Monday, April 13, 2015

CHAMA KIPYA CHA SIASA CKUT CHAPATA USAJILI JIJINI DAR LEO


Mwenyekiti na Muasisi wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT), Ramadhani Semtawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata usajili wa muda wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam, Kushoto ni katibu Mkuu wa Chama hicho, Noel Antapa.

Mwenyekiti na Muasisi wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania (CKUT), Ramadhani Semtawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupata usajili wa muda wa chama hicho uliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti na Muasisi wa Chama cha Kijamaa na Uzalendo Tanzania, Ramadhani Semtawa akiwa ameshika katiba ya CKUT na Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Noel Antapa akiwa katika viwanja va Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa leo jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA)

THAMANI MJENGO WA DIAMOND PLATNUM BALAA


Mjengo wa Staa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ Madale nje kidogo ya Jiji la Dar.

Mjengo huo wa Diamond uliopo maeneo ya Madale nje kidogo ya Jiji la Dar, unadaiwa kufikisha thamani hiyo kutokana na kuwa na vyumba vinne vya kulala, bwawa maalum la kuogelea (swimming pool), sehemu ya mazoezi (Gym), jakuzi, kaunta ya vinywaji, ukumbi wa kuchezea, studio ya muziki, uwanja wa mpira wa kikapu na sehemu ya kuchezea mchezo wa mishale (Darts).

Kwa mujibu wa Diamond, nakshi za dhahabu alizoziweka katika kuta za bafu na chooni pekee, zimemgharimu sh. mil. 70 kitu kinachoendana na utabiri wa mkandarasi huyo kuwa nyumba hiyo inafikia thamani ya zaidi ya sh. mil. 400.

Jikoni.
Akiuzungumzia mjengo huo baada ya kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani umechukua nafasi kubwa, na ‘material’ yaliyojengea ni ya gharama.

”Ukitazama kwa makini, material nyingi zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea,” alisema mkandarasi huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

MANUNITED YAIADHIBU MAN CITY


 
Baada  ya kuonewa kwa muda mrefu na majiraji zao katika ligi kuu ya England, hatimaye leo jiji la Manchester limepakwa rangi nyekundu baada ya kuisha kwa mchezo kati ya Manchester United vs Man City.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde katika dimba la Old Trafford umeshuhudia Man United wakirudisha utawala wao dhidi ya City kwa kuwapa kipigo cha magoli 4-2.
Magoli ya City yalifungwa na Sergio Aguero yote mawili, na huku United yao yalifungwa na Ashley Young, Juan Mata, Maroune Fellaini na Chris Smalling.
Chelsea wao walicheza mchana na QPR na kushinda 1-0, goli la Cesc Fabregas.
Manchester United watasafiri kuelekea Stamford Bridge wikiendi ijayo kucheza na Chelsea.
MSIMAMO WA LIGI ULIVYO
  

PICHA ZA ANDY MURRAY!! STAA WA TENISS DUNIANI ALIVYOFUNGA NDOA


harusi2

Ukiachilia mbali Staa wa mchezo wa tenis duniani Serena Williams kuna huyu mwingineAndy Murray ambaye naye ni miongoni mwa mastaa wanaofanya vizuri katika mchezo huo duniani.
Andy Murray sasa ameingia kwenye ukurasa mpya wa maisha baada ya kufanya uamuzi wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Kim Sears.
Katika harusi hiyo ya kifahari iliyofanyika nyumbani kwao Uingereza, ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wachezaji wenzake sambamba na vyombo vya habari ambavyo vilifanikiwa kuchukua tukio zima.
Moja ya vitu ambavyo vilivutia harusi hiyo ni pamoja na jinsi bwana harusi Murray alivyokuwa amevaa jambo ambalo si rahisi kukutana nalo kwenye harusi nyingi.
harusi
harusi2
harusi3
harusi4
harusi5

Saturday, April 4, 2015

REGNALD MENGI AFUNGA NDOA NA JACKLINE NTUYABALIWA

 

Germany France Plane Crash 
Ndoa imefungwa miezi minne baada ya Reginald Mengi kumchumbia Jackline Dubai kwenye siku ya kuzaliwa ya mrembo huyu December 2014.
Mengi na mke wake Jackline


Germany France Plane Crash



Hii ndoa pia ilishuhudiwa na watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.

Wakifunga ndoa harusi hii ambayo imefungwa kwenye ardhi ya nchi ya Mauritius kwenye mwisho wa mwezi March 2015.
CHANZO BONGO 5