Monday, March 31, 2014

SHIRIKISHO LA FILAMU TANZANIA "HATUITAMBUI BONGO MOVIE UNITY YA STEVE NYERERE"

 
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amedai shirikisho lake haliwatambui wasanii wanaounda kundi la Bongo Movie Unity na kudai kuwa kundi hilo linaundwa na watu sita tu huku wengine wakifuata mkumbo.

Akizungumza na Global Publishers, Mwakifwamba ambaye pia ni muigizaji wa muda mrefu na muongozaji wa filamu amesema hawatambui wasanii hao na anawashauri wajiunge ili watambulike. “Bifu la nini? Mimi ni baba, wao ni watoto. Kwanza sikia… wale sio wanachama wangu.Nawashauri wajiunge kwenye vyama vyangu ili niwatambue kama sehemu ya shirikisho,” alisema.

“Unajua wale wanaongozwa na ustaa. Wanaamini ustaa upo juu ya sheria, sio kweli. Mimi naamini katika uelewa na uwezo.Isitoshe mtu wa kwanza aliyetoa wazo la Bongo Muvi ni mimi. Nakumbuka nilikuwa mimi, Dude (Kulwa Kikumba), William na Ruge Mutahaba, tukaunda Bongo Muvi ili tucheze mechi na Bongo Fleva kwa ajili ya kuchangisha fedha za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto. Tulifanikiwa sana. Hapo sasa walafi wachache wakalazimisha wasanii waende Mwanza wakacheze mechi nyingine ili wapate fedha, nikakataa hilo wazo, ndiyo mwanzo wa kutengana nao. Niwaambie tu Watanzania, chombo mama cha wasanii wa filamu nchini ni TAFF, si vinginevyo,” aliongeza.
“Kwanza Bongo Muvi si chama kama wengi wanavyofikiri, ni kampuni na ina wamiliki wake tisa, hao wengine wanafuata mkumbo kwa sababu hawajitambui. Kama wanabisha, waonyeshe usajili wao wa Basata, maana chombo pekee kinachosajili kazi za wasanii ni Basata.”
Hata hivyo Bongo5 imejaribu kumtafuta mwenyekiti wa BMU, Steve Nyerere kuzungumzia kauli hiyo, lakini amekuwa hapokei simu.

Credit:GPL.

No comments:

Post a Comment