Sunday, February 22, 2015

RAIS KIKWETE AWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, Mhe. William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Mhe Salva Kiir, Rais wa Burundi, Mhe Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Mrisho Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Dk Richard Sezibera wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki

Rais Jakaya Mrisho Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi rasmi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo Ijumaa Februari 20, 2015 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment