Monday, June 30, 2014

DIMOND AKISALIMIANA NA NELLY KWENYE TUZO ZA BET


n1 
Tukio la BET awards 2014 limefanyika na mambo mbalimbali yalitokea, zaidi ya interview kwenye redcarpet Diamond amekutana na wasanii tofauti. Hivi sasa ameshare picha zake akiwa na msanii Nelly wakionekana kwenye mazungumzo na salamu. Hayo yote yametokea kwenye redcarpet ya BET usiku wa kuamkia leo 30/6.

MSAJI WA VYAMA AMPIGA STOP MBOWE NA DR SLAA KUOMBEA UONGOZI CHADEMA



Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi.
Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imesema haitambui kuondolewa kwa kipengele cha ukomo wa uongozi uliofanywa na Chadema bila kufuata idhini ya mkutano mkuu wa chama hicho.
Mwaka 2006, Katiba ya Chadema ilifanya marekebisho yaliyoruhusu wanachama kugombea uongozi bila ukomo wakati awali, waliruhusiwa kugombea kwa vipindi viwili vya miaka mitano.
Barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema, inasema kipengele hicho katika Ibara ya 6.3.2 (C) kiliondolewa kwenye katiba bila idhini na mkutano mkuu wa chama hicho. Mutungi alisema baada ya kupitia muhtasari wa kikao cha mkutano mkuu wa mwaka 2006 suala la kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi halikuonyesha kujadiliwa katika mkutano huo.
Hata hivyo, akizungumza kwa simu jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema kipengele hicho kiliondolewa kwa vikao vya chama ambavyo ni wilaya na mkoa.
“Mjadala kuhusu ukomo wa uongozi ulishamalizika na haujadiliwi tena, ulishapitishwa na vikao halali vya chama, mkutano mkuu ulipitisha yale yaliyoamuliwa na vikao vya chini,” alisema Dk Slaa.
Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema: “Chadema wamefanya mabadiliko bila kufuata katiba”
Alishauri waitishe mkutano rasmi na halali kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ili waweze kurekebisha kasoro zilizopo.
Alisema kama chama hicho hakitarekebisha kasoro hiyo, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa haiwezi kuitambua ibara hiyo.
Alisema ingawa hoja hiyo iliwasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba ambaye sasa si mwanachama wake, bado hoja hiyo ni muhimu na inahitaji kufanyiwa kazi.
“Ni vizuri mkaifanyia kazi hoja hiyo bila kujali kwamba aliyeiwasilisha si mwanachama tena wa Chadema,” alisema katika barua hiyo
chanzo mwananchi

Saturday, June 14, 2014

GEORGE TYSON AZIKWA LEO KIJIJINI KWAO SIAYA,NCHINI KENYA


 Hapa ndipo mwili wa Marehemu George Tyson ulipozikwa mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.George Tyson ambaye alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini Tanzania,alifarika kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma kikazi akirejea jijini Dar.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amin.
Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
Ndugu na jamaa mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu George Tysombani kwako,katika kijiji cha Siaya nchini Kenya.
Baadhi ya Ndgu na Jamaa mbalimbali wakiwa kwenye maombolezo ya mwisho ya mazishi ya marehemu George Tyson mapema leo mchana,nyumbani kwao
Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
Mdau Felix akizungumza jambo na kuwashukuru Watanzania wote na wengineo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha mpendwa wao,ambaye Mwenyezi Mungu kampenda zaida anaenda kuishi kwenye nyumba yake ya milele.
Watoto wa marehemu George Tyson wakiwa katika picha ya pamoja.

Nyumba ya milele ya marehemu George Tyson kabla ya kulazwa.Picha kwa hisani kubwa ya Mdau William Mtitu kutoka kijiji cha Siaya,nchini Kenya

Friday, June 13, 2014

BRAZILI YASHINDA 3 DHIDI YA CROATIA


Neymar alifunga mabao mawili Brazil iipoilaza Croatia 3-1
Wenyeji wa kombe la dunia Brazil walitoka nyuma na kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua fainali ya dimba la mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo (Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki 65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22 aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika baada ya refarii kutoka Japan
Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni yao hayakusikika

Thursday, June 12, 2014

SOKO LA MACHINGA KARUME LATEKETEA


 Soko Maarufu la Mitumba Karume jijini Dare es Salaam limetekea kwa moto ambao mpaka sasa haujajulikana chanzo chake. Moto huo ambao unasemekana ulianzia majira ya jana usiku saa tatu umeteketeza mali za mamilioni ya shilingi na kuacha wafanya biashara wengi kwenye wakati mgumu.
 Moto ukiendelea kuunguza mabati yaliyosalia.
 Kila kitu kimeungua.
Watu wakiokoteza mabati
Mabango ya Matangazo ya Biashara yakiwa yametekea pia.

WAZIRI: TUWAEPUSHE VIJANA WETU NA UHAFIDHINA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,  akifunguza majadiliano  kuhusu mazingira yanayochangia kuendenea kwa vitendo vya  kigaidi.  majadiliano hayo yamefanyika siku ya  Jumatano yakitangulia mkutano wa nne utakafanya tathmini kuhusu Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibidi Ugaidi.  Katika salamu zake, Katibu Mkuu amesema hakuna sababu iwayo yoyote ile  inayoweza kuhalalisha ugaidi.  Kulia kwake ni Rais wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa Bw, John Ashe .
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe.  Pereira Silima ( Mb) akichangia majadiliano hayo. Naibu  Waziri anaongoza ujumbe wa Tanzania.  Katika  mchango wake amesema kuna kila sababu ya  kuhakikisha kuwa vijana hasa wale wasiokuwa na  ajira hawashawishiki kujiunga na uhafidhina na kwamba kutoka na changamoto mbalimbali zikiwamo za ukubwa wa mipaka baina ya nchi na nchi, tishio la ugaidi na uhafidhina kwa nchi za Afrika Mashariki ni kubwa.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu  ukiongozwa na Naibu Waziri Silima walioketi  nyuma ni  Bw.  Abdalla Khamis  Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu na    Bw. David Hiza. Kamishna Msaidizi wa  Jeshi la Polisi na  Mratibu  Kituo cha Kitaifa cha  Kuratibu Mapambano dhidi ya Ugaidi.
Wajumbe ukumbini

MAPIGANO MAKALI YATOKEA KWA SIKU MBILI KATI YA DRC NA RWANDA


Mapigano yameendelea kwa siku ya pili kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wale kutoka Rwanda kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Milio ya risasi iliyodumu karibu saa mbili iliripotiwa kusikika mapema Alhamisi.
Pande hizo zimekuwa zikishutumiana kwa kuanza mapigano.
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa vikosi vya Rwanda viliingia Mashariki mwa Congo, kumteka nyara na kumuua mwanajeshi wake, huku nayo Rwanda ikisema kuwa wanajeshi wa Congo ndio walioingia nchini mwao na kuwafyatulia risasi.
Makabiliano yalianza Jumatano katika kijiji cha Kanyesheza, kilomita 20 kutoka Goma mji mkuu wa mkoa huo na kudumu kwa saa kadhaa.
Wanajeshi hao walishambuliana kwa zana nzito za kivita, asubuhi na mapema kwa mujibu wa mmoja wa walioshuhudia makabiliano hayo.
Pande hizo mbili zimekuwa zikilaumiana huku afisaa mmoja wa Rwanda akidai kuwa wanajeshi wa DRC ndio waliowashambulia kwanza.
Hata hivyo duru zinasema kuwa hapakuwa na majeruhi ingawa wanajeshi walikuwa wanafyuatuliana risasi kiholela. Makabiliano ya leo yamezuka baada ya pande hizo mbili kushambuliana Jumatano

SOKO LA KARUME LA TEKETEA KWA MOTO USIKU WA LEO

 


Mabanda ya wamachinga eneo la Soko Karume yanaungua na moto.

Habari zaidi zitafuata.

Moto bado ni mkali, unazidi kusambaa na sasa unaelekea Breweries. Usipodhibitiwa mapema utaleta athari kubwa sana.

Hali bado ni tete, Fire walifika katika eneo la tukio na sasa wanaondoka bada ya kukubali kushindwa, hakuna wanachoweza kuokoa.

Nguzo za umeme zinaungua pia.

Kuna umati wa watu mkubwa, baadhi wanalia kwa uchungu wakiwa wamejishika kwa kukata tamaa.

Chanzo kinadaiwa kuwa ni sehemu ya "Mama Ntilie" (ambao inasemekana huchemsha maharage na kuyaacha usiku ili yaive vizuri)

 PICHA hizi zimepigwa na mwandishi wa JamiiForums:




DR WIIBROAD SLAA SITAGOMBEA URAISI 2014




Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa

DK. Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais 2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu kitafanywa kwa wakati muafaka,kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.
Akizungumzia hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, niaheshimu uamuzi wa Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.
UKAWA imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la rais,serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.
Serikali ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph Warioba."

Chanzo:Mtanzania

Wednesday, June 11, 2014

KUTANA NA KASA ALIYEITABIRIA BRAZIL KUIFUNGA CROATIA KESHO


Kasa aitwaye Big Head akitabiri mechi ya kesho ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia.

BAADA ya pweza Paul aliyekuwa akiishi Ujerumani kujizolea umaarufu wakati wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, fainali za mwaka huu nchini Brazil ameibuka mtabiri mwingine aitwaye Cabeção au Big Head.
Big Head ambaye ni kasa mwenye umri wa miaka 25, anayeishi katika kijiji cha Praia Do Forte nchini Brazil ameitabiria nchi yake ya Brazil kuibuka na ushindi katika mechi ya ufunguzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Croatia kesho.
Big Head ameanza kazi yake hiyo jana, Jumanne kwa kutabiri mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia. Kasa huyo anafanya utabiri kwa kuchagua vyakula.…

TFF YAPANGUA PINGAMIZI LA WAMBURA, MSIMBAZI MASHABIKI WAFURAHIA!


Shabiki wa Simba akifurahi kwa kuonyesha Katiba ya Simba.



Mashabiki wa Simba wakionesha furaha yao klabuni Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo.

Ilikuwa ni pata-shika nguo-kuchanika na pongezi motomoto kwa shujaa wao Wambura.

Sherehe za kumpongeza Wambura zikiendelea.

Chereko za kufa mtu zikiendelea mchana huu.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetupilia mbali pingamizi lililowekwa na wanachama wa Simba na kumruhusu mgombea wa nafasi ya urais katika klabu hiyo, Michael Wambura kuendelea na mchakato huo.
Mwenyikiti wa Kamati ya Rufaa wa TFF, Julius Lugazia alipotangaza rufaa hiyo alisema Wambura ni mwanachama halali wa Klabu ya Simba kisheria hivyo anayo haki ya kugombea nafasi hiyo kama wagombea wengine kwani amekuwa akishirikishwa katika kamati mbalimbali huku mchango wake wa kimawazo ukitumika ndani ya klabu hiyo
Mashabiki wa Klabu ya Simba ambao ni wafuasi wa Wambura, walipokea taarifa hiyo ya TFF kwa mikono miwili na kushangilia kwa staili ya kipekee kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi kwa kufurahishwa na maamuzi hayo.

(Picha na Stori Deogratius Mongela GPL)

ALIYEPIGA PICHA NA MH; KOMBA AJITOKEZA NAKUSEMA HAYA


 
Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar anayedaiwa kupiga picha tata na mheshimiwa Komba.
SIKU chache zimekatika baada ya tukio la kusambaa mitandaoni kwa picha tata zenye pozi kati ya mheshimiwa Komba na mrembo aliyejulikana kwa jina moja la Angel.
Hatimaye mrembo huyo ameibuka na kuanika mambo mazito kama si makubwa, Risasi Mchanganyiko linakudadavulia.

Awali katika gazeti hili toleo la Jumamosi iliyopita ukurasa wa mbele kulikuwa na habari hiyo ikiwa na kichwa; KHAA! KOMBA! Katika habari hiyo picha zilizomuonesha mheshimiwa Komba akiwa na mrembo huyo zilipamba ukurasa huku mwenyewe (Komba) akidai ni picha za kutengeneza).

OFM YAINGIA MITAANI
Kwa vile Komba alikataa picha si zake huku baadhi ya vyombo vya dola kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) vikitangaza kuingia kazini kumtafuta sosi wa picha hizo, ilibidi timu makini ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kutoka Global Publishers iingie kazini kumsaka mrembo huyo kwa udi na uvumba.

Mheshimiwa Komba.

YATUMIA NUSU SIKU
OFM ambayo huwa haishindwi kitu, ilitumia nusu siku ya Ijumaa iliyopita na kufanikiwa kuinasa namba ya simu ya mkononi ya Angel pamoja na picha nyingine ikiwepo iliyotumika ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Aidha, ilibainika kwamba, mrembo huyo anaitwa Angel Kissanga, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, bila ajizi Paparazi wetu alimwendea hewani Angel na kumuuliza kama ana habari zozote kumhusu yeye.
Angel: “Habari kama zipi? Mimi sina habari zozote.”

Paparazi: “Hujaona kwenye mitandao ya kijamaii wameweka picha zako ukiwa katika mapozi tata na mheshimiwa Komba?”
Angel: “Ngoja kwanza, nitakupigia.”

MUDA UNAKWENDA, ANGEL ARUDIWA
Baada ya kuona muda unakatika bila mrembo huyo kupiga simu kama alivyokuwa ameahidi, paparazi wetu alimrudia hewani ambapo safari hii simu yake ilipokelewa na mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni dada wa Angel.

 
Angel Kissanga katika pozi na mheshimiwa.

“Mimi si Angel, ni dada yake. Angel amepandwa na presha baada ya wewe kumwambia kuna picha zake na mheshimiwa Komba kwenye mitandao.
“Unajua ngoja nikuambie ukweli. Mdogo wangu ameshtuka sana, hivi hapa tupo Hospitali ya Micco Sinza, amelazwa.”

PAPARAZI ATIA TIMU HOSPITALINI
Kusikia hivyo, paparazi wetu alifunga safari hadi kwenye hospitali hiyo ambapo kweli mrembo huyo alikuwa amelazwa kwa matatizo ya presha ya kupanda.

Mwanamke aliyejitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Angel alimjia juu paparazi wetu akidai yeye ndiyo chanzo cha mwanaye huyo kupandwa na presha ghafla, akamtimua asimuone mgonjwa.

MAZUNGUMZO YA BAADAYE
Siku iliyofuata, paparazi alibahatika kuzungumza na Angel ambaye aliweka wazi mambo yake kuhusu picha hizo kama ifuatavyo:

“Mimi nataka kusema kwamba picha nimeziona, nazifahamu kweli ni mimi.”
Paparazi: “Ni kweli ulipigwa ukiwa na mheshimiwa Komba?”
Angel: “We jua tu kwamba picha nazijua. Zilipigwa na simu ya LG.”
Paparazi: “Alipiga nani?”

Angel: “Nimesema nazifahamu.”
Paparazi: “Hiyo simu ni ya nani?”
Angel: “We wa nini?”

Angel Kissanga.

Paparazi: “Okey, mheshimiwa Komba unamfahamu?”
Angel: “Namfahamu ndiyo.”
Paparazi: “Ni nani wako?”

Angel: “Nimekwambia namfahamu.”
Paparazi: “Sasa mbona mheshimiwa Komba anasema picha zimetengenezwa?”
Angel: “Mimi sijui sasa.”

ANGEL ATAKIWA KUTIA TIMU GLOBAL
Baada ya mazungumzo hayo, paparazi alimtaka msichana huyo kufika kwenye ofisi za magazeti ya Global ambapo alikubali.

Hata hivyo, baadaye alisema amebatilisha baada ya baba yake kuingilia kati sakata la picha hizo akidai yeye ndiye atakuwa msemaji mkuu.
Habari za chini kwa chini zilidai kwamba, kusita kuweka miguu kwa Angel kwenye ofisi za Global kulitokana na zuio la mheshimiwa mmoja ambaye alimchimba mkwara kwamba asitoe ushirikiano wowote na vyombo vya habari.

MASWALI MUHIMU
Maneno ya Angel na mheshimiwa Komba yanapingana. Mmoja anasema picha zilitengenezwa, mwingine anazitambua na zilipigwa kwa simu ya LG, nani mkweli? (endelea kufuatilia Magazeti Pendwa ya Global Publishers).

ANATAJWA PAULINA
Mbali na kupishana kwa maneno ya wawili hao, mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Paulina anatajwa kuwa nyuma ya sakata hilo.

Mwanamke huyo anadaiwa wakati fulani kuingia kwenye mzozo na Angel na akaja kudai ameipata simu yenye picha za mrembo huyo na mheshimiwa bila kujulikana alikoipata. Je, aliipata kwa Angel au mheshimiwa Komba? (endelea kusoma magazeti ya Global).

Ni mzozo gani aliokumbana nao Angel kwa Paulina? Unaweza kuwa wa wivu wa mapenzi? Na kama ni wivu wa mapenzi walikuwa wanamgombea nani? (Endelea kusoma magazeti ya Global).



UTATA KUHUSU KOMBA
Katika mahojiano na Risasi, Komba alipopigiwa simu kwa mara ya kwanza, Alhamisi mchana wa saa 7 baada ya kutoka bungeni, kabla ya kuelezwa sababu za kupigiwa simu, alijibu anajua alichopigiwa simu. Alijuaje?

Aidha, Komba alisema anazijua zile picha lakini yule msichana hamtambui. Kivipi? (Endelea kufuatilia magazeti ya Global).
Komba alisema anazo picha nyingine akiwa kwenye pozi la kawaida bila yule msichana, alipotakiwa kuzituma kwa mwandishi ili ajiridhishe, alikataa! Kwa nini? (Usikose kuendelea kutufuatilia).

Achana na maneno ya kwenye mitandao ya kijamii, Komba alipohojiwa na kituo kimoja cha redio, Ijumaa asubuhi, akasema anajua zile picha zimetengenezwa na wabaya wake, lakini akasema anamwachia Mungu. Kwa nini amwachie Mungu jambo zito kama hilo?

MAGAZETI YA GLOBAL
OFM ni kitengo rasmi, makini kilicho ndani ya Global. Hakijawahi kushindwa. Kimefichua uovu mwingi sana unaofanyika kwenye jamii. Kwa hili la Komba na Angel, ni dogo sana. Tunaahidi kuendelea kufuatilia na tutaanika ukweli halisi wa kila kinachoendelea.

Magazeti pendwa ya Global ni Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi na Risasi. Hakikisha hukosi nakala yako. Tutakuwa wa kwanza kukuhabarisha ukweli halisi pengine kabla hata ya vyombo vya dola venye kila aina ya vifaa.
CHANZO GPL

NEY WA MITEGO ANUNUA GARI MPYA PICHA HIZI HAPA

IMG_0514 
Mastar mbalimbali wa Tanzania wamekua wakionyesha magari yao ambayo mengi yamekua ya kifahari,kwa mwaka 2014 ni mwaka unaonyesha wasanii wengi kumiliki magari ya gharama zaidi,mpaka sasa ni zaidi ya wasanii watano ambao wameonyesha magari yao ya kifahari.
Star wa single mbalimbali ikiwemo Nakula Ujana Ney wa Mitego nae yupo kwenye list ya wasanii wanaomiliki magari haya ya thamani hii ya Ney wa Mitego ni Nissan Morano ya mwaka 2007 na hii inakamilisha gari la pili kwenye kipindi kifupi baada ya ile Toyota Mark X.
Kwa maelezo ya mwenyewe Ney ingawa hakutaka kutaja bei kamili aliyonunulia lakini kasema ni zaidi ya Milioni 35 za Kitanzania,na hii aliinunua kama zawadi kwake siku ya June 09 alipokua anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

IMG_0539 

IMG_0534 

IMG_0521 

IMG_0520 

IMG_0510 

IMG_0515

Tuesday, June 10, 2014

MKENYA DIVORC ORIGI KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA CHINI BRAZIL

Divorc Origi ni mkenya na mwanaafrika mashariki wa kwanza kushiriki kombe la dunia
Mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa , Mkenya Divorc Origi ambaye ni mzaliwa wa Ubelgiji ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya taifa ambayo imeondoka Jumanne kuelekea Brazil kwa mashindano ya kombe la dunia kuanzia Alhamisi wiki hii.
Origi, mwanae Mike Okoth, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars atakua mchezaji wa kwanza wa Afrika Mashariki kuiwakilisha Ubelgiji, na yuko pamoja na wachezaji nyota kama vile Vincent Kompany wa Manchester City na Eden Hazard wa Chelsea.
Watakabiliana na Algeria mechi yao ya kwanza ya kundi H Juni tarehe 17 na siku tano baadae wanapepetana na Urusi kisha Korea Kusini kwenye mechi za mchujo.
Akizungumza na BBC kwa njia ya simu akiwa Ubelgiji Origi anasema:'' Algeria ni timu yenye wachezaji wazuri kwa hivyo hatuwezi kuidharau. Tutacheza mchezo wetu wa kawaida lakini nina matumaini makubwa tutashinda.’’ Anasema Urusi na Korea pia si timu hafifu hasa Warusi. Lengo lake kubwa ni Ubelgiji kufuzu kwa raundi ya pili kisha kutoka hapo anasema mambo yatakuwa sawa kabisa.
Kuhusu mbona ameamua kuiwakilisha Ubelgiji na sio taifa la babake Kenya, Origi anasema alitilia maanani mambo mengi kama vile usimamizi mzuri wa kandanda nchini humo, mizizi yake ya kandanda iliyoko huko, marafiki, ushauri wa babake pamoja na Ubelgiji kufuzu kwa kombe la dunia kwani haijulikani ni mwaka upi Kenya itafuzu kwa kombe la dunia.

DIAMOND AFANYA KOLABO NA MAFIKI ZOLO SOUTH AFRIKA

2
Hapa ni kwenye gari safari ya kuelekea studio ndio inaanza, Mameneja Bab Tale kushoto na Salam kulia pembeni na Diamond
Hatimae mpango wa Mafikizolo wa South Africa ambao ni mastaa wa hit single ya ‘khona’ waliochukua tuzo mbili kwenye MTV Africa music awards 2014 kufanya kolabo na Diamond umefanikiwa kwenye usiku wa June 9 2014.
Diamond pamoja na mameneja wake wawili ambao ni Salam na Bab Tale waliongozana mpaka kwenye studio za msanii mkongwe aitwae Oskido ili kurekodi kolabo hiyo ya Mafikizolo, kundi la Afrika kusini lililorudi kwenye chati kupitia mikono ya Oskido.
3
Ndio tunawasili kwa Oskido, mtu wako wa nguvu nilikuepo kuhakikisha kila kinachotokea kinakufikia
Kama hukusikiliza Clouds FM Top 20 Jumapili ya June 8 2014, wakati wa kufanya mazoezi ya tukio la MTV kwenye tuzo za Mama Durban South Africa June 7 2014, Mafikizolo waliomba kurekodi wimbo na Diamond baada ya kushawishika kufanya nae kolabo hivyo wakaahidi kushughulikia gharama zote za kumuongezea Diamond muda wa kuendelea kukaa South Africa pamoja na kubadili ticket ya ndege ili wakamilishe kazi yao.

9
Oskido ni msanii mkubwa sana na mwenye uwezo hapa South Africa na anapendwa sana ila pamoja na ukubwa wa jina lake, huwa hajiweki juu kabisa… ni mpole na simple kila wakati, nakumbuka hapa yeye ndio aliomba kupiga picha na Diamond.
8
Diamond alipoingia studio alikua bado hajapewa topic ya wimbo, yani alikua hajui wimbo unahusu nini ila dakika kadhaa baadae akaanza kushusha mistari yake… alipoingia kuingiza voco ya kwanza Mafikizolo pamoja na Producer wakampigia makofi na kusmile kuashiria kijana katishaa.



Mafikizolo na Diamond
14
Upande mwingine ambao wengi hawaujui, Diamond ni mtani na anachekesha sana, ana aina yake ya kuhadithia kitu mpaka ukacheka… ilikua goodtimes studio kiukweli
CREDIT MILLARD AYO.

Monday, June 9, 2014

KATIBU MKUU WA CCM, KINANA AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA NCHINI BI. DIANNA MELROSE


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimkaribisha kwa furaha, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Dianna Melrose, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam,  leo June 9, 2014.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Balozi  huyo wa Uingereza hapa nchini, Dianna Melrose, wakipena mikono kabla ya kuanza mazungumzo yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, June 9, 2014.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Dianna Melrose, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam