Mapigano yameendelea kwa siku ya pili kati ya wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wale kutoka Rwanda kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Milio ya risasi iliyodumu karibu saa mbili iliripotiwa kusikika mapema Alhamisi.
Pande hizo zimekuwa zikishutumiana kwa kuanza mapigano.
Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo inasema kuwa vikosi vya Rwanda viliingia Mashariki mwa Congo, kumteka nyara na kumuua mwanajeshi wake, huku nayo Rwanda ikisema kuwa wanajeshi wa Congo ndio walioingia nchini mwao na kuwafyatulia risasi.
Makabiliano yalianza Jumatano katika kijiji cha Kanyesheza, kilomita 20 kutoka Goma mji mkuu wa mkoa huo na kudumu kwa saa kadhaa.
Wanajeshi hao walishambuliana kwa zana nzito za kivita, asubuhi na mapema kwa mujibu wa mmoja wa walioshuhudia makabiliano hayo.
Pande hizo mbili zimekuwa zikilaumiana huku afisaa mmoja wa Rwanda akidai kuwa wanajeshi wa DRC ndio waliowashambulia kwanza.
Hata hivyo duru zinasema kuwa hapakuwa na majeruhi ingawa wanajeshi walikuwa wanafyuatuliana risasi kiholela. Makabiliano ya leo yamezuka baada ya pande hizo mbili kushambuliana Jumatano
No comments:
Post a Comment