Sunday, July 20, 2014

VIONGOZI WA CHADEMA WAJIUZULU MKOANI KIGOMA



Viongozi wa CHADEMA Mkoa waliojiuzuru ,kuoka kushoto ni Msafi Wamarwa aliyekuwa Katibu wa chama Mkoa,wakatika ni Ramadhani Kasisiko aliye kuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa pamoja Malumba Simba liyekuwa Katibu wa BAWACHA
Na Mwandishi wetu,Kigoma
VIONGOZI wa chama cha maendeleo na demokrasia (CHADEMA)wamejiuzulu leo rasmi nyadhifa zao pamoja na uanachama wa chama hicho.
Viongozi hao waliotangaza kujiuzuru nafasi zao katika chama hicho mbele ya waandishi wa habari ni Jafari Ramadhani Kasisiko ambaye alikuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa,Msafiri Hussen Wamarwa amabye alikuwa katibu wa chama Mkoa pamoja na Malunga Masoud Simba alikuwa Kaibu wa Baraza la wanawake BAWACHA.
Akitangaza uamuzi kwa niaba ya wenzake aliyekuwa Mwenyekii wa CHADEMA Jafari Kasisiko alisema kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya kuona CHADEMA kimepoteza sifa ya kuwa chama cha demokrasia na kuwa chama cha wababe.

No comments:

Post a Comment