Thursday, July 31, 2014

DIMOND APOKELEWA AIRPORT KWA SHANGWE NI SHIDAAAA!!!!

30dmnd 

Ni mamia ya wakazi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioamua kwenda kumpokea Diamond Platnumz baada ya safari yake ya kutoka Marekani ambayo imekua njema kwa Tanzania baada ya kurudi na tuzo.
Mapokezi yalianzia  uwanja wa Julius Nyerere International Airpot kisha msafara ukaelekea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ukipitia Buguruni,Kariakoo na baadae kumalizia nyumbani kwake Sinza.
Wakati akiwa kwenye gari ya wazi Diamond Platnumz muda wote alikua kaishikilia tuzo yake aliyoipata Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA ambapo kwa upande wake ameibuka na ushindi wa tuzo ya Msanii bora wa Afrika Mashariki.
Ratiba ya Diamond kuingia Tanzania ilikua iwe jioni ya Jana July 29 lakini kutokana na sababu walizosema zilizokuwa nje ya uwezo wao safari yao ikasogezwa mpaka leo July 30 na alifanikiwa kuingia saa 1 asubuhi.
Ingawa hali ya hewa ilikua imetawaliwa na manyunyu pamoja mvua ndogo ndogo,Hizi ni baadhi ya picha za mashabiki waliojitokeza kumpokea Diamond.








GREDIT MILLARD AYO

No comments:

Post a Comment