Monday, June 1, 2015

DIAMOND AANZA KUUZA KAZI ZAKE KWEA NJIA NYINGINE



Nyota wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia kama vile Mziiki iliyozinduliwa hivi karibuni ili ziweze kuwafikia watu wengi na kwa wakati huohuo wanamuziki pia kunufaika na

jasho lao.
“Duniani kwa sasa hivi kuna ushindani mkali katika nyanja zote. Sisi kama wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki wa viwango vya juu na kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ndani na ya nje kama wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia ya kisasa na kumnufaisha msanii kama ilivyo program hii ya Mziiki. Kuna umuhimu mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa” anasema Diamond Platinumz
Aliwaomba wapenzi wa muziki nchini kuwaunga mkono wanamuziki wa hapa nchini kwa kupakua nyimbo zao kwenye Mziiki kwa kuwa njia hii iko wazi na inamuwezesha mwanamuziki kujua kirahisi jinsi kazi zake zinavyokubalika sokoni na inamuwezesha kujua mapato yake tofauti na njia nyingine kama uuzaji wa CD kwenye maduka na mitaani.

Programu ya Mziiki ambayo ilizinduliwa na Vodacom kwa kushirikiana na Spice VAS Africa imeanza kufanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini na nje ya nchi na katika kipindi cha muda mfupi tayari imesajili wanamuziki wapatao 1,000 ambao kazi zao hususani zile mpya zitasambazwa kwa njia ya kidigitali na malengo yake makubwa ni kuhakikisha wanamuziki wanapeleka kazi zao sokoni kwa haraka na kunufaika na jasho lao hususan pale ambapo wananchi wengi watatumia mtandao kwenye simu zao kupakua nyimbo wazipendazo za wanamuziki ambao wamejiunga kwenye tovuti ya kampuni hiyo ambayo inapatikana kwa kubofya tovuti ya 
www.mziiki.com.

No comments:

Post a Comment