Monday, December 29, 2014

MVUA KUBWA ‘YALILOWESHA’ JIJI LA DAR ES SALAAM

Mtaa wa Ohio katikati ya jiji ulivyokuwa umekumbwa na maji.
Hali ilivyokuwa maeneo ya Mwananyamala A. 
 Maeneo ya Hongera, Sinza, nayo yalijaa maji.
Maeneo ya Afrika Sana yalionja adha ya mvua hiyo kama sehemu nyingine nyingi.
Hapa ni eneo la Mwenge-Bamaga ambalo nalo liliathirika vibaya.  

MTANDAO wetu leo umefanikiwa kuzunguka baadhi ya maeneo katika viunga vya jiji la Dar es Salaam na kujionea baadhi ya maeneo baada ya mvua kubwa ‘kuanguka’ katika jiji hili na maeneo ya jirani na kusababisha adha kubwa kwa wakazi wake.
GREDIT GPL

Saturday, December 27, 2014

TAMASHA LA WAFALME: DIAMOND, MZEE YUSUF NI HISTORIA DAR LIVE


Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Diamond akiwachombeza mashabiki.

Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.

Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.

Mfalme Mzee Yusuf on da stage.

Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.

Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.

Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.

Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.

Platnumz akizidi kufanya yake stejini.

Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.

Diamond na Idris wakifanya yao stejini.

Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.

Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.

Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.

Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.

Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.

Diamond akifanya makamuzi na dansa wake.

Dansa wa Diamond akionyesha umahiri wake stejini.

…Sebene time.

Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.

NIMEMALIZA: Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.

Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.

Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.

Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.

Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.

Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
 
 
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.


Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.


Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.
MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.

Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL)

MAN UNITED CHELSEAL, ARSENAL MAN CITY ZAZID KUNG"ARA KWENYE EPL



Olivier Giroud alipewa kadi nyekundi katika ushindi wa arsenal dhidi ya QPR
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa Olivier Giroud alihitaji kupewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya QPR,lakini akathibitisha kuwa mshambuliaji huyo ameomba msamaha baada ya kisa hicho.
Giroud mwenye miaka 28 alionekana akimpiga kichwa Nedum Onuoha katika kipindi cha pili cha ushindi wa 2-1.
Wakati huohuo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa beki John Terry anacheza kama wakati alivyoiongoza the blues kushinda ligi ya Uingereza miaka kumi iliopita.
Ana motisha chungu nzima. John Terry alifunga bao la kwanza la Chelsea

''Sioni tofauti ya John wa miaka ya 2004,05,06 sioni tofauti yoyote'',alisema Mourinho.
Terry alifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham na kuifanya timu hiyo kusalia kileleni mwa ligi hiyo.

Kwengineko mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa ametosheka na uongozi unaotolewa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ambaye alicheza katika safu ya kati na kuisadia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford. Rooney aliifungia Manchester United mabao mawili katika ushindi wa mabo 3-1 dhidi ya Newcastle

Rooney alifunga mabao mawili na kutoa usaidia wa bao la tatu kwa Robin Van Persie.
Nayo Manchester City ilifunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza dhidi ya West Bromwich licha ya barafu iliokuwa ikianguka katika uwanja huo na kusalia nyuma ya Chelsea kwa alama tatu.
Fernando aliifungia City bao la kwanza,baada ya Ben Foster kutoa kross nzuri kutoka kwa Jesus Navas. Yaya Toure alicheka na wavu wa Westbromwich alipopiga mkwaju wa Penalti

Yaya Toure alifunga bao la pili kupitia mkwaju wa Penalty kabla ya David Silva kufunga bao la tatu.

West Brom 1 - 3 Man City West Bromwich walifunga bao la kufutia machozi wakati wa kipindi cha pili.

KOCHA WA MANCHESTER UNITED TUTANATAKA KUSHINDA LIGI



Kocha wa Manchester Louis van Gaal
united Louis Van GaalManchester United bado ina matumaini ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu.
Kulingana na mkufunzi Louis Van Gaal lengo lao ni kushinda ligi hiyo msimu huu licha ya kuwa wako alama 10 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo sasa Chelsea.
Baada ya kuanza na matokeo mabaya, mashetani hao wekundu wameshinda mechi sita mfululizo kabla ya kutoka sare katika mechi ya saba.
''Lengo letu kuu ni kushinda ligi mwishoni mwa msimu huu'',alisema Van Gaal.

KOREA KASKAZINI YAMTUSI RASI OBAMA


 
Rais Barrack Obama wa marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa Tropiki
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview. Filamu ya the interview ambayo rasi Obama alishinikizwa ionyeshwe 


Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.
Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

MKE WA RAIS WA ZAMANI WA IVORY COAST ASHITAKIWA BI SIMONE GBAGBO


Mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast laurent Gbagbo,bi Simone Gbagbo amefunguliwa mashtaka ya ghasia za baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast
Mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo amefikishwa mahakamani kutokana na mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 300 waliuwa.
Bi Gbagbo na watu wengine 82 akiwemo waziri mkuu wa zamani wameshtakiwa kwa kuhujumu usalama wa nchi, ukabila na kwa kubuni makundi ya uhalifu.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu miaka minne iliyopita anasubiri kesi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kutokana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Zaidi ya watu 3000 waliuawa katika ghasia hizo baada ya rais huyo wa zamani kukataa kushindwa katika ya kura ya awamu ya pili.
Bi Gbagbo ambaye alikuwa anazuiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu ameshtakiwa kwa jaribio la kuhujumu usalama wa taifa hilo.
Aliyekuwa waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na kiongozi wa chama cha FPI Affi N'Guessan pia wamefunguliwa mashtaka na bi Gbagbo.

Tuesday, December 16, 2014

AJALI YA BASI YAUA SABA, NA KUJERUHI TABORA


 


Picha zote zikionyesha mandhari ya sehemu ajali hiyo ilipotokea.

Watu saba wamefariki Igunga, mkoani Tabora, ambapo wengi wamejeruhiwa baada ya basi…