Maafisa wa Marekani wamesema
kuwa Waziri wa mambo ya nje John Kerry, amekataa kukutana na Rais wa
Urusi, Vladmir Putin, mpaka pale Moscow itakaporidhia mapendekezo ya
Marekani kuhusu kumaliza mzozo nchini Ukraine.
Kerry amemwambia waziri wa mambo ya nje wa Urusi
kuwa uvamizi wa kijeshi wa Urusi mjini Crimea umefanya mazungumzo ya
kufikia muafaka kuwa magumu mno.Maafisa wa Marekani wamesema ikiwa kura ya maoni iliyopendekezwa itapigwa mwishoni mwa juma kuhusu kuridhia kwa Crimea kuwa sehemu ya Urusi, hakuta kuwa na suala jingine la kuzungumza.
Maafisa hao wamesema kuwa ikiwa hali itafikia hivyo, Marekani itaiwekea Urusi vikwazo vikali.
chanzo bbc
No comments:
Post a Comment