Monday, March 31, 2014

PICHA ZA RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOKUTANA NA WATANZANIA UINGEREZA



Mhe. Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mkewe mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali wa kitaifa kwenye mkutano wa Watanzania nchini Uingereza siku ya Jumapili March 30, 2014 katika ukumbi wa uwanja wa Wembley.

Mhe. Rais Jakaya Kikwete pamoja na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernard Membe wakipitiapitia mambo mawili matatu kwenye karatasi zao kabla Mhe. Rais Jakaya Kikwete hajazungumuza na Watanzania nchini Uingeraza siku ya Jumapili March 30, 2014 katika ukumbi wa uwanja wa Wembley.
Mama Salma Kikwete akiwa meza kuu alipokuwa kwenye mkutano wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete alipozungumuza na Watanzania nchini Uingereza siku ya Jumapili March 30, 2014. katika ukumbi wa uwanja wa Wembley.

JK akiwa London amesema maamuzi ya wananchi ndiyo yatakayoheshimiwa kwa sababu kama wananchi wataamua basi CCM wajiandae hizo serikali tatu.

Pia amesema alishawashauri CCM kwenye vikao vya ndani wajiandae kupokea hiyo serikali tatu kama wananchi wataamua
Mhe. Rais Jakaya Kikwete akiongea na Watanzania nchini Uingereza siku ya Jumapili March 30, 2014.

Watanzania na viongozi mbalimbali wa kitaifa wakifuatilia hoyuba ya Mhe. Rais Jakaya Kikwete alipokua akiongea na Watanzania nchini Uingereza.

 
katikati waziri wa uchukuzi Mwakembe.

Hussen Mwinyi, Sospeter Mhongo nawaziri wa feza

 

Baazi ya mawaziri  na Manaibu aliongozana nao


 
Raris akiwasili.


Anatoasalam kwa watanzania waishio Uingereza.

 


 
Waandishi wahabari nao walikuwa wengi
 



Rais akiwahuhubia
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na miongoni wa watanzania waishio Uingereza.

HAYA NDIO MAKUNDI YA SANAA YALIYOPIGWA STOP NA BASATA KUTOA BURUDANI KATIKA MISS TANZANIA!



BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limeitaka Kamati ya Miss Tanzania kutohusisha burudani zinazokiuka maadili ya Mtanzania wakati wa mashindano yao mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kikao cha tathmini ya mashindano ya Miss Tanzania 2013 kilichofanyika kwenye ukumbi wa baraza hilo, Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Idaya ya Ukuzaji Sanaa Basata, Vivian Shalua, alisema kuwa, maadili ni muhimu kuzingatiwa katika mashindano hayo ili kuepukana na dhana potofu kuwa, yanahusiana na uhuni.
“Maadili yazingatiwe katika mashindano ya mwaka huu, kuanzia kwa washiriki hadi burudani zitakazohusishwa, kama ‘vigodoro’, ‘kanga moja mbendembende’ na nasikia siku hizi kuna ‘tisheti ndembendembe’,” alisema mkurugenzi huyo.

Alisema kuwa, Basata ipo tayari kuyapigania mashindano ya Miss Tanzania kuhakikisha yanakuwa katika ubora wa hali ya juu, kwa kushirikiana na Kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji.

Mkurugenzi huyo pia aliitaka Lino kuwaelimisha mawakala wanaoandaa mashindano hayo juu ya umuhimu wa kuwa na vibali kutoka Basata, ikiwa ni pamoja na kutowavumilia watovu wa nidhamu bila kujali ukongwe wao katika tasnia hiyo.
Kwa upande wake, Ofisa Sanaa Kitengo cha Matukio, Kurwijira Maregesi, aliitaka Lino kujipanga kujiweka tayari kufanya mashindano hata pale inapokosa mdhamini, huku mjumbe mwingine katika kikao hicho, ambaye ni Ofisa Sanaa Basata, Philemon Mwasanga, akisisitiza mawakala kuwekeana mikataba na warembo kabla ya mashindano kuanza.

“Lino isiwafumbie macho mawakala wasiojali mikataba na warembo, na warembo waisome na kuielewa ili kuepusha migogoro inayoweza kutokea,” alisema.

Akijibu hoja kadhaa zilizoibuliwa katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashimu Lundenga, alisema kuwa, wamejipanga ili kuweza kufanya mashindano yao bila kutegemea wadhamini, huku akiitaka Basata kuwasaidia katika hilo.

“Tatizo mashindano yetu gharama yake ni kubwa sana, nasi hatupendi kuona ubora wake ukishuka kutokana na kushindwa kumudu gharama, ndio maana tumekuwa tukihangaika kuomba udhamini kutoka katika makampuni mbalimbali makubwa hapa nchini,” alisema.
Juu ya mikataba baina ya warembo na mawakala, Lundenga alisema: “Mwaka huu tumesisitiza mawakala waingie mikataba na washiriki kabla ya mashindano na tutakuwa makini katika kufuatilia hilo na changamoto nyinginezo zilizoibuliwa katika kikao hiki.”
Mmoja wa warembo walioshiriki mashindano ya mwaka jana ambaye ni Miss Sinza 2013, Prisca Clement, alisema kuwa, kuna umuhimu wa kuongezwa kwa zawadi katika ngazi za chini ili kumwezesha mshiriki kujivunia na kujitosa kwake katika mashindano hayo bila kujali kama ameshinda au la.
Mashindano ya Miss Tanzania 2014 yamezinduliwa mapema wiki hii, ambapo fainali zake zinatarajiwa kuwa kati ya Septemba na Novemba mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

JE,ULISOMA HABARI HII YA KAJALA KUHONGWA GARI NA KIGOGO MMOJA WA IKULU!


 
NI madai mazito! Kwamba, nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja amehongwa gari na mtu anayedaiwa kuwa ni kigogo wa Ikulu.
Kwa mujibu wa habari hizo ambazo zipo hadi kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, Kajala alinunuliwa gari hilo aina ya Toyota Brevis lenye rangi ya bluu iliyoiva wiki mbili zilizopita mara baada ya kutua Bongo akitokea nchini China ambako alikwenda kwa mambo yake binafsi.
TAARIFA ZINAVYODAI
Wasambaza taarifa hao walidai kuwa, kigogo huyo wa Ikulu ni yule Clement ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.
“Mmeisikia hii? Kajala amenunuliwa gari na Kile (Clement), lina thamani ya shilingi milioni kumi na moja, Wema alie tu nakwambia. We ukisema cha nini wenzako wanajiuliza watakipata lini?
“Kwanza mnajua kama bifu la Wema na Kajala lilitokana na Clement? Alipoachana na Wema akatua kwa msichana anaitwa Naima, lakini akaona bado akaenda hadi kwa Kajala. Wema alipogundua ndiyo akamnunia na kuanza ushoga na Aunt Ezekiel,” msambaza habari za mjini mmoja aliliambia Risasi Jumamosi juzi.

Akaendelea: “Unajua nini? Naamini Wema alimwacha yule bwana na akurudi kwa Diamond baada ya kuona mambo yake siyo mazuri, lakini sasa jamaa (kigogo wa Ikulu) mambo ni safi kwa hiyo anataka kumwoneshea Wema ndiyo maana ameamua kumnunulia gari Kajala baada ya kuwa naye.”

RISASI LALISAKA MITAANI
Baada ya kuzinyaka habari hizo za kimjini, timu ya waandishi wa Risasi Jumamosi, Jumatano iliyopita iliingia mitaani kulisaka gari hilo hasa baada ya Kajala kutopokea simu.

Awali, mtoa habari mmoja alisema Kajala yupo na gari hilo Kinondoni kwa Manyanya, lakini alipofuatwa hapo hakuonekana.
Habari zikapatikana kwamba, alikuwa kwenye Mgahawa wa Steers uliopo jengo la Millennium Tower, lakini pia alipofuatwa eneo hilo hakuonekana.
ALHAMISI SAA 9:06 ALASIRI
Juzi, saa 9:06 alasiri, Kajala alipigiwa simu ambapo alipokea na mahojiano yakawa hivi:
Risasi: Mambo Kajala?
Kajala: Poa tu, mambo?
Risasi: Mambo poa. Eti, namba za gari lako Toyota Brevis ni ngapi?
Kajala: Mh! Yaani hata mimi mwenyewe sizijui, sijazishika kabisa.
Risasi: Sasa, kuna habari kwamba hilo gari umenunuliwa na Clement, yule aliyekuwa na Wema zamani. Kuna ukweli wowote?
Kajala: Mh! Hizo habari si za kweli. Wapo watu wanajiita Team Wema ndiyo wameamua kunipakazia hivyo, wameandika hadi kwenye Instagram, lakini siyo kweli kabisa.
“Mimi nimelinunua hili gari kwa mtu. Aliniuzia kwa shilingi milioni kumi na moja (11,000,000). Sijahongwa wala sijanunuliwa. Kuna watu wanataka kunichafua tu.
KUHUSU USHOGA WAO KUFA
Kuhusu kufa kwa ushoga wao, awali Kajala hakutaka kulizungumzia suala hilo lakini alipobanwa alidai hana tatizo na Wema na kwamba kwa sasa yuko bize kutengeneza filamu zake.
WEMA AKWEPA SIMU
Kwa upande wake, Wema alipopigiwa simu hakupokea lakini siku za nyuma aliwahi kuanika kwamba haamini kama Kajala anaweza kutembea na Clement. Hapo ni wakati ule wakiwa mashoga.
TUJIKUMBUSHE
Katika gazeti la Ijumaa, Machi 21, mwaka huu ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo yenye kichwa;
WEMA, KAJALA KIMENUKA!
Katika habari hiyo, ilidaiwa kuwa, wawili hao si mashoga tena huku sababu mbalimbali zikianikwa.
Ilidaiwa kuwa, kisa kilianzia kwenye saluni moja Kinondoni, Dar ambapo Kajala alifika akiendesha baiskeli iliyosababisha kuloa jasho sehemu kubwa ya mwili.
Chanzo kilisema, Wema alipomuona Kajala alitaka kumkumbatia lakini Kajala alimkwepa kwa sababu alikuwa na jasho jambo lililomfedhehesha Wema na kununa.
“Alichokifanya Wema, alimrushia Kajala maneno makali akimhoji kwa nini alimfanyia hivyo wakati hawana tatizo lolote kati yao,” kilidai chanzo.
Siku nyingine ilidaiwa kwamba Kajala alikwenda nyumbani kwa Wema, Kijitonyama kwa lengo la kumchukua waende location (sehemu ya kurekodia sinema), lakini alipofika aliambiwa ‘bimkubwa’ huyo alilala na Diamond hawezi kuamshwa.

Chanzo hicho kilisema Kajala aliwasiliana na Wema kwa njia ya simu ya mkononi akamwambia asubiri lakini alikaa kwa muda mrefu bila mafanikio hivyo hawakwenda kushuti siku hiyo.
Chanzo hicho kilidai pia kwamba ushosti wa wawili hao ulianza kupepesuka muda mrefu lakini uzi wa mwisho umekuja kukatwa na Diamond mara baada ya kurudiana na Wema.


Credit:GPL

JINSI ROMA MKATOLIKI ALIVYOUZA WIMBO WAKE KWENYE WHATSAPP

  
Inawezekana kama mitandao ya kijamii ukiitumia vizuri inaweza kukupatia faida kubwa kuna watu kadhaa ambao kupitia mitandao ya kijamii wanendesha maisha yao vizuri miongoni mwao kuna jamaa mmoja anajiita dalali Mkombozi aliwahi ku-amplify anavyoitumia Instagram kuendesha maisha yake.



Roma Mkatoliki leo ametoa idadi ya pesa alizowahi kuingiza kupitia wimbo wake wa 2030 ambao alianza kwa kuuza kupitia mtandao wa Whatsapp >>’2030 nilikua nauza kwa shilingi 3,000 kuna artist wanatoa album au mixtape ina nyimbo 20 anauza 5,000 ambao unakuta wanaongea huyo Roma ni nani anatoa wimbo anauza 3,000′

‘Badala ya kusaidiwa na wasanii wenzangu ndiyo wananikandia mi Tanga nina ofisi yangu na napokea album kibao nawauzia tu wana,unakuta watu wanaongea mbona wimbo wenyewe taarifa ya habari halafu anauza 3,000,kwa haraka haraka niliuza kama 1,400,000 kwa kipindi kile cha mwanzo’. Source 255 Clouds Fm

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA "HATUITAMBUI BONGO MOVIE UNITY YA STEVE NYERERE"

 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amedai shirikisho lake haliwatambui wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Unity na kudai kuwa kundi hilo linaundwa na watu sita tu huku wengine wakifuata mkumbo.

Akizungumza na Global Publishers, Mwakifwamba ambaye pia ni muigizaji wa muda mrefu na muongozaji wa filamu amesema hawatambui wasanii hao na anawashauri wajiunge ili watambulike. “Bifu la nini? Mimi ni baba, wao ni watoto. Kwanza sikia… wale sio wanachama wangu.Nawashauri wajiunge kwenye vyama vyangu ili niwatambue kama sehemu ya shirikisho,” alisema.

“Unajua wale wanaongozwa na ustaa. Wanaamini ustaa upo juu ya sheria, sio kweli. Mimi naamini katika uelewa na uwezo.Isitoshe mtu wa kwanza aliyetoa wazo la Bongo Muvi ni mimi. Nakumbuka nilikuwa mimi, Dude (Kulwa Kikumba), William na Ruge Mutahaba, tukaunda Bongo Muvi ili tucheze mechi na Bongo Fleva kwa ajili ya kuchangisha fedha za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto. Tulifanikiwa sana. Hapo sasa walafi wachache wakalazimisha wasanii waende Mwanza wakacheze mechi nyingine ili wapate fedha, nikakataa hilo wazo, ndiyo mwanzo wa kutengana nao. Niwaambie tu Watanzania, chombo mama cha wasanii wa filamu nchini ni TAFF, si vinginevyo,” aliongeza.
“Kwanza Bongo Muvi si chama kama wengi wanavyofikiri, ni kampuni na ina wamiliki wake tisa, hao wengine wanafuata mkumbo kwa sababu hawajitambui. Kama wanabisha, waonyeshe usajili wao wa Basata, maana chombo pekee kinachosajili kazi za wasanii ni Basata.”
Hata hivyo Bongo5 imejaribu kumtafuta mwenyekiti wa BMU, Steve Nyerere kuzungumzia kauli hiyo, lakini amekuwa hapokei simu.

Credit:GPL.

HII NDIO TRENI ILIYOPINDUKA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WAWILI


Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali hivi karibuni katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa.

Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa.

 
Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo hayakusombwa na maji katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika stesheni ya Gulwe, hiyo imetokea saa 9.15 usiku. Treni hiyo ya Mizigo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam na kuelekea Mkoani Kigoma na ilikuwa na mabehewa yaliyobeba ngano, sukari na mafuta.


 
Njia ya Reli iliyoondolewa na maji katika stesheni ya Gulwe Wilaya ya Mpwampwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneno mbambali nchini.


 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akitoka kwenye maji baada ya kuangalia kichwa cha treni kilichopata ajali na kusombwa na maji katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa, usiku wa kuamkia leo, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali za nchi. Ajali hiyo imesababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa iliyoko wilayani Mpwampwa.

 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk, Shaaban Mwinjaka akimfariji mmoja wa Majeruhi wa Ajali ya treni ya mizigo iliyotokea katika Stesheni ya Gulwe Bw. Michael Lupatu wakati alipomtembelea katika hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Wilayani Mpwampwa leo mchana. Ajali hiyo ya treni ya mizigo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha watu wawili na wengine saba kujeruhiwa.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini uchukuzi)

DR. SLAA ;CHADEMA KWA SASA IMEUNGANA NA NCCR-MAGEUZI NA CUF NA KUUNDA UKAWA BUNGENI





BAADA ya kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ndani ya Bunge Maalum la Katiba, vyama vya siasa vya upinzani ,vimeunda umoja wa aina hiyo nje ya bunge hilo (UKAWA- nje) na kupanga kuwashawishi wananchi nchi nzima kudai Katiba yenye kujali maslahi yao.

Kwa mujibu wa makatibu wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo ndani na nje ya Bunge hilo; CHADEMA,NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF), lengo ni kuwahamasisha wananchi waunge mkono jitihada zinazofanywa na UKAWA kuhakikisha wajumbe wanafuata taratibu kuandaa Katiba mpya, ikiwa ni pamoja na kuzipa hoja za wananchi nafasi.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam jana, kwa niaba ya makatibu wakuu wenzake, Dk Willbrod Slaa kutoka Chadema alisema, utekelezaji wa malengo ya UKAWA-nje unaanza rasmi leo mkoani Mwanza, kwa kuzindua mkutano utakaohutubiwa na viongozi hao.

“Bada ya kufuatilia yanayoendelea katika Bunge Maalum la Katiba, sisi viongozi wa vyama vinavyounda UKAWA ndani ya Bunge, ambao tupo nje ya bunge hilo tumeona kuna umuhimu wa kuunda umoja huo nje pia kuhakikisha tunawaelewesha wananchi mambo yote wanayopaswa kuyaelewa kuhusu mchakato unaoendelea ili wakati wa kupiga kura ya kukubali au kukataa Katiba itakayopendekezwa wawe na uelewa wa mambo yote”.

“Tunajionea kinachoendelea bungeni sasa hivi na wala hatutaki kufanya jambo lolote litakalo ufanya mchakato wa kupata Katiba mpya uvurugike au kuvunjwa kabla ya muda wake kwa sababu kufanya hivyo hakutatusaidia wala kutuletea Katiba mpya tuliyoililia kwa miaka mingi...”

“Cha msingi kwetu ni kuwaunganisha wananchi na kuwaomba ushirikiano katika kuwahimiza wajumbe wafuate kanuni ili muda usiishe bila kutuletea Katiba tunayoitaka. Tunakwenda kuwaelimisha kwa mikutano ya hadhara, ili walilie Katiba inayojali maslahi ya watu na si ya chama chochote cha siasa au watu wachache.Tunataka wakisema ndio wafanye hivyo wakijua sababu na waseme hapana wakiwa na sababu,” Dk Slaa alisema.

Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Shaweju Mketo, alieleza kuwa nia yao kuu ni kutengeneza na si kuvuruga kama inavyofikiriwa na baadhi ya watu wanaovitazama vyama vya upinzani kama vurugu wakati hoja wanazoziibua ni kwa ajili ya kutengeneza.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema, hawategemei kuwaambia wananchi wagome wala kufanya vurugu katika mikutano yao kutokana na yanayoendelea bungeni, bali watawafundisha jinsi ya kudai Katiba mpya kwa kufuata taratibu na sheria zilizopo.

Kwa hisani ya Habarileo.

Sunday, March 30, 2014

MH LEMA :DHAMIRA YANGU SASA NI KUONDOKA DODOMA WIKI IJAYO




Kama Mbunge na Kiongozi ninatambua umuhimu wa kutunga katiba mpya ni fursa muhimu katika maisha yangu , harakati muhimu za wanasiasa haswa wapinzani na wadau wengine wa mabadiliko zimeleta fursa hii lakini masikitiko yangu ni mchakato mzima unavyoendelea ambapo nia njema imepotezwa na misimamo ya Watawala juu ya kile wanachokitaka wao .
Nitaongea na Viongozi wangu wa Ukawa kesho ikiwezekana na nitawaeleza wajibu muhimu ninaofikiria kujiondoa kama Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wiki ijayo mapema , dhamira yangu imekwishaamua kwa sababu za msingi kabisa ambazo nitaongea nao kesho na ni Imani yangu kuwa wataniruhusu kutenda tendo hili jema . Hata hivyo nitaeleza na kuandika sababu zote muhimu kabla sijabeba begi langu na kurudi Nyumbani Arusha kuongea na Wananchi walionichagua na kuwaeleza sababu ya kujiondoa katika Mkutano mkuu wa CCM hapa Dodoma unaojulikana kwa jina la Bunge Maalumu la katiba

shauri kwa mh.Godless Lema

Mods nawaomba sana msiunganishe huu uzi na kama ni lazima kufanya hivyo basi nawaomba muache walau kwa masaa machache tu ili mh.aweze kupata fursa ya kusoma nilichoandika

Mh.Lema nakuomba na kukusihi usiwashirikishwe viongozi wako wa UKAWA katika uamuzi wako wa kujitoa katika hilo bunge "fake" zaidi ya kuwapa taarifa tu na kisha utimize dhamira yako.

Mh.Lema nina imani asilimia 97 kuwa hao viongozi wako watakushauru vinginevyo kwani si watu wenye misimanmo "thabiti" na wana imani potofu kuhusu "maridhiano".Na katika wote hao katu usimsikilize kabisa mtu anaeitwa James Mbatia.Huyu ni mtu ambae anaongoza kuamini katika "maridhiano uchwara".Hapo Dodoma hakuna kitu kinachoitwa maridhiano zaidi ya usanii wa kisiasa kudanganya umma wa watanzania.

Mh.Lema kumbuka wako watakauokubeza kwa uamuzi wako huu lakini pia kumbuka hili ni "pigo" kwao kwani wanatambua kuwepo kwenu katika huo mchakato, ni kuupa uhalali kama sio baraka kwani ni wazi mkijitio sasa ni "dosari" kwabu kwa mchakato mzima, hivyo uwepo wenu hapo ni sababu tosha ya wao hapo baadae kuja kuwabeza kuwa hata nyinyi mlishiriki na posho mlichukua na hawata sita kuja kuwaita "wanafiki".

Kuhusu posho usijali kwani hata baba wa taifa alikufa masikini(japokuwa si kama nitakavyokufa mimi na wewe) kwa kuweka mbele uzalendo sasa nawe ukifa masikini cha ajabu ni nini hapo?

Wangapi wamekufa matajiri kwa kudhuluma mataifa yao lakini leo hawana heshima mbele wa macho ya walimwengu wa leo?Leo hii hadhi ya Mobutu na Mandela zinalingana?Hadhi ya Nyerere na Mobutu zinalingana?

Ni bora ukajitoa leo kulinda heshima yako na utakuja kuwa na uhalali wa kuhamasisha umma kuikataa hiyo katiba kwa utakuwa hukushiriki kuitengeneza.

May God blees you!

Mzalendo wa kwel

Saturday, March 29, 2014

KAMATI YAMRIDHIANO YAKUBALINA KURA YA WAZI NA SIRI ZOTE KUTUMIKA


Hatimaye Bunge Maalumu la Katiba limeridhia wajumbe kupiga kura ya wazi na siri katika kupitia mchakato wa rasimu ya katiba mpya.
Maamuzi hayo yalitolewa jana jioni baada ya Kamati ya Maridhiano iliyokutana kuanzia juzi usiku hadi jana mchana kukubaliana kuwa na kura za aina mbili, kufuatia mvutano mkubwa ulioibuka baina ya wajumbe hao.
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, aliamua kuunda kamati hiyo baada ya mapendekezo kutokana na michango iliyotolewa na wajumbe katika mjadala wa juzi, ambapo Freeman Mbowe, alikuwa mmoja wa wajumbe waliotoa hoja hiyo.
Sitta aliunda kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim LIpumba,   
Askofu (mstaafu) Donald Mtetemela na Vuai Ali Vuai.
Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, Sitta aliwaruhusu wanakamati hiyo kila mmoja kutoa yale waliyoamua.
Akiongea kwa niaba ya Mbowe, Johna Mnyika alisema mazungumzo yamesaidia kupiga hatua moja mbele ingawa ya kukubaliana kutokubaliana.
“Sisi tulikuwa na mtazamo kuwa kura iwe ya siri lakini wengine walitaka kura ya wazi. Pamoja na majadiliano yote wenzetu waliona wana uhuru wa kupiga kura ya wazi, ilibidi tufike hatua ya kuamua kulivusha taifa ili lisonge mbele.”
Alisema walipendekeza maamuzi haya yafanywe kwa kura ya wazi lakini wao waliamua yafanyike kwa siri.
Alisema wameamua anayetaka kupiga kura ya wazi apige ya wazi na atakayeamua ya siri iwe ya siri. Matokeo yatakayopatikana kwa minajili ya kupiga hatua moja mbele na kulisogeza taifa mbele.
“Wenye kukubaliana na kura ya wazi watakuwa wengi, na wanaotaka kura ya siri watasema hapana na kwa vyovyote walio wengi watashinda,”
Alisema utaratibu huu wa mashauriano ni vizuri utumike hata pale ambapo hawakubaliani ili kupiga hatua mbele.
“Sisi hatuna njama zozote za kuvuruga bunge hili kwa sababu tumepigania sana jambo hili na kutaka Watanzania wapate Katiba iliyo bora,” alisema.
Alisema wapinzani hawana dhamira ya kukwamisha mchakato wa Katiba. “Kwa sababu kuna magazeti yamemnukuu Mheshimiwa Rais …

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
Alisema unapofanya mchanganyiko wa kura ya wazi na siri ni kuwafanya wale wanaotaka kura ya siri kutopata haki yao lakini Ili tusonge mbele na kuanza kujadili Rasimu ya Katiba, tupige kura ya wazi na siri tufanya maamuzi.
Lakini hii si kura nzuri ni kura itakayotupa vikwazo. “Mimi binafsi ntasema hapana kwa jambo ambalo limeletwa juu ya meza kulifanyia maamuzi. Lakini ili tusonge mbele tumeona tulifanyie maamuzi hayo.
“Natoa wito kwa CCM pamoja na kuwa wengi ni vyema kuheshimu mawazo ya wachache “, alisema na kuongeza kuwa CCM wangekuwa na busara wangeweza kuongeza idadi ya kamati kwa kuweka mbele ya Watanzania

DIMOND ACHAGULIWA KWENYE TUZO ZA KORA ANAOMBA KURA YAKO



 
Tuzo kubwa za Afrika,KORA zimewadia..na Dimond amechaguliwa na wasanii wengine wa Africa  ...hivyo basi kama wewe ni  mpenzi na shabiki wa Music wa Diamond  muwezeshe kushinda kwa kumpigiakura  ingia katika Facebook page yao ambayo ni "Kora Awards" kisha Katika kila post niliyoshiriki Comment kwa kuandika jina Diamond Platnumz

 
Hawa ni baaz ya wasanii kkutoka nchi mabali mbali za Africa walio chaguliwa kazi ni kwako kutoa support kwa nchi yako.

KANGI LUGOLA ,DEO PHILIKUNJOMBE, ESTHA BULAYA WATOFAUTIANA NA MSIMAMO WA CHAMA CHAO


Kangi Lugola

Deo Filikunjombe

Estha Bulaya
Ukiangalia sifa ambazo huwanyanyua watu kufikia umaarufu mkubwa kisiasa, huwa mara nyingi sio kulilia vyeo bali kuwa na misimamo yakinifu, tena bila uoga, mifano ya watu hawa ni kama Nelson Mandela (RIP), Mahatma Gandhi NK. Kwa upande wetu kuana wabunge kama vile Kangi Lugola,Deo Philikunjombe na Estha Bulaya wamekuwa na misamamo inayoweza kupimwa katika mizania ya kisiasa, kama ya mwanasiasa yakinifu. Hajali katoka chama gani, lakini ameweza kukemea kuvunjwa kwa katiba ya JMT na kuonyesha kuunga hutuba makini ya Jaji Warioba bila kujali msimamo wa chama ,  na kusahau maslahi ya Taifa. Kwa  hawa hali imekuwa tofauti wamekataa. Wote wanapendekeza serikali tatu vivilevile kura ya siri

Friday, March 28, 2014

MH EDWARD LOWASA AMUAGA MKUU WA MKOA WA MARA


photo
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Mwalimu Nyerere kumuaga mwili wa Mkuu wa Mkoa wa Mara marehemu John G Tuppa Mungu ailaze roho ya marehem pema peponi aman.Pembeni ni mbunge wa Mwibara Kangi Lugola

TASWIRA YA KAMPENI CHALINZE KWA MGOMBEA WA CHADEMA

 

Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ndugu Mathayo Mang'unda Torongey akiendelea na mikutano ya Kampeni Jimboni Chalinze.

TAZAMA UCHAGUZI WA KATIKA CHUO CHA CBE CAMPUS YA MWANZA



 
 Huu ni mmoja wa msafara wa mgombea Urais wa wanafunzi wa chuo hicho cha CBE.


Hapo juu ni mabango ya wagombea.
 
Huu ndio uchaguzi katika chuo cha cbe cumpus ya mwanza

Kama vyuoni imekuwa hivi bunge uchaguzi wa kuelekea Bungeni.
Je Tutafika?

ROBERT MUGABE KUSUSIA MKUTANO UMOJA WA ULAYA ENDAPO MKEWE HATAALIKWA



Serikali ya Zimbabwe imeeleza kuwa rais Robert Mugabe ataususia mkutano uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa April kati ya Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) endapo mkewe Grace hataalikwa.
Mkutano huo utafanyika Brussels, Ubeligiji (katika bara la Ulaya) ikizingatiwa kuwa mwaka 2002 Umoja wa Ulaya uliwawekea vizuizi Robert Mugabe na mkewe Grace kutozitembelea nchi za bara la Ulaya.
Mugabe ambaye ni makamo mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) amepewa mualiko wa kuhudhuria mkutano huo lakini mkewe hakupewa mualiko huo.
Balozi wa EU nchini Zimbwabwe, Aldo Dell’Ariccia alieleza wiki iliyopita kuwa Umoja huo wa Ulaya unawaalika kwenye mkutano watu ambao wana kazi ya kufanya kwenye mkutano huo na kwamba program za kikao hicho hazihusishi wana ndoa.
Kauli ya balozi huyo ilionekana kumkera Mugabe na msemaji wake akarudisha mashambulizi kwa mshangao.
“Ni kitu cha kushangaza kwamba EU haikutoa mualiko kwa First Lady. Kitu ambacho Mungu amekiweka pamoja EU inataka kukitenga. Hivi wanatarajia rais aiheshimu EU na kuikosea heshima ndoa yake mwenyewe?” alikaririwa msemaji wa Mugabe, George Charamba.
Mke wa Mugabe alikuwa akikosolewa kuwa hutumia pesa nyingi kufanya manunuzi ya anasa kila anapolitembelea bara la Ulaya.

MASHABIKI WA MACHESTER UNITED WAJIPANGA KUMPINGA MOYES KESHO


Mashabiki wa Manchester united wanaochukizwa na mwenendo wa timu yao chini ya uongozi wa David Moyes wamefanikiwa kupata ndege itakayopita juu ya paa la uwanja wa Old Trafford jumamosi ya kesho huku ndege hiyo ikiwa imebeba bango la ‘Moyes Out’.Ndege hiyo imepangwa kupita juu ya paa la OT kwa dakika 10 kabla ya mchezo kuanza na baadae kwa dakika 5 na wakati wa mchezo vs Aston Villa.
Kundi la mashabiki hao tayari limethibitisha kwamba kesho ndege hiyo yenye bango la “Wrong One: Moyes Out.” itafanya kama walivyopanga.

Bango hilo ni kinyume ya lile walilotaka kulishusha kutoka kwenye jukwaa la Stretford End linalosomeka ‘Chosen One’.

RAISI KIKWETE AZINDUA MRADI WA MAJI MUHEZA

 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwisha ndoo ya maji Bibi Rukia Bakari muda mfupi 
baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Kwemhosi wilayani Muheza Mkoa wa Tanga Jana .Mradi huo utavinufaisha vijiji vinane katika wilaya hiyo yenye uhaba mkubwa wa maji

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua na kukagua bidhaa Soko la Vyakula Michungwani wilayani Muheza jana 

Hapa Raisi anachagua matunda

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua na kuzungumza na wafanyabiashara katika soko la Vyakula Michungwani Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga jana .Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi mkoa wa Tanga.Picha na Freddy Maro-IKULU

OSTAZ JUMA NA MUSOMA AZAMA KWA JOHARI WA BONGO MUVI.


PENZI limekolea na kinachoonekana sasa kwa Ostaz Juma Namusoma ni kukazia penzi lake kwa mwanadada Blandina Chagula ‘Johari’ anayesumbua kwenye Bongo Muvi.
Habari zilizolifikia Amani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba Ostaz alifunga safari kwenda nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi lakini pia kumnunulia mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali kwa lengo la kupalilia uchumba wao.
“Jamaa alikuwa Sauzi (Afika Kusini), aliondoka hapa tarehe 17 (Machi) na amerudi tarehe 21. Kamletea zawadi kibao lakini kubwa zaidi ni kamera kubwa, nzuri ya kisasa kwa ajili ya kerekodia filamu,” kilipasha chanzo hicho.
Amani lilifanikiwa kumpata Ostaz kwa njia ya simu, akafafanua: “Ni kweli nilikuwa Afrika Kusini. Kuhusu Johari, ni kweli si mke wangu? Nimemletea zawadi nyingi sana, achana na hiyo kamera unayosema.
“Lengo ni kuweka uchumba wangu na yeye sawa. Nilitamani sana kusafiri naye lakini sikutaka kufanya hivyo ili kuweka usawa, mke wangu asione nimeegemea zaidi kwa mke mdogo.”
Alipoulizwa kwa nini amemuita Johari mkewe, haraka alisema: “Ndoa ipo karibu, nimeshaamua Johari awe mke wangu wa pili. Wadau wasubiri waone, uzuri ni kwamba dini yangu si kikwazo.”
hagula ‘Johari’ anayesumbua kwenye Bongo Muvi.
Habari zilizolifikia Amani kutoka kwa chanzo chetu zinasema kwamba Ostaz alifunga safari kwenda nchini Afrika Kusini kwa mapumziko mafupi lakini pia kumnunulia mpenzi wake huyo zawadi mbalimbali kwa lengo la kupalilia uchumba wao.
“Jamaa alikuwa Sauzi (Afika Kusini), aliondoka hapa tarehe 17 (Machi) na amerudi tarehe 21. Kamletea zawadi kibao lakini kubwa zaidi ni kamera kubwa, nzuri ya kisasa kwa ajili ya kerekodia filamu,” kilipasha chanzo hicho.
Amani lilifanikiwa kumpata Ostaz kwa njia ya simu, akafafanua: “Ni kweli nilikuwa Afrika Kusini. Kuhusu Johari, ni kweli si mke wangu? Nimemletea zawadi nyingi sana, achana na hiyo kamera unayosema.
“Lengo ni kuweka uchumba wangu na yeye sawa. Nilitamani sana kusafiri naye lakini sikutaka kufanya hivyo ili kuweka usawa, mke wangu asione nimeegemea zaidi kwa mke mdogo.”
Alipoulizwa kwa nini amemuita Johari mkewe, haraka alisema: “Ndoa ipo karibu, nimeshaamua Johari awe mke wangu wa pili. Wadau wasubiri waone, uzuri ni kwamba dini yangu si kikwazo.”

Credit:GPL

MSANII WA KIZAZI KIPYA H.BABA AKUTWA AKIWA AMEMBEBA MTOTO WAKE MGONGONI KITAANI




Mwanamuzi Maarufu wa Bongo Flava H-Baba Hivi Karibuni amekutwa amembeba mtoto wake mgogoni
kwa kutumia mbeleko kama wabebavyo wamama huku akiwa hana habari na mtu alipoulizwa alisema yeye anapenda kumsaidia mke wake (Flora Mvungi ) Kulea mtoto kwani ni Jukumu lao wote wawili......

MVUA YALETA ADHA KWA WAKAZI WA DAR ES SALAAM HASA BARA BARA KUJAA MAJI

Screen Shot 2014-03-28 at 4.45.29 PM
 Vijana wanafanya jitihada ilikulitoa gari lililokwama kwenye dimbwi la maji

Ukimuuliza mwenyeji yeyote wa Dar es salaam  ni sehemu gani anazozijua wanakaa watu wenye uwezo wa kifedha na hata baadhi ya viongozi wakubwa wa Serikali, basi lazima atakutajia na Mikocheni.
Pamoja na hilo, Mikocheni ni moja ya maeneo yanayojaa maji sana kipindi cha mvua Dar es salaam kama ambavyo unaona kwenye baadhi ya picha ya juu na hii inayofata hapa chini.
Sehemu nyingine ambazo zipo kwenye hizi picha hapa chini ni pamoja na Kinondoni na Kijitonyama.

  Screen Shot 2014-03-28 at 4.45.37 PM 
maeneo mengi kwa watembea kwa miguu walishindwa kutoka au kuingia kwenye maeneo 
 mengi kwani mfumo wa miundombinu hasa mitaro ya mji ni mibovu. 

 Screen Shot 2014-03-28 at 4.45.12 PM 
 Gari la polisi laingia kwenye mtaro watu wana fanya jitihada ya kulitoa
  Screen Shot 2014-03-28 at 4.45.04 PM 
Hali ilikuwa tetesana hasa kwa magari madogo, bajaji na bodaboda