Raia wa Misri wanapiga kura kwa
muda wa siku mbili kumchagua rais mpya chini ya ulinzi mkali kuhakikisha
mchakato wa upigaji kura unafanyika kwa usalama.
Karibu maafisa wa usalama laki mbili wameshika
doria kote nchini Misri serikali ikionya dhidi ya hatari za usalama
zinazoweza kusababishwa na itikadi kali za kiislam .
Adbel Fatah al-Sisi Kiongozi wa
kijeshi wa zamani aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais wa
awali Mohammed Morsi anatarajiwa kupata ushindi kwa u rahisi.
Oparesheni kubwa ya usalama inayoendelea nchini
Misri ni ushahidi kamili kuwa utawala wa sasa unaoungwa mkono na jeshi
unatambua kuwa ugaidi unaoungwa mkono na Waislamu wenye itikadi kali upo
na unaweza kuteguliwa wakati wo wote.
Mbinu ya kukabiliana na ugaidi huo ya Abdel
Fatah al-Sisi haijabadilika ila tu ni magwanda yake ya kijeshi ya field
Mashel yaliyojaa medali yaliyobadilishwa na nguo za kiraia.
Ametangaza katika kampeni yake kuwa anaunga
mkono kuangamizwa kabisa kwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo
limeshuhudia maelfu ya wanachama wake wakizuiliwa na mamia wakihukumiwa
vifo.
Bwana Sisi ametoa wito kwa watu wanaotakia Misri
amani na utangamano baada ya miaka kadhaa ya mapinduzi na ghasia na
ameheshimiwa kiwango cha kusujudiwa na wengine hivi kwamba unaweza
kununua peremende au chokoleti dukani iliyopachikwa picha yake.
Mpinzani wake mwenye mrengo wa kushoto, Hamdeen
Sabbahi, anatajwa katika vyombo vya habari ambavyo vinaoenekana kuamua
tayari kuwa yeye atashindwa katika Uchaguzi unaoanza leo.
Ingawa wapiga kura wana mazoea ya kubadilika
dakika za mwisho kabla ya uchaguzi lakini wengi nchini Misri watashangaa
iwapo Bwana Sisi hashindi uchaguzi huu, na tena kwa urahisi
No comments:
Post a Comment