Saturday, March 7, 2015

MBUNGE WA KINONDONI AFIWA NA KAKA’KE, AZIKWA!


Mbunge wa Kinondoni (aliyesiamama kushoto), Idd Azzan akiwa nyumbani kwa marehemu.

Waombolezaji wakiwa msibani nyumbani kwa marehemu.
Wakina mama wakiwa msibani hapo.

MBUNGE wa Kinondoni, Mh. Idd Azzan amepata pigo kwa kufiwa na kaka yake, Azzan Mohamed usiku wa kuamkia leo aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la ini.Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwa kaka yake Magomeni-Somanga, jijini Dar, mbunge huyo alisema kifo cha kaka yake huyo ni pigo kubwa kwani alikuwa na msaada mkubwa kwake na kwa ndugu zake.
Alisema marehemu alisumbuliwa na tatizo la ini kwa takriban miaka miwili iliyopita ambapo katika kipindi chote hicho walijaribu kumpeleka katika hospitali mbalimbali jijini Dar kupatiwa matibabu lakini hali ilikuwa ikibadilikabadilika siku hadi siku.
Azzan aliongeza kuwa, marehemu kaka yake ndiye alikuwa kijana mkubwa katika familia na hata marehemu baba yao alipofariki, yeye ndiye aliyekuwa tegemeo kama kiongozi lakini naye Mungu amemchukua.
“Kifo cha marehemu kaka yangu kimeniuma sana maana kaka yetu baada ya kifo cha marehemu baba yetu ndiye aliyehakikisha tunapata haki zote za msingi katika familia,’’ alisema Azzan.Azzan Mohamed alifariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni na amezikwa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar.Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, amina. (PICHA/HABARI: DENIS MTIMA/GPL)

No comments:

Post a Comment