Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifunguza majadiliano
kuhusu mazingira yanayochangia kuendenea kwa vitendo vya kigaidi.
majadiliano hayo yamefanyika siku ya Jumatano yakitangulia mkutano wa
nne utakafanya tathmini kuhusu Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibidi
Ugaidi. Katika salamu zake, Katibu Mkuu amesema hakuna sababu iwayo
yoyote ile inayoweza kuhalalisha ugaidi. Kulia kwake ni Rais wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw, John Ashe .
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Pereira Silima ( Mb) akichangia majadiliano hayo. Naibu Waziri
anaongoza ujumbe wa Tanzania. Katika mchango wake amesema kuna kila
sababu ya kuhakikisha kuwa vijana hasa wale wasiokuwa na ajira
hawashawishiki kujiunga na uhafidhina na kwamba kutoka na changamoto
mbalimbali zikiwamo za ukubwa wa mipaka baina ya nchi na nchi, tishio la
ugaidi na uhafidhina kwa nchi za Afrika Mashariki ni kubwa.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu ukiongozwa na Naibu Waziri Silima
walioketi nyuma ni Bw. Abdalla Khamis Afisa katika Uwakilishi wa
Kudumu na Bw. David Hiza. Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi na
Mratibu Kituo cha Kitaifa cha Kuratibu Mapambano dhidi ya Ugaidi.
Wajumbe ukumbini
No comments:
Post a Comment