa ajili mradi wa maendeleo ya tawi hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo

TBC NA CRI YAZINDUA TAMTHILIYA YA KICHINA ILIYOTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI


Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam


Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou akieleza jambo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe ikiwa ishara ya kukamilika kwa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia) wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam

Mshana akipewa zawadi

Wadaiu waliohudhuria

Wadau waliohudhuria




Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika leo

Monday, April 28, 2014

BASI LA SUMRY LAUA KWA KUGONGA WATU 13 AKIWEMO ASKARI WA USALAMA BARABARANI SINGIDA USIKU HUU

 
  WATU 13 akiwemo askari wa kikosi cha usalama barabarani wamepoteza maisha baada ya kugongwa na basi la kampuni ya Sumry lililokuwa likitoka Kigoma kwenda Dar katika kijiji cha Ikungi mkoani Singida usiku huu.
Ajali hiyo imetokea baada ya ajali ya kwanza iliyolihusisha lori lililomgonga mwendesha baiskeli aliyepoteza maisha papo hapo na wakati wananchi wakiwa wamekusanyika eneo hilo la ajali huku trafiki akiendelea kupima ajali hiyo, lilitokea basi la kampuni ya Sumry na kuwagonga watu hao pamoja na trafiki na kupelekea jumla ya watu 14 kupoteza maisha eneo hilo.
Basi hilo lililokuwa likitokea Kigoma kwenda Dar halikuweza kusimama eneo hilo mpaka dereva wake alipokwenda kujisalimisha kituo cha polisi Ikungi, Singida.
Miili 14 ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa mkoani Singida pamoja na majeruhi wawili waliopelekwa hospitalini hapo.
MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

MAMA SHUJAA WA CHAKULA WAINGIA RASMI KIJIJI CHA MAISHA PLUS PROFESA ANNA TIBAIJUKA


Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhudia Kukaribishwa Rasmi kwa Mama shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2012 Sister Anna Mwasu wa tatu kutoka kulia akiwa katika sherehe za kuwakaribisha mama Shujaa wa Chakula ambao  wameingia rasmi katika Kijiji cha Maisha Plus Jana.
Mwakilishi kutoka Forum CC Faidhari akizungumza jambo wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus.
Teresa Yates Mwakilishi kutoka OXFAM akitoa salama za Shukurani kwa wadau wote
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mh. Ahmed Kipozi akiwakaribisha Rasmi wageni wote katika Kijiji cha Maisha plus pia kumkaribisha Mgeni Rasmi Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi  ili aweze kutoa hotuba yake
Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa katikati akitoa hotuba yake fupi wakati wa Sherehe za kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Maisha Plus, katika Hotuba hiyo aliwapongeza waandaaji na wabunifu wa Shindano hilo, pia Grow kupitia OXFAM kwa kuungana na Maisha Plus kuwaleta Mama Shujaa wa Chakula, Mwisho aliahidi kuongeza Milioni 5 kwa Mama Shujaa wa Chakula atakaye nyakua ushindi, Kutoa Milioni mbili na nusu kwa Mama Shujaa wa Chakula aliyepita ili zikamsaidie katika kilimo na Mwisho Kutoa Milioni Mbili kwa Washiriki wa Shindano la Maisha Plus ambao sasa wamebakia 16 mpaka mwisho wa Shindano Tarehe 18.05.2014
Mmoja wa washiriki wa Maisha Plus akisoma Jina la Mama yake ambaye atakuwa naye katika Kipindi hiki kilicho bakia cha Shindano la Maisha Plus/ Mama Shujaa wa Chakula.

Vijana na Washiriki wa Maisha Plus wakiwa na Mama zao walezi ambao ndio wameingia Rasmi kijijini Jana
Huyu Ndiye Mama Shujaa wa Kwanza kupata nafasi ya Kuwa Markia wa Kijiji cha Maisha Plus Mary J. Mwanga, na wa kwanza kulia ni Rais wa Kijiji cha Maisha Plus Abisai Caron kutoka kenya hapa akiwa anavishwa kofia ya utambulisho na Epheta Msiga Meneja Miradi kutoka DMB

Mkurugenzi Mtendaji wa DMB ambao ndio waendeshaji wa Shindano la Maisha Plus/Mama Shujaa wa Chakula Ally Masoud(Masoud Kipanya) Akitoa utaratibu wa jinsi Akina mama Shujaa wa Chakula watakavyo ishi na vijana hao katika kijijni
Moja ya Bendi Matata kutoka Bagamoyo wakiwa wanatumbuiza nyimbo Nzuri wakati wa kuwakaribisha Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji Cha maisha Plus

Wakipokea maelekezo kadha wa kadha
MAISHA PLUS/ MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014

SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.

 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.

 
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.

 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.

 Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.

 Kikosi cha Wanamaji 

 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.

 Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .

 Maandamano ya Pikipiki.

 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .

Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.