Sunday, May 11, 2014

POMBE YENYE SIMU YAUA WATU ZAIDI YA 70 NCHINI KENYA SOMA HAPA


Washukiwa waliouza pombe hiyo wameripotiwa kukamatwa
Watu wawili wamekamatwa nchini Kenya kuhusiana na mkasa wa watu 70 kufariki kutokana na kunywa pombe iliyokuwa imetiwa sumu. Vifo hivyo vimetokea katika muda wa saa 48 baada ya walevi kuanza kulewa siku ya Jumapili na Jumatatu asubuhi.
Pombe hiyo iliyopewa jina la 'Countryman', inasemekana iliwekwa sumu aina ya Methanol na kusababisha baadhi ya waliokuwa wamekwenda kuibugia kufariki huku wengine wakisalia hali mahututi na wengine kupoteza uwezo wao wa kuona.

No comments:

Post a Comment