Friday, February 28, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATEMBELEA MRADI WA MAJIKO SANIFU NA KUZURU KABURI LA SOKOINE MONDULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya moja ya nyumba zinazotumia majiko sanifu wakati alipotembelea katika kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akicheza ngoma ya kimasai na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dkt. Binilith S. Mahenge, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani Arusha, ambapo ameambatana na Makamu wa Rais kwenye ziara hiyo.

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kifimbo kutoka kwa wazee wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha mara baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la kijiji hicho.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange juu ya kusafisha na kuyafanya maji kuwa salama, wakati alipotembelea sehemu ya karakana hiyo inayotumia umeme wa nguvu za jua (Solor Power Energe)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Kisioki Moitiko kuhusu utengenezaji wa majiko hayo, wakati alipotembelea kwenye karakana hiyo

Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekua Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoine, wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu Mkoani Arusha

SPORTS! TFF YASITISHA MKATABA WA KOCHA KIM POULSEN



                                                   Timu ya Taifa ya Tanzania

Hatimaye Shirikisho la Kabumbu nchini Tanzania TFF limetangaza kuvunja mkataba wake na Kocha mkuu wa Timu ya taifa ya soka ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen kwa kile kilichoelezwa maafikiano ya pamoja baina ya kocha huyo,TFF, na Serikali.
Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa Shirikisho la soka Tanzania amesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida hasa baada ya wadau mbali mbali kuona kuwa huu ni wakati wa kufanya mabadiliko ya lazima katika benchi la ufundi la Taifa Stars ambayo inajiandaa kwa mechi za kufuzu kwa Fainali za kombe la mataifa Afrika hapo mwakani zitakazofanyika nchini Morocco.
Kuhusu gharama za kuvunja mkataba na Kocha huyo Bwana Malinzi amesema serikali haitagharamia uvunjaji huo wa mkataba na kocha huyo na badala yake wapo wadau waliojitokeza kugharamia kutokana na kuona umuhimu wa kufanya mabadiliko katika kipindi hiki kwa faida ya soka la Tanzania.
Kwa Upande wake Kocha Kim Poulsen amesema na rekodi yake inaonyesha kuimarika kwa soka la Tanzania katika kipindi cha takriban miaka miwili aliyokuwa akikinoa kikosi cha Taifa Stars lakini kusitishwa mkataba ni jambo la kawaida kwa kocha yeyote baada ya kipindi fulani kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine na ndiyo sehemu ya maisha.
“Kama kocha unapoona ndiyo umefanya kazi yako,unapaswa kuangalia mbele zaidi baada ya kufanya kazi yako si lazima uendelee kuwa hapo, mnakaa na kujadiliana na kuachana kwa amani kisha unapaswa kusonga mbele,ninaondoka nikiwa najivunia kipindi nilichofundisha soka hapa,na ninawatakia kila la kheri Tanzania na Taifa Stars kwa ujumla.”alisema Poulsen.
Kuhusu Kocha mpya wa Taifa Stars Jamal Malinzi ambaye ni Rais wa TFF amesema hadi sasa wapo makocha watatu raia wa Uholanzi ni wawili na Mjerumani mmoja wanaosailiwa kwa ajili ya kumrithi Kim Poulsen,lakini moja ya vigezo Malinzi amesema kuwa ni lazima kocha huyo awe amewahi kuipeleka kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika moja ya nchi zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara.
Katika hatua nyingine kocha Salum Madadi ameteuliwa kukaimu nafasi iliyoachwa wazi na Kim Poulsen ambapo kocha huyo akisaidiwa na Hafidh Badru kutoka Zanzibar watasimamia Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyoko kwenye kalenda ya FIFA baadaye mwezi ujao.

MAREKANI KULETA UMEME AFRIKA( HASA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA)



Marekani inasema umeme utawafikia zaidi ya watu milioni 50
Wabunge nchini marekani wameidhinisha mpango wa kuleta umeme kwa zaidi ya watu millioni hamsini katika jangwa la Sahara barani Afrika na hivyo basi kutoa fursa kwa mradi huo wa serikali ya Obama kuanza kutekelezwa.
Mswada huo uliopitishwa na kamati ya maswala ya kigeni nchini humo unalenga kujenga megawati elfu ishirini barani Afrika ifikiapo mwaka 2020 na kuwafikia watu elfu hamsini ambao wanaishi bila umeme.
Mpango huo ulitangazwa na rais Obama wakati wa ziara yake barani afrika mnamo mwezi juni mwaka jana.
Mswada huo utahitajika kupitishwa na bunge la wawakilishi pamoja na lile la sineti lakini hatua hiyo ya kamati ya maswala ya kigeni ni dhihirisho tosha kwamba unuangwa mkono na pande zote za kisiasa.

KAMPENI ZINAVYOENDELEA JIMBONI KALENGA

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrfod Slaa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni wa uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Juu na chini Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kiwele katika mkutano wa kampeni juzi.

Wananchi wa kijiji cha Kiwele wakiitikia moja ya salama za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mkutano wa kampeni za chama hicho za uchaguzo mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa juzi.
Mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Grace Tendega akisalimiana na mmoja wa wazee wa kijiji cha Kiwele, baada ya mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo juzi.








BENKI YA DUNIAYASITISHA MSAADA KWA UGANDA


Wafadhili wakatiza misaada Uganda
Benki ya dunia imebana msaada wa dola milioni 90 kwa Uganda , siku chache tu baada ya Rais Yoweri Museveni kuishinisha sheriua mpya dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Benki hiyo imesema kuwa inataka kufanya tathmini yake kuhakikisha kuwa malengo yake ya maendeleo nchini Uganda katika sekta ya afya, ambayo msaada huo ulikuwa unanuiwa, hayataathirika .
Sheria iliyoidhinishwa na Rais Yoweri Museveni, ilitiwa saini Jumatatu na inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Wafadhili wengine tayari wameanza kusitisha misaada Uganda. Wahisani kama Denmark na Norway wamesema kuwa wataanza kufadhili mashirika moja kwa moja badala ya serikali.
Aslimia 20% ya bajeti ya Uganda inategemea michango ya wafadhili.
Mpaka sasa nchi tatu za Ulaya zimeamua kukata misaada yao kwa mamilioni ya dola.
Wizara ya fedha ya Uganda imesema inasubiri mawasiliano rasmi ya nchi husika, na iko tayari kukabiliana na athari za hatua hiyo.
Hadi kufikia sasa Waziri wa Fedha Wa Sweden, akiwa mjini Kampala, alisema waekezaji kutoka nchi yake watakuwa na wakati mgumu kuweka pesa zao nchini Uganda kwa sababu watakuwa na hofu kuwa sheria yo yote inaweza kupitishwa kuwadhulumu watu.
Jana serikali ya Uholanzi ilisema itazuia kwa muda misaada kwa Serikali ya Uganda. Norway na Denmark pia zimetangaza kupunguza au kusimamisha kwa muda misaada yake kwa Uganda.

SOMA WALICHOSEMA BAADHI YA WASANII KUHUSIANA NA ISSUE YA PNC NA OSTAZ JUMA


Cjapendezwa ata kidogo Na kitendo alichofanyiwa msanii uyu PNC Na Ostadh Juma Na musoma baada ya kwenda kumuomba samahan! Ichi ndicho alichofanyiwa kupigishwa magoti Na kupigwa Picha Na kurecodiwa clip ya video. Tazama Picha hii we kama shabiki Wa bongo fleva huu c udharirishaji? Huu c utumwa kabisa? Mziki ulikuwa ni sehem ya vijana wenye vipaj kujipatia ajira nw unaelekea kuwa sehem ya wapenda CFA wachache wenye visent vya magumash kuwanyanyasia vijana wadogo waliotoka kwnye familia za kimaskini Na Vipaj vyao! Je we kama shabiki Wa msanii uyu maarufu kwa hali hii unayoiona hapo utamueshm kweli Na kumpa thaman kama zaman? Au we kama Ndo ungekuwa msanii uyo baada ya kufanywa hvyo, uyo jamaa anaweza kuwa boss wako kweli? Cwez kumlaumu PNC kwa sbb ana kitu Ndo maana alikubali kufanywa hvyo! Ila we ungependa kuona mziki Wa bongo fleva Na wasanii wanaojipatia majina makubwa nchini mwishon wakiishia kufanywa HV Na wapenda CFA? @sammisago @bongo5 @hassbaby @dogojanja @djchoka @DarTalk @kingkapita

adamjumanxl Sanaa ina thamani gani katika jamii? Wengi wanaichukulia sanaa kama upotezaji muda tu, wengi hawaithamini sanaa kabisa. Na sizungumziii sanaa ya kuimba tu bali sanaa zote, hata kupiga filamu, kutaarisha mziki au uchoraji ni moja ya sanaa na inahitaji umahiri. Jamii yetu kwa ujumla haitupi sifa wanasanaa tunazostahili, sipendi mtu akinichukulia mimi kama “ MPIGA VIDEOOO” huku akiongea na mimi kwa fedheha kisa anauwezo wakulipa, kamwe huwezi kumlipa msanii naomba litambulike hilo. Pia litambulike kuna watu wameeacha kazi zao ambazo walipata mpaka madegree wakaamua kufanya sanaa, kwahiyo sio kila anayefanya sanaa ana njaa au anafanya kwa shinda. Mimi binafsi maisha yangu na yafamilia yangu yaendeshwa kwa kutumia sanaa. Mtu akinidharau kamwe sifanyi nae kazi hata kama anamipesa Hivi leo polisi akitukanwe hadharani kutakua na usalama, polisi wengine hawatakubali? Hivi mtu amdhalilishe dereva wa boda boda unafikiri ni sawa? Kwanini mtu amdhalilishe msanii alafu wana sanaa wote mnakaa kimya kama hayawahusu vile. Mimi PNC sio msanii wangu, lakini naheshimu kazi zake na jitihada zake kama msanii, mimi kama msanii naamini yeye kama msanii amepitia changamoto mpaka amefikia hapo alipo. Naamini huyu msanii ana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wanamtazama, hivi wanamchukuliaje huyu msanii kwa kudhalilishwa mbele ya umma. Baada ya kupata taswira hiyo vuta picha nyingine wanaichukuliaje sanaa kwa ujumla kama mtu anaweza akamfanya msanii hiyvo na asifanywe lolote, maana yake ni sanaa haina thamani. OSTADHI JUMA umeikosea sanaa, umewakosea wanasanaa wote na kama wewe ni msanii basi hustahili sifa hiyo ya usanii. Muombe radhi huyo kijana na jamii nzima ili ulinde heshima yako iliyobaki na heshima ya sanaa kwa ujumla.
SHUKA CHINI KUTOA MAONI YAKO TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Thursday, February 27, 2014

THE QUEEN NA SINGLE YAKE


Video: Whoa - Victoria Kimani feat AY na Prezzo







THE QUEEN IS BACK!!! kufatia mafanikio yake ya single na video yake ya kwanza katika tasnia ya mziki "MTOTO" , Victoria Kimani amekuwa katika spotlight tangu hapo, huku akiwa maefanya kazi na producers na wasanii wakali kutoka Africa, Victoria Kimani kwasasa amedondosha video ya single mpya akiwa na wasanii kutoka Africa mashariki AY na Prezzo "Whoa" ambapo ndani yake ameonyesha talent yake kwa ku-direct video hiyo.










OPRAH WINFREY KUTAYARISHA FILAMU YA MARTIN LUTHER KING ITAITWA ;SELMA.


 
 
Mchakato wa kuhakikisha mwaka huu filamu ya mwanaharakati wa Marekani, Martin Luther King inakamilika unaendelea baada ya kushindwa kukamilika mwaka jana.

Kwa mujibu wa Deadline, malkia wa talk show duniani Oprah Winfrey amejiunga na mchakato huo moja kwa moja na yeye ndiye atakuwa mtayarishaji wa filamu hiyo itakayokuwa imebeba picha ya kampeni iliyoendeshwa na Martin Luther ya August 6, 1965 kuhusu haki ya kupiga kura.

Jina la filamu hiyo ‘Selma’, linatokana na sehemu yalipoanzia matembezi ya kampeni hiyo yaliyopitia Alabama hadi Montgomery na kupelekea rais Lyndon B Jonson kutangaza kuanzishwa kwa sheria ya kupiga kura ya mwaka 1965.

Moja kati ya matukio yanayokumbukwa katika kampeni hiyo, ni tukio la Jumapili ya March 7, 1965 siku ambayo kwa mara ya kwanza lilifanyika jaribio la kufanya matembezi hayo, na kisha polisi waliyazuia na kufanya ukatili mkubwa. Jumapili hiyo ilibatizwa jina maalum ‘Bloody Sunday’

Kwa mujibu wa ripoti, Ava Duvernay ndiye aliyechaguliwa kuiongoza ‘Selma’ na kuandika script upya.

Wednesday, February 26, 2014

RIHANNA NA DRAKE WAONEKANA WAKIJIACHIA PAMOJA NDANI YA PARIS

RIRI
Drake alikuwa Paris kwa ajili ya show lakini mapaparazi wamejua kwamba Rihanna na Drake walikuwa wana-hang out pamoja weekend iliyopita sehemu mbalimbali na kupata dinner kwenye mgahawa maarufu wa L’Avenue.

Unaambiwa pia Rihanna baada kujiachia weekend yote na Drake hakuwa nyuma kwenda kushuhudia show ya Drake usiku huo.

Baada ya show wote wawili waliambatana kwenye night club na mapaparazi wanasema baada ya kujiachia usiku huo wote pamoja waliondoka kwenda Hyatt hotel ambapo Drake ndipo alipofikia.

WAZUIWA KUPINGA SHERIA YA MAVAZI MAFUPI UGANDA


Huyu ni dada aliye vaa nguo fupi inayopigwa marufuku nchini Uganda

Polisi wa Uganda wamezuia kundi la wanawake waliopanga kuandamana kupinga sheria inayopiga marufuku picha chafu.

Chini ya sheria hiyo ni marufuku kwa wanawake kuvalia mavazi mafupi, yenye kubana mwilini kiasi cha kuonekana mapaja na makalio na sheti inayoonyesha matiti.

Wanawake hao waliopanga kuandamana mjini Kampala walibeba mabano kupinga sheria mpya baadhi wakuvalia mavazi mafupi. Baadaye walikubaliwa kukusanyika katika uwanja nje ya ukumbi wa kitaifa.

MICHEZO! MOURINHO: ALALAMA KUREKODIWA KWA SIRI


Jose Mourinho kocha wa Chelsea

Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.

Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.

Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.

"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.

"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."

UGANDA YAHOFIA KUNYIMWA MISAADA



Sheria mpya dhidi ya ushoga inatoa adahabu ya maisha jela

Waziri wa mambo ya nje nchini Uganda, Sam Kutesa amesema ana wasiwasi kuwa Marekani huenda ikasitisha msaada wake kwa taifa hilo baada ya Rais Yoweri Museveni kuidhinisha sheria dhidi ya ushoga nchini humo.

Bwana Kutesa amesema kuwa watu sharti wawe na maadili na kukubali msaada.
Balozi wa Marekani nchini Uganda Scott DeLisi, awali aliitaka serikali ya Uganda, kubatilisha sheria hiyo.

Alisema alihitaji kufafanuliwa zaidi sheria hiyo, kabla ya Marekani kujua ikiwa itaendelea na mipango yake ya misaada kwa nchi hiyo hasa miradi ya kupambana dhidi ya HIV na Ukimwi..

Sheria hiyo mpya, inatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kupiga marufuku kile inachosema kusambazaa vitendo vya ushoga.

Monday, February 24, 2014

SABABU ZA LADY JAY DEE KUJIFUNZA KARATE HIZI HAPA.

Moja kati ya surprises zilizokuwepo wiki iliyopita ni pamoja na habari ya Lady Jay Dee aka Anaconda kujifua kikomando kuumudu mchezo wa Karate, habari iliyoambatana na picha zikimuonesha akifundishwa mchezo huo tena akiwa ndani ya mavazi rasmi.

Itakuwaje Jide akishakuwa fiti kwenye mitindo hatari ya karate kama Shotokan, Wado-ryu, Shito-ry na Goju-ryu? Na je, anataka kumkabili nani hasa? Haya ni kati ya maswali ambayo wengi tulijiuliza.
“Kwa sababu ninao muda wa ziada, halafu kukaa tu idol bila kufanya kitu saa zingine inaweza kupelekea mawazo yako kufikiria vitu vibaya. Kwa hiyo nikaona sio vibaya nikifanya mazoezi.” Alisema Lady Jay Dee aka Anaconda.

Alipoulizwa kama kuna mtu anataka kupigana naye alisema hakuna mtu ila anajiweka fiti tayari kwa lolote
“Hapana ni kutaka kujiweka fiti unajua kufanya mazoezi sio kwa ajili ya kutaka kupigana na mtu, ni wewe mwenyewe tu uwe vizuri ili jambo likitokea ujue jinsi ya kuji-protect.” Ameeleza. Mkali huyo wa Joto Hasira amedai kuwa ana mwalimu mzuri na kwamba yeye pia ni mwanafunzi mwenye bidii


Msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania, Judith Wambura ei kei ei Lady JayDee amepost baadhi ya picha kupitia ukurasa wake wa Facebook zinazomuonyesha akifanya mazoezi ya mchezo wa ngumi aina ya Karate kwenye kituo kimoja kinachotoa mafunzo hayo hapa jijini Dar es salaam, ingawa bado hajaweza kufahamika wazi kama msanii huyo ameanza rasmi kujifunza mchezo huo ambao ni maarufu na unaopendwa na watu wengi sana Duniani, unaweza ukatazama picha hapo chini.


















TETEMESHA KUJA NA MSANII DA PRINCE MWAKA 2014

IMG-20140224-WA0008
Huyu ni msanii baraka da prince kutoka Tetemesha record
Tetemesha Records ni moja kati ya studio zilizoanzia safari yake ya kimuziki mikoani na kisha kuhamia Dar es salaam, awali makazi ya studio hii yalikua 88.1 Mwanza Kwa Dar es salaam rasmi ilihamia 2012 na kwa sasa Tetemesha inamtambulisha msanii wake mpya aitwaye Barakah da Prince.

Msemaji wa studio hiyo amesema kuwa Barakah ndiye atakua msanii mpya kwa mwaka 2014 kutoka Tetemesha ambaye anatarajiwa kutoa video mpya iliyotayarishwa na Director Nisher kutoka Arusha.

Barakah da Prince atakua ni msanii wa nne kutambulishwa na Tetemesha Records baada ya Hussein Machozi,Sajna na C-Sir Madini.
Video na audio za Barakah zinatarajiwa kutoka hivi karibuni.

MH;SAMWELI SITA: NITAGOMBEA UENYEKITI KWENYE BUNGE MAALUMU LA KATIBA KWANI NINA SIFA.






Waziri Samweli Sita.
Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Dodoma.
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema atagombea uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu anaamini kuwa ana sifa za kutosha.
Hii ni mara ya kwanza kwa Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa kuweka wazi uamuzi wake huo. Mwingine anayetajwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Sifa za mtu anayepaswa kuongoza Bunge hilo ni kuwa na shahada ya sheria kutoka katika chuo kinachotambulika pia kuwa na uzoefu wa kuendesha mijadala kama ya Bunge.
Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema pamoja na propaganda chafu zinazoenezwa dhidi yake, hatakata tamaa na kwamba ataendelea na msimamo wake huo ili nchi ipate Katiba bora.
“Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha sifa za mtu anayetakiwa kuwa mwenyekiti na mimi nina sifa na nina mipango mizuri ya kuwafanya Watanzania wapate Katiba bora kama ndoto ya Rais wetu (Jakaya Kikwete) ilivyo,” alisema.
Alipoulizwa kuhusu njama za kumzuia asigombee nafasi hiyo, Sitta alisema “Haishangazi watu hao kutumia mbinu chafu… Hawana maadili, ndiyo maana wananihofia lakini sishtuki hata kidogo.”
Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema wabaya wake wamekuwa wakieneza maneno ya uongo kwamba ikiwa atakalia kiti hicho, atasimamia mpango wa Serikali tatu.
“Wanasema Sitta ataruhusu Serikali tatu, sasa nashangaa maana wajumbe ndiyo wenye mamlaka hayo… wanaeneza propaganda kuwa nina mkataba na wapinzani ndiyo maana wananiunga mkono. Wanasema mambo ya ovyo kabisa,” alisema.
Sitta alisema wapinzani kama walivyo wajumbe wengine kutoka CCM na makundi mengine, wanamuunga mkono kwa kuwa wanaamini akikalia kiti hicho ataendesha Bunge hilo kwa misingi ya uwazi na haki.
“Mimi sina mkataba na wapinzani ila wao kama watu wengine wananiunga mkono kwa sababu wanajua nitatenda haki, nina rekodi nzuri katika kuliendesha Bunge la Tisa wala hiyo haina mashaka,” alisisitiza Sitta.
Sitta na Chenge
Kumekuwa na msuguano na kampeni za chini chini kati ya kundi la Sitta na Chenge, lakini habari zilizopatikana jana kabla ya Sitta kutangaza kuwania nafasi hiyo, zilisema CCM walikuwa wakikusudia kuwaondoa makada hao, na kumpendekeza Mathias Chikawe badala yao.
Ilielezwa kuwa hatua hiyo imefikiwa kutokana na mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho unaotokana na wapambe wa makada hao kuanza kupakana matope.
Hata hivyo Chikawe alisema hana taarifa yoyote kuhusu mpango huo. “Ahaaa! Sina taarifa hiyo, sijawahi kufikiria kushika nafasi hiyo, wewe (mwandishi) ndiyo unaniambia na nimeshtuka sana, lakini nitafuatilia,” alisema Chikawe.
Kwa upande wake, Chenge juzi alisema hana sababu ya kulumbana na watu aliowaita kuwa hawataki kuelewa na kwamba tayari CCM kilikuwa kimetoa mwelekeo wake.
Hata hivyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema chama hicho hakijatoa msimamo wa mtu kinayetaka agombee nafasi hiyo kwani hakuna kikao chochote kilichojadili suala hilo.
“Kama uamuzi unafanywa, lazima vikao vya chama vikae, lakini hadi sasa kwa uelewa wangu hakuna kikao chochote cha chama ambacho kimeketi na kuamua suala hilo,” alisema Nnauye.

Kauli ya Nnauye iliungwa mkono na ile ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, William Lukuvi ambaye alisema chama hakijatoa mwongozo wowote kuhusu suala hilo kwa kuwa muda wake bado.
“Chama hakijatoa mwongozo wowote ingawa tunajua watu wameanza kuumana kwa hilo, wako kama saba,” alisema Lukuvi.
Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), alikuwa akijibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake kwamba ndiye anayeshawishi Sitta asiwe mmoja wa wagombea katika kinyang’anyiro hicho ili kulinda mwonekano wa Spika wa Bunge, Anna Makinda.
“Wanahofia endapo Sitta atafanikiwa kupata uenyekiti na kuendesha vizuri Bunge na Makinda akaja kuendesha Bunge la Bajeti ataonekana kupwaya sana,” kilisema chanzo chetu.
Lukuvi alikanusha kuhusika na mpango huo akisema: “Mimi nahusika vipi kwenye hilo. Kwanza kama chama hatujatoa mwongozo lakini hatuwezi kutoa mwongozo kabla Bunge halijatoa kanuni za namna ya kumpata mwenyekiti.”
Lukuvi alikiri kufahamu kuwapo kwa vita ya uenyekiti, lakini akasema yeye haoni mantiki ya kuhusishwa kwake. “Mimi najua watu wameshaanza kuumana lakini kwa nini sasa, wakati hata kanuni hazijatoka na chama hakijatoa mwongozo,” alihoji.

Sunday, February 23, 2014

NILIVYOKUTANA NA DIRECTOR WA MAXCOM BWANA ERIC HAULE





Hapa ni mimi Richard (kushoto) na bwana Eric Haule alivyo nitembelea.

SNURA KUJA NA USHAHARIBU MWANZONI MWA MWEZI WA TATU STAY TUNE....

 
Kaa tayari kwa ajili ya wimbo huu mpya wa Snura Mushi. Unaojulikana kama Ushaharibu, Huu wimbo Unawazungumzia watu wenye tabia yakuiangalia leo na kuidharau kesho, kwa mfano kuna watu Wamezungumziwa umo ndani kuwa ”Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha,huna pakulala shida Umezizidisha,

Na haya ndio mashahiri ya wimbo huu wa ushaharibu….

Verse ya 1
Unatafuta kick na upo kwenye muziki, Ndio kwanza unahit umetukana mashabiki
Ulikimbia wazazi ukayafanye mabaya, Tena ulimwaga radhi na umepata miwaya
Ulitukana wakunga na wakati una mimba, Ulijiona mjanja kumbe wewe ndio mjinga
Umeombewa kulala umekojoa kitandani, Umetutia haibu kwenye chumba cha jirani
Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha , Una pakulala shida umezizidisha,
Kuto kujiamini umetapatapa, Umeliacha dume umelamba galasa.x 2
Chorus
Ndo basi tena ushaharibu,uuuhu
Kujifanya mjuaji ushahaaribuuuuhu
Umejitia ufundi ushaharibuuuuhu
Jipange upya ushaharibuuuuuuhu x 2
Vers ya 2
Unataka heshima kutoka kwa wako wana , Mbele ya watoto wako matusi unatukana,
Baba yupo ICU mmeukata umeme, Tena mmeshaharibu wacheni mimi niseme.
Nilipokuwa chini ulikuwa unitaki,leo hii niko juu unataka urafiki.
Umechomwa sindano na umemeza vidonge, Ulivyo na dharau eti umekunywa pombe.
Uliuza nyumba kwa ugumu wa maisha , Una pakulala shida umezizidisha,
Kuto kujiamini umetapatapa, Umeliacha dume umelamba galasa.x 2
chorus
Ndo basi tena ushaharibu,uuuhu
Kujifanya mjuaji ushahaaribuuuu
Umejitia ufundi ushaharibuuuu
Jipange upya ushaharibuuuuh x 2
Bridge
Ebu jaribu sasa kufikiria jambo usiharibu, Umeharibu sasa limekushuka sura ina haibu.
Ebu chunga uchunge uchungweee usiharibu tena.
Hk chunga uchungwe usiharibu tena,
We Snura chunga Uchungweeee.
Baby talha chungwa uchungweeeee,
Na mapacha chungwa uchungweeee msiharibu tenaa.
Ebu chungwa chunga uchungweee UsiharibuTenaaaaaaaaaaaaaaaaa
Kaa tayari kuupokea wimbo huu mzuri mwanzoni mwa mwenzi wa tatu.

WAZIRI WA FEZA : SERIKALI HAITARUDI NYUMA MATUMIZI YA MASHINE ZA EFD;




Waziri wa feza Mh, Saada Salum Mkuya

Leo 22/02/2014 Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya amesema kuwa Serikli haitarudi nyuma kwenye matumizi ya mashine za kielectroniki, EFD. Aliyasema hayo katika mahafali ya chuo cha TRA.

Waziri amesema wafanyaabiasha waache visingizio vinavyotokana na wao kutokuelewa vizuri juu ya mashine hizo, pia amesisitiza kuwa sisi walaji tunaponunua biadhaa tudai risiti.

WATANZANIA inabidi tuelewe kwamba HATUWEZI kuendelea bila kuwa na mifumo dhabiti ya KODI!

TUJIULIZE,
Hivi kweli mfumo wa kulipishana kodi kwa kukadiriwa kwa kutumia busara na utaalamu wa mkadiriaji wa TRA uko sahihi au umepitwa na wakati?. Nadhani umepitwa na wakati na kuchochea kushamiri kwa vitendo vya rushwa.
Hivi endapo mfanyabiashara ananunua kwa gharama yake na anarejeshewa pesa yake kuipitia malipo yake ya kodi, si ni kama amepewa bure?, mathematically ni sawa na kusema umetoa nne ukapata nne mwisho wa siku unakuwa umetoa sifuri.

Hivi ELIMU ndugu zetu wa TRA si wamejitahidi kuitoa ya kutosha?. Katika baadhi ya mikutano ambayo TRA wamekuwa wakiifanya na wafanyabiashara, mahudhurio ya wafanyabiashara yamekuwa ni hafifu sana kiasi cha kusikitisha, je hapo TRA watalaumiwa hawajatoa elimu ya kutosha?, je lawama hii inawatendea haki TRA?, au wangewafuata kwenye biashara zenu kuwapa elimu huko?
Matengezo ya mashine, je si ilishafahaishwa na TRA kwamza matengenezo ya mashine ni BURE walau kwa mwaka wa kwanza wa matumizi ya mashine?, na baada ya mwaka wa kwanza kupita gharama ya matengezo ya mashine endapo itaharibika italipwa na mfanyabiashara na katika kipindi ambacho mfanyabiashara analipia kodi atarejeshewa kiasi alichotengeneza mashine ile kwani kimsingi mashine hizo ni za TRA.

UONGO UNAOENEZWA, kuna wanaoeneza uongo kuwa mashine hizi zinakata asilimia 18, hiyo siyo kweli. HAZIKATI KIASI CHOCHOTE. Kimsingi ni kuwa badala ya kutumia VITABU sasa tunkwenda kidigitali unabofya na risiti inatoka. Tafuteni majedwali ya KODI kwenye ofisi za TRA. Kwa kuwasaidia tu wanaotaka kujua.

Mfanyabiashara akiuza chini ya shilingi 0 na shilingi milioni 4 hakatwi KODI. Huyu anahitaji kukua kwa kutumia senti zake zote kujikuza kibiashara.
Kati ya shilingi 4Million na 7.5Million kodi ni shilingi 100,000/= kwa mwaka.
Kati ya shilingi 7.5Million na 11.5Million kodi ni shilingi 212,000/= kwa mwaka.
Kati ya shilingi 11.5Million na 16Million kodi ni shilling 364,000/= kwa mwaka.
Kati ya shiling 16Million na 20Million kodi ni shilling 575,000/= kwa mwaka.
Kiasi kinachozidi 20M, hairuhusiwi kukadiriwa ila mfanyabiashara atatakiwa na sheria aandae audited accounts, hapa mfanyabiashara atatozwa kodi kulingana faida aliyoipata, namna hii kitu inavyofanyakazi wasiliana na hii namba ya bure ya TRA 0713800333 au wasiliana na ofisi y TRA iliyo karibu nawe.
Kama tuliweza kuhama ANALOGIA na kuingia DIGITALI tunashindwaje KUHAMA kutoka kwenye kwenye VITABU na kuhamia kwenye EFD machine kwa ajili ya kutolea risiti?
WAFANYABIASHARA TUACHE UJANJA UJANJA, TULIPE KODI!

Saturday, February 22, 2014

ANGALIA PICHA CHADEMA WAANZA KAMPENI ZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA


Viongozi na wanachama wa CHADEMA wakielekea kwenye makumbusho ya Chifu mkwawa kabla ya kuanza kampeni hizo

Hapa wakitoka kwenye Makumbusho ya Chifu Mkwawa huku hali ya hewa ikiwa ni ya ubishi kutokana na mvua kubwa kunyesha

Mgombea wa Ubunge kupitia chama cha CHADEMA akinadiwa na Katibu mkuu wa chama hicho Dr. W. Slaa wakati wa kampeni hizo zilizoanza hii leo katika jimbo la Kalenga

MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA JIMBO LA KALENGA WAZUIWA NA POLISI IRINGA

Polisi mkoani Iringa wakiwa wameuzuia msafara wa mgombea ubunge jimbo la Kalenga, Bi Grace Tendega kupitia Chadema kwa madai hawakuwa na kibali cha kufanya maandamano hayo ya magari hapa ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo ulikuwa ukitokea maeneo ya Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi ili kuchukua fomu.


Friday, February 21, 2014

DIAMOND KUHUDHURIA TUZO ZA 'AFRIMMA' ZITAKAZOFANYIKA TEXAS MAREKANI, ZITAHUSISHA WASANII WAKUBWA AFRIKA.


July 26 mwaka huu, wasanii wengi wakubwa Afrika kutoka katika mataifa ya 17 watakutana Dallas, Texas, Marekani kuhudhuria utoaji wa tuzo za kiafrika zinazojulikana kama ‘AFRIMMA Awards’, na tayari Diamond Platinumz tayari ameshaonesha uthibitisho wa kuwa katika daftari la mahudhurio siku hiyo.
Diamond amepost kwenye Instagram video inayomuonesha akifanya promo maalum iliyoandaliwa na watayarishaji akiwaambia mashabiki kwa swag za kimarekani kuwa atakuwepo siku hiyo, na kisha akaisindikiza na maneno yanayosomeka, “Yess! i'll be ryt there....Afrimma Awards 26/07/2014 Texas, Dallas (USA).
Tuzo hizo zilizoandaliwa na Big A Entertainment na African Muzik Magazine, zimelenga katika kuwatunuku wasanii mbalimbali wakubwa wa Afrika waliopo duniani kote na itagusa nyanja mbalimbali za burudani ikiwa ni pamoja na wasanii wa muziki, wachezea santuri aka Dj’s, watayarishaji wa muziki, mameneja na watu wanaousapoti utamaduni wa Afrika
Tuzo hizo zinatarajiwa kusindikizwa na vicheko vya mara kwa mara kwa kuwa mshereheshaji wa shughuli hiyo ni mchekeshaji maarufu wa kimataifa, The Basket Mouth na atakuwa na muigizaji mrembo wa Nollywood, Juliet Ibrahim.