Rais
Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya
kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza
Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi
MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya
siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi
wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda
amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita
kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na
hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.
Mwenyekiti
wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa
anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa
amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.
No comments:
Post a Comment