Saturday, January 10, 2015

GODBLESS LEMA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KINONDONI OCTOBER MWAKA HUU

Katika kikao chake na waandishi wa habari mchana huu katika hotel ya Snowcrest jijini Arusha, Lema amesema anaenda kupambana na Iddi Azan kwenye jimbo la Kinondoni ktk uchaguzi mkuu ujao mwezi October mwaka huu. Akielezea nia yake hiyo mbele ya mamia ya waandishi wa habari, Lema amesema anataka kuleta mapinduzi ya fikra kwa wana kinondoni na kuijenga ngome imara ya chadema jimboni hapo. Alisema mpango wake huo alikuwa nao toka mwaka 2013 pale alipovuliwa ubunge na alitafakari kujiingiza kwenye changamoto mpya kisiasa ifikapo mwaka 2015.
“Wana wa Arusha wasiwe wanyonge, kamanda wao naenda kupambana kwenye uwanja mwingine wa vita lakin wajue tupo pamoja” Alinukuliwa akisema bw. Lema. Hata hivyo alikwepa kujibu swali la mwandishi wa Radio 5 aliyetaka kujua kama pengine ni mbinu ya Lema kukwepa aibu ya kushindwa kwenye uchaguzi huu ikizingatiwa historia yake tata ya utekelezaji wa ahadi zake alizotoa mwaka 2010 na pia ushindani mkali unaomkabili ndani ya chama chake. Imefahamika kuwa wanachama zaidi ya 30 wameshatangaza waziwazi kuchuana na Lema kwenye uchaguzi wa Octoba.
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya Lema kukimbia changamoto na kujaribu karata yake mahali pengine

No comments:

Post a Comment