Saturday, February 14, 2015

MWENYEKITI WA VIJANA CHADEMA ATANGAZA NIA KUWANIA KITI CHA UBUNGE ARUSHA

Aliyekuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe wa arusha mjini ametangaza kugombea ubunge wa arusha mjini kupitia chadema.

Ametangaza nia baada ya kuitisha press conference na waandishi wa habari Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014
Alieleza kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless Lema
Aidha alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza umaskini
Alitoa wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu
  GREDIT Pamela Mollel wa jamiiblog

No comments:

Post a Comment