
Katibu Mkuu Taifa wa Muda wa Chama cha Alliance For Change And Transparency (ACT) Samson Mwigamba (ambaye alivuliwa uanachama wa CHADEMA) akizungumza na waandishi wa habari kulaani juu ya vurugu zilizofanywa na wafuasi wa CHADEMA wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Chama hicho Jijini Mwanza kwenye viwanja vya Mbugani .

Ameongeza kuwa ACT Tanzania kimekuja na dhamira ya dhati ikiwa imejengwa na mfumo wa ukweli na uwazi tangu kuanzishwa kwake na jinsi kitakavyoongozwa misingi yake na malengo yake vyote vimelenga kumkomboa mtanzania mnyonge.
"Vyama vingine vyote vinaitikadi inayojali nguvu ya soko, na sisi (ACT) tunasema mtanzania ambaye amekosa elimu asiye na mtaji huwezi kumsukuma kwenye soko huria akaenda kushindana na wafanyabiashara wenye mitaji, hivyo ACT haitaliruhusu hilo liendelee na badala yake tutaleta usawa katika jamii na kumwezesha mwananchi kujiendeleza kiuchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo " alisema Mwigamba.

Mwenyekiti Taifa wa ACT Kadawi Limbu akitoa ufafanuzi kwa wanahabari juu ya Chama chake kupeleka malalamiko yake kwa Msajili wa vyama vya Siasa nchini kukichukulia vyama vinavyofanya vitendo vya vurugu kwenye mikutano ya vyama vingine kwa kutumia wafuasi wao kama ilivyojitokeza Jijini Mwanza hivi karibuni kwa wafuasi wa CHADEMA kufanya fujo ka kuwashambulia Makada wa ACT waliokihama chama cha CHADEMA na kujiunga ACT kwenye mkutano wa hadhara.

Bendera ya ACT Tanzania.

Mweyekiti Limbu akiendeleea kutoa msisitizo kuhusu dhamira ya chama hicho kipya. Kulia ni Pendo Ojijo (mmoja kati ya wanachama wa ACT)

Kusanyiko la Viongozi, wanachama na wanahabari katika ukumbi wa hotel ya JB Belmonte jijni Mwanza.
No comments:
Post a Comment