Thursday, March 26, 2015

USIKOSE NAFASI HII HADIMU.





MESS ANAONGOZA KWA KULIPWA HELA NYINGI DUNINIANI AMZIDI RONALDO





Haya ndio majina makubwa zaidi kwenye soka kwa sasa.. Ushindani ni mkubwa huku wengine wakivutana kuufikia muafaka, eti nani mkali kuliko mwenzake, Ronaldo au Messi?

Mkongwe wa soka duniani Pele alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba kura ya nani bora kati ya mastaa hao, yeye angempa Messi!
Leo ishu sio ukali wao uwanjani, ripoti ya mwisho kutolewa na goal.com ilionesha kuwa Ronaldo anaingiza pesa nyingi zaidi kuliko Messi.. Ronaldo anaingia kwenye headlines za kukaa kwenye rekodi kubwa mbili alizoshikilia kwa muda mrefu, ikiwemo hiyo na rekodi ya uchezaji bora wa soka duniani.
Lakini unaambiwa kwa sasa mpinzani wake mkubwa Lionel Messi amemzidi na kutajwa kuwa ndiye mwanasoka anaelipwa pesa nyingi zaidi na Klabu yake ya Barcelona katika list ya wachezaji wa soka, Messi analipwa paundi milioni 26 zinatokana na mshahara huku nyingine zikitokana na dili za mikataba aliyoingia na makampuni mbalimbali.
Kwa sasa Messi anaingiza jumla ya pound milioni 47.8 (zaidi ya Bil. 129) ambapo anamzidi Ronaldo ambaye anapokea pound milioni 39.7 (zaidi ya Bil. 106 Tshs) kwa wiki.

Sunday, March 22, 2015

MVUA YASABABISHA AJALI MSIMBAZI CENTRE JIJINI DAR LEO


Watu wakishuhudia gari lililogongwa. Toyota Prado lililogonga gari dogo likishuhudiwa na wananchi.

AFANDE SELE NAYE AJIUNGA RASMI NA ACT


 
Zitto Kabwe, Afande Sele wakiwa na baadhi ya wanachama wapya wa ACT-Tanzania.

MSANII mkongwe wa Bongo Fleva nchini, Seleman Msindi 'Afande Sele' naye amejiunga rasmi na chama cha ACT-Tanzania.

Afande Sele akiongea na wanahabari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano ndani ya Hoteli ya Serena, Dar.
Afande Sele ambaye alikuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amejiunga na ACT-Tanzania leo wakati wa mkutano na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.…

HATIMAYE ZITO ZUBERI KABWE AHAMIA ACT- TANZANIA



Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT...

- Kumwaga ‘mboga’ mbele ya wandishi wa Habari Jumapili hii Machi 22.

Hayawi hayawi… Sasa yamekuwa! Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.


Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi
waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari
Jumapili ya Machi 22.

NB: ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.


Mwanachama rasmi wa ACT, Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.


“He..he he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi hiyo
kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi za chama cha ACT,
tawi la Tegeta.


Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya
kupokea kadi hiyo.


Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.


Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama
hicho mapema leo.


Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa leo.

Saturday, March 7, 2015

NMB IMEPATA PATA MKURUGENZI MPYA

2

Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wao mpya, Ineke Bussemaker ambaye anachukua nafasi ya Mark Wiessing ambaye amepangiwa kituo kingine cha Kazi ndani ya Benki ya Rabobank iliyopo Brazil.
1
Mkurugenzi mpya wa NMB, Ineke Bussemaker akisalimiana na   naibu gavana wa benki kuu ya Tanzania, Juma Reli
3
.

  Menejiment ya NMB, Bodi ya Wakurugenzi ya NMB wakiwa na Mark Wiessing

MBOWE AWASHA MOTO TABORA UWANJA WA TOWN SHOOOL.


umati wa watu wakifuatilia mkutano na Mh freeman aikael mbowe

ALLY KIBA AFANYA SHOW MOSHI



Mkoa wa kwanza kufikwa na tour ya Ali Kiba ni Kilimanjaro ambapo Moshi walipata nafasi ya kushuhudia show ya Ali Kiba kwenye stage na wimbo wa Cheketua kwa mara ya kwanza Club La Liga.
Show hii pia ilisindikizwa na Recho kutoka THT,kwa maelezo ya Ali Kiba mbali na kuiperfoam Chekecha kwa mara ya kwanza Moshi pia imekua mara ya kwanza kwake kuperfoam akiwa na live band Moshi

ABDU KIBA   Recho kutoka THT

CREDIT MILLARD AYO

MBUNGE WA KINONDONI AFIWA NA KAKA’KE, AZIKWA!


Mbunge wa Kinondoni (aliyesiamama kushoto), Idd Azzan akiwa nyumbani kwa marehemu.

Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu.
Wakina mama wakiwa msibani hapo.

MBUNGE wa Kinondoni, Mh. Idd Azzan amepata pigo kwa kufiwa na kaka yake, Azzan Mohamed usiku wa kuamkia leo aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la ini.Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwa kaka yake Magomeni-Somanga, jijini Dar, mbunge huyo alisema kifo cha kaka yake huyo ni pigo kubwa kwani alikuwa na msaada mkubwa kwake na kwa ndugu zake.
Alisema marehemu alisumbuliwa na tatizo la ini kwa takriban miaka miwili iliyopita ambapo katika kipindi chote hicho walijaribu kumpeleka katika hospitali mbalimbali jijini Dar kupatiwa matibabu lakini hali ilikuwa ikibadilikabadilika siku hadi siku.
Azzan aliongeza kuwa, marehemu kaka yake ndiye alikuwa kijana mkubwa katika familia na hata marehemu baba yao alipofariki, yeye ndiye aliyekuwa tegemeo kama kiongozi lakini naye Mungu amemchukua.
“Kifo cha marehemu kaka yangu kimeniuma sana maana kaka yetu baada ya kifo cha marehemu baba yetu ndiye aliyehakikisha tunapata haki zote za msingi katika familia,’’ alisema Azzan.Azzan Mohamed alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni na amezikwa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amina. (PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

Monday, March 2, 2015

MWILI WA KOMBA UKIWASILI KARIMJEE LEO


Mwili wa marehemu John Komba ukiingia Karimjee ili kuagwa na wananchi na viongozi mbalimbali.…

 


CHELSEA YATWAA UBINGWA WA CAPITAL ONE CUP


Kikosi cha timu ya Chelsea kikiongozwa na kocha wao, Jose Mourinho baada ya kutangazwa mabingwa wa Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup 2014/15 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wembley kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tottenham.

Sunday, March 1, 2015