Friday, April 18, 2014

PICHA YA RAIS ALIYE NYOA KIDUKU KIM JONG-UN YALETA UTATA MJINI LONDONI

Picha ya rais wa Korea kusin KIM JONG-UN

Viongozi wa Korea Kaskazini walitembelea saluni moja iliyoko mjini London, kutaka kujua ni kwa nini walitumia picha ya kiongozi wao Kim Jong-un katika bango la kibiashara.
Bango hilo lenya picha ya rais huyo, lilitumiwa kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa katika saluni moja.

Bango hilo katika M&M Hair Academy lilikuwa na picha ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini pamoja na maneno “Bad Hair Day?” yaani je unahitaji kutengezwa nywele?….
Kinyozi kwa jina Karim Nabbach alisema kuwa maaafisa wa ubalozi wa Korea walifukuzwa na mkurugenzi wa saluni hiyo walipojaribu kuingia katika saluni hiyo huku wakiwa wakali wa maneno.
Polisi nao kwa upande wao wamesema kuwa walizungumza na pande zote mbili husika na hakuna kosa lolote lilibainika.
Saluni hiyo ilibandika bango hilo tarehe 9 Aprili na keshoye wakapokea wageni wawili waliodai kuwa walikuwa maafisaa wa ubalozi wa korea kaskazini walio taka kumwona mkurugenzi wa saluni hiyo
Picha iliyozua mgogoro
Karim Nabbach amenukuliwa akisema kuwa waliweka mabango ya kutangaza kupunguzwa kwa bei ya kunyolewa kwa wanaume katika mwezi Aprili.
Bango hilo lilitokana na habari za hivi karibuni kuwa wanaume wa Korea wametakiwa kunyoa nywele kwa mtindo mmoja tu kama alivyonyolewa Rais Kim Jong Un.
Mkurugenzi wa saluni hiyo anasemekana kuwa aliwaeleza wageni wake kuwa walikuwa nchini uingereza nchi ya kidemokrasia na kuwataka waondoke kwenye saluni yake na kisha aliwafahamisha polisi kuhusu yaliyotokea pamoja na ubalozi wa Korea Kaskazini kuwa alikuwa amewasiliana na polisi.
Akizungumza na kipindi cha BBC radio 4 Karim Nabbach alisema kuwa kutoka wakati ule hawakupata shida yeyote ile na kuwa licha ya hayo bango hilo liliwavutia wateja wengi waliodhania kuwa lilikuwa la kuchekesha.
Wakati huo huo aliongeza kuwa bango hilo halikuwa linatumika kisiasa mbali lilitumika tu katika matangazo yao ya kibiashara ili kuwavutia wateja.
Mwezi uliopita Radio Free Asia iliripoti kwamba wanafunzi wa kiume katika vyuo vikuu vya korea kaskazini walitakiwa kunyoa nywele yao kwa mtindo sawa na ule wa kiongozi wao.

No comments:

Post a Comment