Tuesday, March 11, 2014

VODACOM KUWEKEZA ZAIDI KATIKA KUMKOMBOA MWANAMKE

 

Baadhi ya Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone, Jacqueline Barrett, katika hafla iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa wanawake wa Kampuni hiyo ikiwa ni katika Shamra Shamra za kuelekea siku ya Wanawake duniani. Kampuni hiyo imeahidi kuendelea kuunga mkono harakati za kumkomboa mwanamke.





Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone, Jacqueline Barrett, akicheza ngoma, wakati wa Hafla iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo, Hafla hiyo ilifanyika Makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo imeahidi kuendeleza kuunga mkono harakati za kumkomboa mwanamke.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone, Jacqueline Barrett, akizungumza na wanawake wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, katika hafla iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwa wanawake wa Kampuni hiyo ikiwa ni katika Shamra Shamra za kuelekea katika kuazimisha siku ya Wanawake duniani. Kampuni hiyo imeahidi kuendeleza kuunga mkono harakati za kumkomboa mwanamke.

Vodacom kuwekeza zaidi katika kumkomboa Mwanamke
Dar es Salaam 7 Machi 2014 . . . . . Ikiwa ni siku moja tu tangu mke wa Mama Salma Kikwete kuzindua mpango wa “Connected Wommen” wenye lengo la kutambua mchango wa teknolojia ya simu za mkononi katika kubadili maisha ya Mwanamke nchini, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom, Imeahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za kumkomboa Mwanamke nchini.
Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na wafanyakai wanawake wa Kampuni hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam. Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Vodafone Group. Bi Jacqueline Barrett, amesema kuwa Vodafone imejidhatiti katika kumkomboa Mwanamke na kuweka usawa katika jamii ya Watanzania huku akiwasihi wanawake walioajiliwa na kampuni hiyo kuwa chachu ya mabadiliko.
“Vodafone Foundation imekuwa na Mipango mbalimbali katika kuwakomboa wanawake ikiwa ni pamoja na mpango wa kutumia njia ya simu katika kuwatafuta na kutoa huduma kwa wanawake wenye Fistula mpango ambao umewezesha zaidi ya Wanawake elfu 3000 kupata huduma ya Matibabu kutoka Hospitali ya CCBRT” Alisema Bi Barrett na kuongeza.
“Ukiacha Mradi huo wa Fistula, Nimeona Vodacom Tanzania wamewezesha Mradi wa Mwei ambao unatoa mikopo midogo isiyo kuwa na Riba kwa wanawake wajasiriamali wadogo ambao hawakopesheki katika taasisi za mikopo” Mradi huu umeleta mabadiliko ya kiuchumi kwa zaidi ya akina mama . . . . . Tanzania bara na Visiwani.
Kampuni hiyo pia imekuwa ikitekeleza ushirikiano na Taasisis isiyo ya Kiserekali ya T – Marc Tanzania ambapo imekuwa ikitoa elimu pamoja na taulo za kujisitili kwa watoto wa kike wasio na uwezo wa kununua taulo hizo katika mikoa ya lindi na mtwara.
Katika Hatua nyingine Mtendaji huyo aliwasihi wafanyakazi wa kampuni hiyo pamoja na wadau wa masuala ya teknolojia kutumia vyema teknolojia ya Mawasiliano na simu katika kubadili maisha ya wanawake.
Awali akizungumza baada ya kuzindua Mpango wa “Connected Women” mama Salma Kikwete alisema kuwa, Teknolojia ya simu ikitumiwa vyema inaweza kumkomboa mwanamke huku akitoa wito kwa jamii kuuangalia kwa uwanja mpana mchango wa Mwanamke ndani ya jamii kwani siku zote wanawake wamekuwa wakitekeleza majukumu makubwa ndani ya jamii lakini mchango wao hautambuliki ipasavyo.
“Ni kweli kuwa Mara nyingi mchango wa wanawake katika jamii umekuwa hautambuliki vya kutosha, hata hivyo ndani ya akili zao au kwa sauti ya chini au kimya kimya watu wengi wanatambua kwamba mwanamke ni uti wa mgongo wa kila familia,” alisisitiza Mama Salma kwa kusema “Mama ni Malkia, Thamani yake haina kifani.
Mamam Salma alihitimisha kwa kusema “Wakati Umefika sasa tutoe sauti zetu huko nje tena kwa Mwangwi mkubwa kuzungumzia uwezeshaji wa Mwanamke ambao kwa mila na desturi nyingi walitarajiwa kutekeleza majukumu ya nyumbani pekee,”
Katika shamra shamra za siku ya Wanawake duniani kampuni ya Simu za Mkonoi ya Vodacom Tanzania ilianza kutekeleza mpango wa Connected women ambao unatoa fursa za kiteknolojia katika kumkomboa Mwanamke w Kitanzania huku mafanikio mbalimbali yakitajwa kupatikana ikiwemo mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Fistula.

No comments:

Post a Comment