Thursday, March 13, 2014

YAMETIMIA MH SAMWELI SITA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI BUNGE LAKATIBA

  Mh. Samweli Sitta mbali na kuwashukuru wale wote waliomsaidia kushinda uchaguzi wa kugombea kiti cha kuwa Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, aliweza pia kumshukuru sana Mungu pamoja na wachungaji waliomsaidia katika kumuombea na Mungu akasikia maombi yao na hatimaye kushinda. Alisem,kumtegemea Mungu kunafaida kwahiyo Mungu ndiye muweza wa yote.

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta ameshinda nafasi hiyo kwa kura 487 dhidi ya mpinzani wake, Mhe. Hashim Rungwe aliyepaya kura 69 kati ya kura 593 zilizopigwa, na saba kuharibika katika uchaguzi uliofanyika muda mfupi uliopita Bungeni mjini Dodoma. Akitoa Neno la Shukrani mara baada ya kupata nafasi hiyo,Mh. Sitta amewashurukuru Wajumbe wote wa Bunge la Katiba kwa kuweza kumpa nafasi hiyo adhimu. Pia amempongeza mpinzani wake,Mh. Hashim Rungwe kwa kukubali matokeo hayo.

Wajumbe wakipiga kura

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimpongeza Mhe. Sitta kwa ushindi wake wa kishindo

Mikono ya pongezi yazidi kumiminika.

Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba mteule Mhe Samwel John Sitta akitoa neno la shukurani kwa Wajumbe kwa imani waliyoonesha kwake kwa kumchagua kwa kura nyingi kushika nafasi hiyo.

Aliekuwa Mgombea Mwenza wa Nafasi ya Uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Hashim Rungwe akizungumza machache mara baada ya kukubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika Bungeni hapo uliompa Ushindi wa Nafasi ya Uenyekiti,Mh. Samuel Sitta kwa kura 487.

Mh. Hashim Rungwe akiendelea kuzungumza.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakibadilishana mawazo.

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Edward Lowassa na Mh. Anne Tibaijuka wakibadilishana mawazo wakati Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge hilo ukiendelea.

Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta akiteta jambo na Mjumbe wa Bunge hilo,Mh. Paul Makonda.

Mwenyekiti Mteule wa Bunge Maalum la Katiba,Mh. Samuel Sitta akipongezwa na Wajumbe mbali mbali wa Bunge hilo.



No comments:

Post a Comment