Friday, August 15, 2014

MKE WA AFANDE SELE MAMA TUNDA AFARIKI DUNIA


Screen Shot 2014-08-14 at 11.10.46 AMMsanii wa longtime kwenye bongofleva Afande Sele amewajulisha watu wake wa karibu na mashabiki kuhusu msiba uliomkuta kwa kufiwa na mama wa wanae.
Kupitia ukurasa wa facebook Afande Sele aliandika “Ndugu zangu!! Nimefiwa na mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. Sisi ni waja wa mwenyezi mungu na hakika kwake tutarejea; mungu ampumzishe pema.”
Screen Shot 2014-08-14 at 11.12.56 AM
Kutoka kulia ni Marehemu Asha, Afande na watoto wake Asante na wa mwisho kushoto ndio Tunda.

AFANDE 
R.I.P Asha.

DIMOND ASHINDA TUZO NCHINI BURUNDI

dd
Story  kuhusu ujumbe mrefu aliondika Diamond kupitia ukurasa wake wa facdebook
Diamond kushinda award ya wimbo bora wa East Africa na wimbo wa Number One. Award hiyo imetolewa nchini Burundi kwenye TTTMAwards.


diamond3

DIAMOND AWAPIGA VIJEMBE MA FANC WOTE WA WEMA SEPETU




STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amemtupia vijembe mpenzi wake Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram usiku huu akionekana kuchukizwa na tabia ya staa huyo kupenda maisha ya starehe zisizo na faida.



Diamond Platnumz.

Katika ujumbe huo, Diamond ameandika kuwa angewaona mashabiki wa mrembo huyo wana akili na mapenzi ya dhati kama wangemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na kuacha starehe zisizo na faida na kutumia fedha kufanya mambo ya maendeleo kuliko kuvifaidisha viwanda vya kutengeneza pombe.

Wema Sepetu.

USOME UJUMBE HUO HAPA CHINI:


WASANII WATINGA KASIBANTE FM KUFANYA MAHOJIANO, KUKINUKISHA LEO



Dj Slay akiendesha kipindi cha mahojiano na wasanii wanaotarajia kupanda jukwaani leo kwenye Tamasha la Srengeti Fiesta 2014 Bukoba wakiwa wanamsikiliza kwa makini wakati wa Maswali na majibu kutoka kwa wananchi ndani a Studio za Kasibante Fm 88.5.
Wasanii wa Bongo flava wakiendelea kufanya mahojiano na mtangazaji wa Kasbante Fm, Dj Slay.

Msanii wa Bongo Fleva, Madee akijibu maswali ya wasikilizaji kupitia Kasibante FM.


Mr. Blue na Christian Bella wakifurahia jambo.


Barnaba akisikiliza jambo.


Jux, Ney wa Mitego na Mr. Blue wakiwa katika pozi.


Mr. Blue akijibu maswali ya wasikilizaji kupitia Kasibante FM.


Mtangazaji wa Radio Kasibante FM 88.5, Dj Slay akiendesha kipindi hicho.

Wasanii wa Bongo Fleva , Linah akiwa na Recho

Sunday, August 10, 2014

JINSI FIESTA ILIVYOFANYIKA MWANZA NI SHIIIIIDAAA!!!!!!!!


Mwanza umekua ndiyo mkoa wa kwanza kufungua shamra shamra hizi za Fiesta kwa mwaka 2014 ambapo on stage zaidi ya wasanii 15 walipata nafasi ya kushow love na wakazi wa Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Inawezekana show hii ikaingia kwenye list ya miongoni mwa show zilizowahi kuhudhuriwa na wakazi wengi sana wa jiji hili la Mwanza kwa sababu nilipata taarifa kuwa ilipofika saa 5 tu usiku tiketi zote zilikuwa zimeisha.

 
Ukiachilia mbali wasanii waliokuwa wakitajwa kwenye matangaazo kulikuwa na SAPRAIZ nyingine kwenye jukwaa la Fiesta,Mwanza walimuona Jokate akiimba kwa mara ya kwanza kwenye jukwaa na kushangiliwa sana kutokana na alivyoifanya show hiyo.

Ratiba ya Serengeti fiesta baada ya Mwanza ni wakazi wa Bukoba na Kahama itakua zamu yao kuonja utamu wa Serengeti Fiesta na kwa miji hii miwili itakua ndiyo mara ya kwanza wanaiona,kwa Bukoba ni August 15 wakati Kahama ni August 17.

Hizi ni baadhi ya picha za usiku huu ulivyokuwa.