Sunday, April 20, 2014

UKAWA"HATUJAMPIGIA MAGOTI ZITTO KABWE" NA UMOJA HUU UNASHIMU MAAMUZI YA KILA MTU




Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.
Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi kuombwa ashiriki ktk shughuli za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.
Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z Kabwe akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa taifa na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"

Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana baadhi ya wajumbe kama ISACK CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni lakini keshoye walirejea na kuendelea na bunge.
Umoja huu unaheshimu haki wajibu na maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda mamlaka na maoni ya wananchi.
Tutafanya kazi na mtu yeyote ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile ambacho tunakiamini.
J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar

No comments:

Post a Comment