Friday, February 27, 2015

WASANII WA TANZANIA WANAUZUNGUMZIA UCHAGUZI MKUU WA 2015


 ‘IZZO BUSINESS’
Mkali huyu wa Bongo Fleva kutoka Nyanda za Juu Kusini, mkoani Mbeya, naye amefungukia uchaguzi mkuu kwa kueleza kuwa anaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani na utulivu.
“Kuhusu mambo mengine kama vurugu na machafuko, hivyo havina nafasi kabisa,” alisema.


MRISHO MPOTO ‘MJOMBA’
Mkali huyu wa kughani na tungo za Kiswahili, yeye amefunguka:
“Kwanza kabisa uchaguzi umegawanyika sehemu mbili, kuna viongozi ambao wanahitaji madaraka na kuna wengine wanahitaji kufanya biashara.
“Vilevile hata wapiga kura nao wapo wanaojiandaa kufanya biashara kwa kujua kwamba wakimpigia kura kiongozi fulani, watanufaika na kitu fulani, tofauti na zamani ambapo utii na nidhamu kwa viongozi na wapiga kura ulikuwa mkubwa.“Sasa hivi hata wasanii nao wanafanya biashara kwa kutazama mgombea gani ana fedha ndiyo wanaenda kumfanyia kampeni, kwa hali hii tutegemee kuwa uchaguzi utakuwa wa kibiashara na si kutafuta kiongozi bora kwa taifa.”

KHADIJA KOPA ‘MALKIA’
Malkia huyu wa mipasho, ambaye pia ana uelewa mkubwa kwenye mambo yanayohusu siasa alisema: “Kwa kweli mi naona mwaka huu utakuwa mzuri kwa upande wa wanawake kwa sababu katiba inayopendekezwa ikipitishwa kutakuwa na usawa katika kila nafasi ya uongozi kati ya wanaume na wanawake.
 
BABY MADAHA.
Mwanadada huyu anayefanya poa kwenye gemu la Bongo Fleva, alifunguka: “Naamini kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu bado nafasi ya wanawake kwenye urais itakuwa ni ndogo lakini kwa upande wa nafasi za ubunge na udiwani wanaweza kufanya vizuri zaidi na watu wakashangaa kuona viti vingi vikichukuliwa na wanawake wenye kiu ya kuleta maendeleo ndani ya taifa letu. Mi naamini wanawake tunaweza.” EMMA-NUEL SIMWINGA

KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
Msanii huyu wa filamu alisema “Mtazamo wangu kwa kweli mi naona uchanguzi wa mwaka huu utakuwa mgumu kuliko changuzi zote zilizowahi kutokea ndani ya taifa hili, kwa sababu watu wengi wameamka na wanajua nini wanafanya.
“Lakini pia wananchi wanaanza kuwakataa baadhi ya vigogo wanaokuja mtaani kwa mbwembwe na baada ya kupata kile wanachokitaka wanakimbia na kujali maslahi yao binafsi, kwa hali hii baadhi ya vigogo wataanguka sana kwenye nafasi zao, tumeona kwenye Serikali za Mitaa mambo yalivyokuwa, tusubiri lakini uchanguzi utakuwa mgumu sana, vijana wengi walikuwa hawapigi kura lakini sasa wamejua maana halisi ya kura zao”.
AMINI MWINYIMKUU
Msanii huyu wa muziki wa Bongo Fleva naye alifunguka: “Uchaguzi wa mwaka huu mimi naona utakuwa mzuri kwa sababu kila chama kina mashabiki na wapenzi wake na kikubwa ambacho kinaonekana ni kwamba wananchi wengi wameelewa nini maana ya kupiga kura kwa lengo la kupata viongozi ambao wataleta maendeleo ndani ya taifa letu.”

 

EMMANUEL ELIBARIKI ‘NAY WA MITEGO’
Msanii huyu wa Bongo Fleva ameeleza mtazamo wake kuelekea uchaguzi mkuu:
“Uchaguzi wa mwaka huu unaweza kuwa mgumu sana kwa sababu watu wameelimika tofauti na zamani ambapo watu walikuwa wanafanya mambo bila kujielewa. Vijana na watu wengine wameelimika na kujua kiongozi gani anafaa na nani hafai.“Ule ujanja wa kusema baadhi ya vyama vitaiba kura nadhani hilo litakuwa gumu sana mwaka huu kwani kila mtu anapiga kura akiwa anajua haki zake za msingi.”
 ‘IZZO BUSINESS’
Mkali huyu wa Bongo Fleva kutoka Nyanda za Juu Kusini, mkoani Mbeya, naye amefungukia uchaguzi mkuu kwa kueleza kuwa anaamini uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani na utulivu.
“Kuhusu mambo mengine kama vurugu na machafuko, hivyo havina nafasi kabisa,” alisema.

Monday, February 23, 2015

USIKU WA NUHU MZIWANDA NA SHILOLE NDANI YA MAISHA CLUB




Usiku wa kuamkia Feb 23, 2015 mashabiki wa muziki waliweza kukutana na kushuhudia event iliyoandaliwa na Nuh Mziwanda Shilole iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maisha Club Dar es Salaam huku shangwe za burudani zilitolewa kutoka kwa Makomando, Country Boy, Shilole, Darasa, na wengineo .




SHISHI NA NUH MZIWANDA


SHISHI BABY
.

Flowers


D


Makomando.

NUH KATIKATI NA WADAU

FLOWERS NAO WALIKUWEPO



WADAU
DARASA COUNTRY BOY

MAKOMANDO
CREDIT MILLARDAYO.

Sunday, February 22, 2015

MANCITY YAIADHIBU NEWCASTLE UNITED 5-0





Kilabu ya Manchester City ilipata ushindi wao mkubwa zaidi katika ligi ya EPL msimu huu kwa kuicharaza Newcastle 5-0 na hivyobasi kupunguza pengo lililopo kati yake na viongozi wa ligi kwa sasa Chelsea hadi pointi tano.
David Silva alifunga mabao mawili katika ushindi mkubwa baada ya kilabu ya Burnley kupata sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea.
Huku Yaya Toure akiwa amerudi kutoka dimba la mataifa ya Afrika naye Wilfried Bonny akiwa ameanza kama mchezaji wa Ziada,City ilianza mechi hiyo kwa kasi ikilinganishwa na mechi zao nyingine katika uwanja wa nyumbani Etihad.
Mancity ilifunga mabao yake kupitia Aguerro,Dzeko na Samir Nasri.

WASICHANA SYRIA WAJIUNGA NA (IS) WAASI

 
Wasichana wa Uingereza wanaodaiwa kuelekea Syria ili kujiunga na IS
Familia za wasichana watatu raia wa Uingereza ambao wanakisiwa kusafiri kwenda nchini Syria kujiunga na kundi la Islamic State zimewasihi kurudi nyumbani.
Wasichana hao kutoka mji mkuu wa Uingereza London walionekana mara ya mwisho walipopanda ndege iliyokuwa ikienda nchini Uturuki.
Familia ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 ilisema kuwa inaelewa kuwa alikuwa na nia ya kuwasaidia wale wanao taabika nchini Syria lakini eneo hilo ni hatari.

RAIS KIKWETE AWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU

Saturday, February 21, 2015

MEZ B KUZIKWA JUMATATU MAKABURI YA WAHANGA DODOMA

Mez B akiwa katika moja ya mahojiano yake na kituo cha TV.


Marehemu, Mez B akiwa studio enzi za uhai wake.
ALIYEKUWA memba wa kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ ambaye amefariki jana mjini Dodoma anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya Wahanga yaliopo Maili Mbili mjini Hapo. Mtandao huu uliongea na mama wa marehemu, Marry Mkandawile ambaye alisema kuwa kwa sasa msiba upo maeneo ya Kisasa mjini hapo.

Sunday, February 15, 2015

BABA MZAZI WA DULLY SYKES, MZEE SYKES AFARIKI DUNIA

 Baba mzazi wa msanii dully sykes enzi za uhai wake.

http://api.ning.com/files/8k2*97pl68yhdm8-dGrBnFsIgRGn5nB4WqMGaCVDWM1BQLmLnY9CpcLCrgtE8utF5bW7gp2yNVZjW*v6ujz5*DKV5LTE1yi4/dullynababaake.jpg 
Tunapenda kutoa pole kwa familia ya msanii dully sykes kwa kufiwa na baba yake! bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

CHRISTIAN BELLA , MZEE YUSUPHW WAFUNIKA VALENTINE'S DAY, DAR LIVE


 Mfalme Mzee Yusuf akiimba na mashabiki wimbo wake mpya wa Mahaba Niue.

Bella akiwakonga mashabiki jukwaani.…

TASWIRA KATIKA KIKAKO CHA BARAZA LA UONGOZI WA KANDA YA KASKAZINI -KATIKA HOTELI YA THE NEW ARUSHA HOTEL


Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman A.Mbowe akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini Mhe Israel Natse wakiwa wanaingia ukumbi wa JUMUIKA

Viongozi wa kuu wa Chadema Taifa pamoja na Kanda wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kikao cha baraza la kanda ya kaskazini kuanza

Waheshimiwa wabunge wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa
 
Katibu wa Kanda ya kaskazini Mhe Amani Golugwa akiwakaribisha wajumbe wa kikao cha baraza la Kanda ya Kaskazini , wajumbe wa kikao wametoka katika majimbo 33 ya kanda

Mwenyekiti wa Kanda ya kaskazini Mhe Israel Nates akitoa neno la ufunguzi kwa wajumbe na kumkaribisha Naibu katibu Mkuu Zanzibar

 
 Naibu katibu Mkuu Zanzibar Mhe Salimu Mwalimu akiongea na Wajumbe wa baraza la uongozi wa kanda ,na kufafanua majukumu na utekelezaji wa kanda kaitika ujenzi wa chama


Mhe Freeman A.Mbowe akiwa hutubia wajumbe wa baraza la kanda pamoja na waandishi wa habari, akifafanua baadhi ya mambo ambayo yanaendendea katika nchi yetu kwa sasa, pia akiitaka tume kuwa na msimamo wa siku na tarehe ya kuanza zoezi la uandikishaji wa Wanachi kwenye daftari la kupiga kura

Saturday, February 14, 2015

MWENYEKITI WA VIJANA CHADEMA ATANGAZA NIA KUWANIA KITI CHA UBUNGE ARUSHA

Aliyekuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe wa arusha mjini ametangaza kugombea ubunge wa arusha mjini kupitia chadema.

Ametangaza nia baada ya kuitisha press conference na waandishi wa habari Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014
Alieleza kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless Lema
Aidha alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza umaskini
Alitoa wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu
  GREDIT Pamela Mollel wa jamiiblog

Tuesday, February 10, 2015

SERIKALI YAIPONGEA BENKI YA ACCESS KUFUNGUA TAWI LAKE JIJINI MBEYA‏


Mwakilishi wa Benki ya Access kutoka Makao makuu jijini Dar es salaam, Sebastian Gaissert, akitoa hotuba yake katika sherehe za uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani Mbeya.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro akizungumza 

JE! UNAJUA UMUHIMU WA KULA NANASI HUU HAPA





Moja kati ya matunda ambayo yanapendwa zaidi ni tunda la nanasi, linapendwa zaidi kutokana na ladha nzuri na tamu ambayo inatokana na sukari iliyoko ndani ya tunda hili ambapo inafanya tunda hili kuwa moja kati ya matunda ambayo yanatumika sana kwa kutengeneza juice.

Hata hivyo baada ya kusoma taarifa hii ya utafiti utapata sababu zaidi za kupenda kula mananasi, zipo faida nyingi sana kwenye mwili wa mwanadamu faida ambazo ni za kiafya zaidi.

Mananasi yana virutubisho hivi muhimu kwa mwili wa mwanadamu.

Mananasi ni chanzo muhimu sana cha vitamin pamoja na madini ambayo yanasaidia kuimarisha afya ya mwanadamu ambazo ni kama vile Thiamin, Riboflavin, Vitamini B-6 , Folate , Acid ya Pantothetic pamoja na madini ya Magnesium, manganese na potasia.

Katika hesabu za kitabibu, kipande kimoja cha nanasi kinatosha kuongeza 131% ya vitamin c ambayo mwili wako unaihitaji kwa siku moja.


Mananasi husaidia kutibu vidonda na uvimbe.

Moja kati ya vurutubisho vilivyoko ndani ya nanasi kinaitwa Bromelain, husaidia sana kuondoa maumivu kwenye viungo, kupunguza hali ya uvimbe kwenye tezi na hata kupunguza uvimbe wa kawaida ambao umetokea ndani ya mwili na pia humsaidia sana mtu akiwa amefanyiwa upasuaji.
Mananasi husaidia Mfumo wa usagaji (Mmeng’enyo) wa chakula.
Manansi yana virutubisho vya kambakamba (fibre) ambavyo husaidia sana kwenye kusagwa kwa chakula mwilini, kirutubisho cha Bromelain pia husaidia kwneye kusaga chakula tumboni kwa kusaidia kuvunja vile vipande vya protini.

Manufaa ya nanasi kwenye ngozi
Vitamini C ipatikanayo kwenye mananasi husaidia sana kuipa ngozi mng’ao ambao unahitajika, mishipa midogo ya damu pia hufaidika sana kutokana na mananasi pamoja na viungo vingine vya mwili na mifupa pia.
Manufaa ya nanasi kwenye mifupa
Mananasi yana madini aina ya Manganese ambayo husaidia kuzalisha nishati mwilini huku ikisaidia kutoa ulinzi kwa seli za mwili wa mwanadamu.
Madini haya yanasaidia sana ufanyaji kazi wa madini mengine na virutbisho kama Thiamine na Biotin ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia kufanya mifupa kuwa migumu na yenye afya zaidi na pia husaidia kuyayusha vyakula vyenye mafuta.

Mananasi husaidia Macho .
Tunda aina ya nanasi lina vitamin A pamoja jna kirutubisho aina ya Beta-Carotene ambavyo kwa pamoja husaidia mfumo wa kinga ya mwili na afya ya macho.
Mananasi hutoa nguvu na nishati na kushusha shinikizo la damu.
Mananasi ya kiwango kikubwa cha Vitamini B1 na B6 ambavyo ni vyanzo muhimu sana vya nishati pamoja na kuvunjavunja sukari kwenye mfumo wa usagaji wa chakula.
Madini ya shaba pia yanapatikana kwenye mananasi yanasaidia sana kutoa afya kwa seli nyekundu zinazosaidia kutengeneza damu na madini ya potasia ambayo yanasaidia kuweka mapigo ya moyo sawa na kushusha shinikizo la damu.

Sunday, February 8, 2015

MKULIMA WA KATAVI ALIYEJISHINDIA MILIONI 10 ZA VODACOM AKABIDHIWA KITITA CHAKE


Hayawi hayawi yamekuwa Haynes Peter Kanumba (20) ambaye ni mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, akiwa mwenye furaha baada ya kukabidhiwa kitita chake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (hayupo pichani) wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi.Ili mteja kujua kama umeshinda unatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba ambaye ni mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Mpanda baada ya kukabidhiwa fedha zake na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) Hafla hiyo ilifanyika katika tawi hilo mkoani humo. Ili kujua mteja kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.

Meneja wa benki ya NMB mkoa wa Katavi Erick Luanda akimuonyesha taarifa za fedha ya benki (bank statement) Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania , Hynes Kanumba mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi(wapili toka kushoto) wanao shuhudia ni Meneja mauzo wa Vodacom kanda ya Kusini Petro Chinyama(kusho) na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia)Ili kujua mteja kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.

Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba ambaye ni mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akiwa anaondoka na mtoto wake mgongoni baada ya kukabidhiwa kitita chake rasmi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(hayupo pichani) kwenye ofisi za benki ya NMB tawi la Mpanda mkoani humo mwishoni mwa wiki. Ili mteja kujua kama umeshinda tuma neno Jay kwenda 15544.

Mshindi wa Milioni 10/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Hynes Kanumba mkazi wa Inyonga Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi akipongezwa kwa kupigiwa makofi na Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu (kulia) Meneja Mauzo wa kampuni hiyo wa kanda za juu kusini na Meneja wa NMB mkoa wa Katavi Erick Luanda,mara baada ya kumkabidhi kitita chake wakati wa hafla fupi iliyofanyika mkoani Katavi mwishoni mwa wiki.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu(kulia) akimkabidhi kitita cha shilingi Milioni 10/- Hynes Kanumba ambaye ni mkulima mkazi wa Inyonga mkoa wa Katavi,alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika tawi la NMB Mpanda mkoani Katavi mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia katika picha kutoka kushoto ni Meneja wa NMB mkoani humo Erick Luanda,Meneja mauzo wa kampuni hiyo wa Kanda za juu kusini Petro Chinyama . Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

MKULIMA WA KATAVI ALIYEJISHINDIA MILIONI 10 ZA VODACOM AKABIDHIWA KITITA CHAKE
-Ni kupitia promosheni ya JayMillions
-Bilioni 24.3 zawasubiri wateja

ARSENAL FC WATEMBEZEWA KIPIGO NA TOTTENHAM CHA BAO 2 - 1




Wachezaji wa timu ya Tottenham wakishangilia baada ya kufunga bao la pili dakika ya 86.


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger (kushoto) akisalimiana na Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino.

Wachezaji wa timu ya Arsenal wakimpongeza Mesut Oezil (wa pili kutoka kushoto) baada ya kufunga bao pekee la timu hiyo dakika ya 11.

Danny Welbeck (katikati) akionyeshwa kadi ya njano na refa Martin Atkinson baada ya kumchezea vibaya Danny Rose.

Christian Eriksen (mbele jezi namba 23) akimtoka kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey.