Thursday, February 27, 2014

OPRAH WINFREY KUTAYARISHA FILAMU YA MARTIN LUTHER KING ITAITWA ;SELMA.


 
 
Mchakato wa kuhakikisha mwaka huu filamu ya mwanaharakati wa Marekani, Martin Luther King inakamilika unaendelea baada ya kushindwa kukamilika mwaka jana.

Kwa mujibu wa Deadline, malkia wa talk show duniani Oprah Winfrey amejiunga na mchakato huo moja kwa moja na yeye ndiye atakuwa mtayarishaji wa filamu hiyo itakayokuwa imebeba picha ya kampeni iliyoendeshwa na Martin Luther ya August 6, 1965 kuhusu haki ya kupiga kura.

Jina la filamu hiyo ‘Selma’, linatokana na sehemu yalipoanzia matembezi ya kampeni hiyo yaliyopitia Alabama hadi Montgomery na kupelekea rais Lyndon B Jonson kutangaza kuanzishwa kwa sheria ya kupiga kura ya mwaka 1965.

Moja kati ya matukio yanayokumbukwa katika kampeni hiyo, ni tukio la Jumapili ya March 7, 1965 siku ambayo kwa mara ya kwanza lilifanyika jaribio la kufanya matembezi hayo, na kisha polisi waliyazuia na kufanya ukatili mkubwa. Jumapili hiyo ilibatizwa jina maalum ‘Bloody Sunday’

Kwa mujibu wa ripoti, Ava Duvernay ndiye aliyechaguliwa kuiongoza ‘Selma’ na kuandika script upya.

No comments:

Post a Comment