Wenyeji wa kombe la dunia Brazil
walitoka nyuma na kuilaza Croatia mabao 3-1 katika mechi ya kufungua
fainali ya dimba la mwaka huu iliyochezwa katika uwanja wa Sao Paolo
(Arena de Sao Paulo).
Mechi hiyo ilikuwa ikitizamwa na mashabiki
65,000 uwanjani humo baada ya kushuhudia tafrija ya ufunguzi
iliyotizamwa na watazamaji zaidi ya bilioni moja kupitia kwa runinga
Wenyeji Brazil walitazamiwa kufunga
bao la kwanza mapema katika mechi hiyo lakini uwanjani mambo yalikuwa
tofauti ,Marcelo alijifunga mwenyewe na kuiweka Croatia mbele baada ya
dakika 11 pekee ya kipindi cha kwanza .
Wenyeji waliotamaushwa na bao hilo walikuwa na
matumaini kuwa kiungo machachari anayechezea Barcelona ya Uhispania
Neymar atawaongoza ''the samba boys'' kutwaa taji lao la sita la dunia
nyumbani.
Na nyota huyo hakuboronga alitumia kila mbinu
ikiwemo kumbo iliyompelekea kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya
njano na refarii kutoka Japan Yuichi Nishimura.
Hata hivyo dakika chache tu baada ya kuonyeshwa
kadi hiyo ya njano Neyma alijifurukuta na kuisawazishia Brazil katika
dakika ya 29 ya kipindi cha kwanza.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 22
aliiweka Brazil Mbele zikiwa zimesalia dakika 19 mechi hiyo kukamilika
baada ya refarii kutoka Japan
Nishimura kupiga kipenga na kuashiria penalti baada ya Dejan Lovren kuonekana kama aliyemtega Fred katika eneo la lango.
hata hivyo picha za runinga zilizorejelea mara kadhaa hazikuonesha kama Lovren alimgusa Fred.
Wachezaji wa Croatia walijaribu kumshawishi
mjapan huyo kuwa haikuwa kweli fred alikuwa amejiangusha lakini maoni
yao hayakusikika
No comments:
Post a Comment