Yanga ya Tanzania. |
Al-Ahly ya Misri. |
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Mabingwa barani
Afrika, Young Africans, maarufu kama "Yanga" leo hii wanakabiliana na
mabingwa watetezi wa kombe hilo, Al-Ahly ya Misri katika mchezo
utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kuingia katika hatua ya raundi ya kwanza ya michuano hii, Yanga
waliitupa nje timu ya Comorro, Komorozine kwa kuichabanga jumla ya
magoli 12-2. Katika mchezo wa kwanza na Komorozine, uliofanyika jijini
Dar es Saalm,Yanga iliitwisha mzigo wa magoli 7-0 na kuiadhibu tena
nyumbani kwao Comorro mabao 5-2, hivyo kujikuta katika raudni ya kwanza
ikipangiwa kukutana na al-Ahly.
Yanga imekuwa na msukumo mkubwa wa kupata ushindi baada ya mwenendo wake
wa kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa na ligi kuu ya nyumbani.
Katika mapambano yaliyopita kati ya Yanga na Al-Ahly, daima timu hiyo ya
Misri imekuwa ikiibuka mbabe kwa kuifunga na kuitoa Yanga katika
mashindano kama hayo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, mthalani mwaka
2009, katika hatua kama hii Yanga ilichapwa na al-ahly mabao 4-0 na
kutolewa nje.
Hata hivyo, safari hii, Yanga imeonekana kupania kusonga mbele katika
michuano hiyo ya Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, kwani imefanya
maandalizi makubwa ikiwemo kupiga kambi ya wiki mbili nchini Uturuki,
barani Ulaya na kuendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya nyumbani.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijn anajivunia kikosi chake na
kutamba kwamba safari hii, al-Ahly hawatatoka salama katika Uwanja wa
Taifa, akijigamba kwamba atawafunga kwani anazifahamu vizuri mbinu za
timu hiyo.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo za mabingwa wa kombe la Afrika ni Gor
Mahia ya Kenya watakuwa wenyeji wa EST ya Tunisia, Kampala City Council
ya Uganda itasafiri kwenda Zambia kumenyana na Nkana Red Devil.
No comments:
Post a Comment