Wednesday, May 21, 2014

NI MIAKA 18 TANGU KUZAMA KWA MV BUKOBA NDUGU NA JAMAA WAWAKUMBUKA KWA KUWAOMBEA.





Baba mzazi wa flaviana pamoja na wadogo zake


Tanzania leo tumewakumbuka ndugu zetu ambao walipoteza maisha kwenye ajali ya kuzama kwa meli ya Mv Bukoba ambayo ilizama siku kama ya leo mwaka 1996 ambapo miongoni mwa watu waliopoteza maisha ni mama mzazi wa mwanamitindo Flaviana Matata pamoja na mtoto wa mjomba wake ambao walikua safarini.

Leo Flaviana Matata akiwa na Ambwene Yesaya ‘Ay’ na baadhi ya wasanii wengine wa Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa dini waliungana na Watanzania waliopata nafasi kuhudhuria ibada iliyofanyika kwenye makaburi yaliyopo eneo la Igoma Jijini Mwanza.












































Nyaisa Simango ni Mmoja wa walionusurika na ajali ya Mv Bukoba

No comments:

Post a Comment