Thursday, July 31, 2014

BASI LA MORO BEST LAPATA AJALI

Capture5 
July 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.

Capture4 
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.

Capture3 
Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.
Taarifa ya kamanda wa Polisi inasema katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5,Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari jingine na kwenda kuligonga basi hilo.

DIMOND APOKELEWA AIRPORT KWA SHANGWE NI SHIDAAAA!!!!

30dmnd 

Ni mamia ya wakazi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioamua kwenda kumpokea Diamond Platnumz baada ya safari yake ya kutoka Marekani ambayo imekua njema kwa Tanzania baada ya kurudi na tuzo.
Mapokezi yalianzia  uwanja wa Julius Nyerere International Airpot kisha msafara ukaelekea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ukipitia Buguruni,Kariakoo na baadae kumalizia nyumbani kwake Sinza.
Wakati akiwa kwenye gari ya wazi Diamond Platnumz muda wote alikua kaishikilia tuzo yake aliyoipata Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA ambapo kwa upande wake ameibuka na ushindi wa tuzo ya Msanii bora wa Afrika Mashariki.
Ratiba ya Diamond kuingia Tanzania ilikua iwe jioni ya Jana July 29 lakini kutokana na sababu walizosema zilizokuwa nje ya uwezo wao safari yao ikasogezwa mpaka leo July 30 na alifanikiwa kuingia saa 1 asubuhi.
Ingawa hali ya hewa ilikua imetawaliwa na manyunyu pamoja mvua ndogo ndogo,Hizi ni baadhi ya picha za mashabiki waliojitokeza kumpokea Diamond.








GREDIT MILLARD AYO

SERIKALI YAPIGA STOP AJIRA 70 ZA UHAMIAJI

  Na Ibrahim Yamola na Beatrice Moses, Mwananchi
Dar es Salaam.
Serikali imesitisha ajira 70 za konstebo na koplo wa Uhamiaji baada ya kuzuka kwa tuhuma za upendeleo uliokithiri wakati wa usaili.
Agizo hilo la Serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil ambaye ametengua kauli yake ikiwa ni wiki mbili tu tangu alipozitangaza nafasi hizo.
Mara baada ya ajira hizo kutangazwa, wadau mbalimbali walianza kulalamika kwa madai kwamba nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo kwa ndugu na marafiki wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji.
Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isack Nantanga ilisema Abdulwakil amesitisha ajira hizo baada ya kuzagaa kwa tuhuma za upendeleo kwa ndugu na jamaa wa watumishi wa idara hiyo.
“Kutokana na kusitishwa kwa zoezi hili, waombaji wote walioitwa na kutakiwa kuripoti makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Agosti 5 mwaka huu sasa watatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena.”
Ilisema Abdulwakil ameunda kamati ndogo kuchunguza tuhuma hizo na ikikamilika ndipo uamuzi utakapofanyika.
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwamba kulikuwapo na upendeleo wakati wa usaili.
Julai 13 mwaka huu, Idara ya Uhamiaji ilifanya usaili wa kujaza nafasi 70 za mkaguzi msaidizi wa Uhamiaji uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waliopita ni 6,115 ambao walichujwa na kufika 1,681 walioingia katika kinyang’anyiro cha kusaka watumishi 70.
Utata ulivyo
Baadhi ya waliotakiwa kuripoti Agosti 5 mwaka huu wanaodaiwa kuwa ni watoto au ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo ambao majina yao yalisambaa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni: Abdulhaq Amin Mandemla – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Amin Mandemla, Alphonce Kishe – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Aleluya Kishe na Asha Burhani Idd – ndugu wa Ofisa Uhamiaji na Tatu Burhani Idd.
Wengine ni Beatrice Temba – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Joseph Kasike, Geofrey Justine Mhagama – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Rose Mhagama, Iginga Daniel Mgendi – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Daniel Mgendi na Issack Michael Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Makwinya.
John Alfred Mungulu – mtoto wa Ofisa, Uhamiaji Alfred Mungulu, Joseph A. Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji, Milambo, Michael J. Choma – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, John Choma, Shimba H Zakayo – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Zakayo Mchele na Upendo E. Mgonja - mtoto wa Ofisa Uhamiaji Mgonja.
Wengine ni Vaileth A. Kidesu – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Adam Kidesu, Elizabeth Edward – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Edward Martin, Ester Mahirane – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Mahirane na Basil Lucian John – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Lucian.
Frank E Kajura- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Kajura, Jacob P. Ulungi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Magnus Ulungi, Janeth John Milinga – ndugu wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Milinga, Janeth R Lukuwi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji Eliza Lukuwi, Joseph N. Yondani – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Mary Yondani.
Leila Khatib Irovya - Mtoto wa Ofisa Uhamiaji Abbas Irovya, Lucian F. Mlula – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Mlula, Neema Kasian Lukosi- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Zubeda Abbas, Pendo D. Gambadu – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Gambadu, Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward Mwenda.
Theresia Ernest Kalunde – mtoto wa Ernest Kalunde, Veronica G Vitalis – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Vitalis Mlay, Victor G. Mlay- mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Vitalis Mlay na Catherine J. Mapunda- mtoto wa Ofisa, Lucy Mapunda.
Uhamiaji wajitetea
Idara ya Uhamiaji imekiri kupokea malalamiko yaliyotolewa dhidi yake.
Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Rosemary Mkandala alisema jana kuwa wamepokea tuhuma hizo na wanazifanyia kazi.
“Ninaomba tu wale ambao walishiriki kwenye usaili huo na wana malalamiko wayawasilishe rasmi ili tuweze kuyafanyia kazi. Suala linachunguzwa sasa na matokeo yake yatabainisha kama kuna ukweli au la,” alisema

CHANZO: MWANACHI

Wednesday, July 30, 2014

ZITO ZUBERI: KABWE SINA IMANI NA UKAWA


ZITTO KABWE
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara ya kwanza ameibuka na kupingana na harakati za Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Zitto amesema hana uhakika wala hauamini Ukawa kama utakuwa umoja endelevu hadi kufikia Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kwa sababu si mara ya kwanza vyama vya upinzani kuungana na kugawanyika.
Mbali ya kutokuwa na imani na umoja huo, pia ameitaka Serikali kusitisha mchakato wa Katiba Mpya hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika.
Alisema ni vema mchakato huo ukasitishwa kwa sasa, kwani inaonekana wajumbe wa Bunge hilo wanafuja fedha za umma.
Zitto alitoa kauli hiyo jana, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha redio cha Clouds cha jijini Dar es Salaam.
Alisema Watanzania wanakabiliwa na changamoto nyingi na si Katiba pekee.
Alisema siku zote Watanzania wamekuwa wakipenda kuwa na upinzani imara ambao watu wanaweka tofauti zao pembeni na kuungana dhidi ya chama ambacho kinaongoza, lakini haoni kama Ukawa utaendelea hadi kufikia kipindi cha Uchaguzi Mkuu.
Alisema hatua ya kusimama kwenye ajenda moja ya Katiba haitausaidia umoja huo, kwani kipindi cha uchaguzi mkuu kinakuwa na ajenda nyingi.
Alisema wananchi watapenda kusikia masuala ya kushughulikia rushwa, matumizi ya rasilimali, maji, umeme, afya na barabara.
“Mambo haya ndiyo yatakayowafanya wananchi waamue namna gani watakabidhi dhamana ya uongozi, si suala la Katiba pekee,” alisema Zitto.
Alisema tusijitoe ufahamu kwa kudhani kwamba hii ndio mara ya kwanza kwa upinzani kuungana.
“Kulikuwa na Kamati ya Mabadiliko ya Katiba (KAMAKA) pia katika chaguzi za mwaka 1995, mwaka 2000 wapinzani waliungana vilevile, lakini kila inapokaribia uchaguzi wamekuwa hawaelewani kwa kuwa kila mtu anataka chama chake kipeperushe bendera.
“Lakini kama Ukawa wataweza kuweka ajenda yao mpaka mwisho itakuwa jambo jema kwa wananchi wenyewe. Kwa sababu nchini kwetu tatizo kubwa ni usimamizi na uwajibikaji, kama ajenda itachukua nafasi naamini hali haitakuwa mbaya, lakini bado siamini na sina uhakika kama umoja huu ni endelevu kwa namna ambavyo tunaona, ni umoja ambao unatokana na matakwa ya sasa ya Katiba, wameungana kwa sababu ya serikali tatu, lakini aina gani ya serikali bado hili linaweza kuwagawa,” alisema.
GREDIT; MTANZANIA

Tuesday, July 29, 2014

WAZIRI WA UCHUKUZI DK.HARRISON MWAKYEMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI KATIKA MAKAO MAKUU YA OFISI ZA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA)

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akisaini kitabu cha wageni wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA.Wapili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Mbwana Mbwana.Kulia ni makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya TCAA ,Charles Chacha. Waziri Dk. Harrison Mwakyemba ndiyo waziri pekee aliyetembelea ofisi hizo tangua kuanzishwa.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Ndege wa Mamlaka Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Nuis Kasambala alivyokuwa akimuelezea na kumuonyesha jinsi wanavyofanya mitihani kwa wanafunzi wa ndege wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wanafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA. Waliosimama nyuma ni Kamati ya bodi ya Mamlaka hiyo wakifuatilia kwa makini
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akikabidhiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Charles Chacha moja ya tuzo waliyotunukiwa Tanzania na Baraza la Usafiri wa Anga Duniani kwa kutambua mchango wa TCAA.anayeshuhudia katikati ni Makamu Mweneyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo Weggoro Nyamajeje, wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Mbwana Mbwana akitoa shukrani kwa niaba ya bodi na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, (wapilia kutoka kulia)wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi Weggoro Nyamajeje na Kaimu Mkurugenzi wa TCAA ,Charles Chacha.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo Mbwana Mbwana, wengine ni Makamu Mwenyekiti Weggoro Nyamajeje na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Charles Chacha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, akiuliza swali kwa Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe swali (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA.
Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania TCAA,(kushoto) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Ofisi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongea na wafanyakazi na kuzindua bodi ya Wakurugenzi ya TCAA.

Monday, July 28, 2014

ALI KIBA KUZINDUA NYIMBO MBILI MPYA MWANA NA KIMASOMASO


Mkali wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’
Kiba ambaye ni mkongwe kunako muziki wa Bongo Fleva, amefunguka yeye siku zote ni staa na huwa hakosei hivyo mashabiki watarajie burudani kali siku hiyo.
Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo;
Shoo kali
Katika shoo zake zote huwa habahatishi. Amekuwa ni msanii wa kwanza kutoka Bongo kwa kupiga idadi ya shoo nyingi nje ya nchi kuliko msanii yeyote hata katika matamasha ya ndani ya Bongo amekuwa akiteka hisia nyingi za mashabiki, kwenye Tamasha la Matumaini amesema itakuwa ni zaidi ya burudani.
Ali Kiba’ akipozi.
Kuchomoka kivingine
Baada ya kukaa kimya kwa muda sasa mfalme huyo mwenye sauti ya ajabu, sauti ya kumfanya kila shabiki aikumbuke inapopotea kidogo, amesema anakuja kivingine ambapo atapiga muziki wake kwa mpangilio maalum kuanzia sauti nzuri ya kuwabembeleza.
Habakishi kitu
Kiba amesema siku hiyo hatabakisha kitu, atazipiga nyimbo zote kali kuanzia zile za zamani kama Single Boy, Dushelele, Mac Muga, Run Dunia na nyingine kibao bila kusahau Mwana na Kimasomaso ambazo ndiyo habari ya mjini.
Tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na matukio kibao ya kusisimua kama ngumi za wabunge, mechi za mpira wa miguu za wabunge na wasanii wa Bongo Fleva, Bongo Movie bila kusahau burudani nzuri kutoka kwa wasanii wanaotamba katika muziki wa Injili.
Burudani zote hizo kwa pamoja, mashabiki watazishuhudia kwa mtonyo wa shilingi elfu tano tu huku sehemu ya mapato yatakayopatikana ikipelekwa katika mfuko wa elimu nchini

Sunday, July 27, 2014

HATIMAYE DIMOND ASHINDA TUZO ZA AFRIMMA 2014

Screen Shot 2014-07-27 at 9.43.50 AM 

Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo.
Good news za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja Babu Tale ambae nae kahudhuria tuzo hizi Marekani alienitumia msg kwa kusema wametangaza ukumbini kwamba Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.
Diamond akihojiwa muda mfupi baada ya kushinda tuzo AFRIMMA
Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.01 AM 

Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka ni Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana Dj Oskido wa South Africa, Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Screen Shot 2014-07-27 at 8.17.33 AM
Tuzo zenyewe zimetolewa kwenye hili jengo

Saturday, July 26, 2014

PICHA YA VIDEO MPYA YA NAY WA MITEGO



 
Yupo Kenya sasa hivi ambako ndio ameifanya hii video ya single mpya inaitwa ‘Mr. Nay’ ambayo itatoka wiki ijayo baada ya mzigo kukamilika chini ya mikono ya Director kutoka Kenya.
Nilipomuuliza Nay kuhusu hawa Warembo, minyororo na damu akanijibu ‘ni dizaini ya video ninazozipenda mimi’















Friday, July 25, 2014

RAIS KIKWETE AMWAPISHA LEO SHABAN ALLY KUWA JAJI KIONGOZI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akimuapisha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila leo jijini Dar es Salaam.

Jaji Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Shaban Ally Lila (kulia) akitia saini hati ya Kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kuapishwa kwake leo jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye miwani Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akishuhudia tukio hilo.



 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini hati ya Kiapo cha Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati ya Kiapo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila wakati wa hafla ya kuapishwa kwa jaji huyo leo jijini Dar es Salaam.




Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(kushoto) akimpongeza Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.


 

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahaka Kuu Tanzania mara baada ya kuapishwa rasmi kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.Kushoto kwake ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman Picha zote na Frank Shija- MAELEZO

PINDA AFUNGUA MKUTANO WA BRN PIA AWASILI NAIROBI KUMWAKILISHA KIKWETE MKUTANO WA MAZIWA MAKUU




 

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiongozana na Katibu Mkuu, Kiongozi, Balozi Seif Sefue (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Dr. Omari Issa baada ya kufungua mkutano wa Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu BRN kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Julai 24, 2014.

 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na baadhi ya watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Kenya baada ya kuwasili wenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Julai 23, 2014 kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika mkutano maalum wa nchi za maziwa makuu kuhusu kupambana na tatizo la ajira kwa vijana unaotarajiwa kufanyiaka Julai 24, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DROGBA AREJEA TENA CHELSEA

Screen Shot 2014-07-25 at 9.05.55 PMUtakua uliziona tu zile headlines za mitandao na magazeti mbalimbali duniani kuhusu uwezekano wa staa huyu wa soka Didier Drogba kurejea kuichezea Chelsea baada ya Jose Mourinho kuonyesha nia ya kumrudisha.
Sasa taarifa rasmi iliyothibitishwa na Chelsea, mzaliwa huyu wa Ivory Coast amerejea rasmi kwenye club hii kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo wakati akitia saini, Drogba amesema ‘ulikua ni uamuzi rahisi kabisa wa kuamua kufanya tena kazi na Jose Mourinho, kila mmoja anajua uhusiano wangu na hii club… imekua ni kama nyumbani’
Jose Mourinho mwenyewe amesema ‘amerudi kwa sababu ni mmoja wa wachezaji bora Ulaya, namjua vizuri… na amekuja kuiweka historia nyingine’
Drogba ameifungia Chelsea magoli 157 kwenye mechi 342 alizotokezea.
Ni halali yako kupata kila kinachonifikia mtu wangu na niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza

Wednesday, July 23, 2014

DAVIDO AWACHANA WANAOMSEMA VIBAYA

dadivo 

Msanii staa wa Nigeria Davido ni mtu ambae huwa anaonyesha kwenye mitandao vitu vingi anavyonunua mfano saa za Rolex za dhahabu, magari ya kifahari, nyumba na vitu vingine ambapo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hii ya kupenda kuonyesha mali zake amejibu “sitoweza kusema kama ni kujionyesha kwa mali zangu, yale ni magari yangu, zile pesa zangu na pia ile ni page yangu’
Sio lazima unifollow kwenye instagram wala kunifata kwenye mtandao wowote wa kijamii, ingekuwa tofauti sana kama nataka kujitangazia mali zangu basi ningetumia mabango ya barabarani lakini sifanyi hivyo.
wwwwwwwwwwwwwww 
Unadhani ni sahihi kwa mastaa kuonyesha mali zao na pesa kama hivi kwenye mitandao ya kijamii? niachie comment yako hapa chini mtu wangu