Jana ilikuwa uzinduzi wa ujenzi wa Barabara jimboni UBUNGO na KAWE uliotawaliwa na shangwe na nderemo kwa wakazi waliopakana na barabaza za Mbezi Mwisho-Goba-Tangi Bovu, Barabara ya External –Kilungule, Barabara ya Msewe-Baruti! Ambapo ni barabara zilizopo kwenye majimbo wa Kawe na Ubungo yaliyo chini ya CHADEMA (Ubungo- Mnyika na Kawe- Halima Mdee)
Hii ni moja ya hatua kubwa sana na muhimu katika utatuzi wa foleni ndani ya Jiji la Dar es Salaam na kuendeleza kwa kiasi kikubwa maeneo ambayo barabara hizo zinapita (ndani ya Jimbo la Ubungo).