Mods nawaomba sana msiunganishe huu uzi na kama ni lazima kufanya hivyo basi nawaomba muache walau kwa masaa machache tu ili mh.aweze kupata fursa ya kusoma nilichoandika

Mh.Lema nakuomba na kukusihi usiwashirikishwe viongozi wako wa UKAWA katika uamuzi wako wa kujitoa katika hilo bunge "fake" zaidi ya kuwapa taarifa tu na kisha utimize dhamira yako.

Mh.Lema nina imani asilimia 97 kuwa hao viongozi wako watakushauru vinginevyo kwani si watu wenye misimanmo "thabiti" na wana imani potofu kuhusu "maridhiano".Na katika wote hao katu usimsikilize kabisa mtu anaeitwa James Mbatia.Huyu ni mtu ambae anaongoza kuamini katika "maridhiano uchwara".Hapo Dodoma hakuna kitu kinachoitwa maridhiano zaidi ya usanii wa kisiasa kudanganya umma wa watanzania.

Mh.Lema kumbuka wako watakauokubeza kwa uamuzi wako huu lakini pia kumbuka hili ni "pigo" kwao kwani wanatambua kuwepo kwenu katika huo mchakato, ni kuupa uhalali kama sio baraka kwani ni wazi mkijitio sasa ni "dosari" kwabu kwa mchakato mzima, hivyo uwepo wenu hapo ni sababu tosha ya wao hapo baadae kuja kuwabeza kuwa hata nyinyi mlishiriki na posho mlichukua na hawata sita kuja kuwaita "wanafiki".

Kuhusu posho usijali kwani hata baba wa taifa alikufa masikini(japokuwa si kama nitakavyokufa mimi na wewe) kwa kuweka mbele uzalendo sasa nawe ukifa masikini cha ajabu ni nini hapo?

Wangapi wamekufa matajiri kwa kudhuluma mataifa yao lakini leo hawana heshima mbele wa macho ya walimwengu wa leo?Leo hii hadhi ya Mobutu na Mandela zinalingana?Hadhi ya Nyerere na Mobutu zinalingana?

Ni bora ukajitoa leo kulinda heshima yako na utakuja kuwa na uhalali wa kuhamasisha umma kuikataa hiyo katiba kwa utakuwa hukushiriki kuitengeneza.

May God blees you!

Mzalendo wa kwel