Saturday, May 31, 2014

GARI ALILOPATANALO AJALI DIIRECTOR GEORGE TYSON SAA NNE KABLA YA TUKIO

 
Dj Choka ambae kwa sehemu kubwa alikua kwenye safari moja ya Dodoma na Marehemu George Tyson, ameandika kwenye http://djchokamusic.com/ kwamba Marehemu alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma.

Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni ikiwa ni saa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.

Kwenye gari walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha ila wengine wamepata majeraha mwilini akiwemo dereva wa gari hilo ambapo kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro baadae asubuhi safari ya kurudi Dar es Salaam itaanza.



 



Kwenye hii safari, George Tyson aliambatana na mtangazaji Mboni Masimba wa The Mboni show.



 
CHANZO DJ CHOKA 

No comments:

Post a Comment