Saturday, March 29, 2014

KAMATI YAMRIDHIANO YAKUBALINA KURA YA WAZI NA SIRI ZOTE KUTUMIKA


Hatimaye Bunge Maalumu la Katiba limeridhia wajumbe kupiga kura ya wazi na siri katika kupitia mchakato wa rasimu ya katiba mpya.
Maamuzi hayo yalitolewa jana jioni baada ya Kamati ya Maridhiano iliyokutana kuanzia juzi usiku hadi jana mchana kukubaliana kuwa na kura za aina mbili, kufuatia mvutano mkubwa ulioibuka baina ya wajumbe hao.
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, aliamua kuunda kamati hiyo baada ya mapendekezo kutokana na michango iliyotolewa na wajumbe katika mjadala wa juzi, ambapo Freeman Mbowe, alikuwa mmoja wa wajumbe waliotoa hoja hiyo.
Sitta aliunda kamati hiyo iliyokuwa na wajumbe Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim LIpumba,   
Askofu (mstaafu) Donald Mtetemela na Vuai Ali Vuai.
Kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, Sitta aliwaruhusu wanakamati hiyo kila mmoja kutoa yale waliyoamua.
Akiongea kwa niaba ya Mbowe, Johna Mnyika alisema mazungumzo yamesaidia kupiga hatua moja mbele ingawa ya kukubaliana kutokubaliana.
“Sisi tulikuwa na mtazamo kuwa kura iwe ya siri lakini wengine walitaka kura ya wazi. Pamoja na majadiliano yote wenzetu waliona wana uhuru wa kupiga kura ya wazi, ilibidi tufike hatua ya kuamua kulivusha taifa ili lisonge mbele.”
Alisema walipendekeza maamuzi haya yafanywe kwa kura ya wazi lakini wao waliamua yafanyike kwa siri.
Alisema wameamua anayetaka kupiga kura ya wazi apige ya wazi na atakayeamua ya siri iwe ya siri. Matokeo yatakayopatikana kwa minajili ya kupiga hatua moja mbele na kulisogeza taifa mbele.
“Wenye kukubaliana na kura ya wazi watakuwa wengi, na wanaotaka kura ya siri watasema hapana na kwa vyovyote walio wengi watashinda,”
Alisema utaratibu huu wa mashauriano ni vizuri utumike hata pale ambapo hawakubaliani ili kupiga hatua mbele.
“Sisi hatuna njama zozote za kuvuruga bunge hili kwa sababu tumepigania sana jambo hili na kutaka Watanzania wapate Katiba iliyo bora,” alisema.
Alisema wapinzani hawana dhamira ya kukwamisha mchakato wa Katiba. “Kwa sababu kuna magazeti yamemnukuu Mheshimiwa Rais …

PROFESA IBRAHIM LIPUMBA
Alisema unapofanya mchanganyiko wa kura ya wazi na siri ni kuwafanya wale wanaotaka kura ya siri kutopata haki yao lakini Ili tusonge mbele na kuanza kujadili Rasimu ya Katiba, tupige kura ya wazi na siri tufanya maamuzi.
Lakini hii si kura nzuri ni kura itakayotupa vikwazo. “Mimi binafsi ntasema hapana kwa jambo ambalo limeletwa juu ya meza kulifanyia maamuzi. Lakini ili tusonge mbele tumeona tulifanyie maamuzi hayo.
“Natoa wito kwa CCM pamoja na kuwa wengi ni vyema kuheshimu mawazo ya wachache “, alisema na kuongeza kuwa CCM wangekuwa na busara wangeweza kuongeza idadi ya kamati kwa kuweka mbele ya Watanzania

No comments:

Post a Comment