Monday, January 26, 2015

BALOTELI AELEZEA SABAUBU ZA KUACAHANA NA MPENZI WAKE

mario fany 6

Mrembo ambaye alikuwa mpenzi wa Star wa klabu ya Liverpool Fanny Neguisha amefichua chanzo cha kuachana na mchezaji huyo baada ya kimya cha muda mrefu .
Baloteli na Fanny walionekana kuwa pamoja kwa muda mrefu kabla ya kuachana baada ya muda huku kukiwa hakuna sababu iliyowahi kutajwa na yoyote kati ya wapenzi hao wa zamani ya kuachana kwao .
Balotelli alifikia hatua ya kumchumbia binti huyo raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Ethiopia akimvisha pete ya thamani ya paundi elfu 25,000 wakati wakiwa nchini Brazil .
Baloteli na Fanny wakati uhusiano wao ulipokuwa unaendelea .
Mwanadada huyo amefichua kuwa chanzo cha wawili hao kuachana na kitendo cha Mario Baloteli kumlazimisha aachane na fani yake ya uanamitindo pamoja na muziki .
Fanny amefichua kuwa Balotelli alikuwa hapendezewi na picha za mitindo ambazo alikuwa akipiga , kimsingi hakuwa anakubaliana na kazi yake hali iliyofanya arudishe pete yake ya uchumba na kusitisha mipango yao ya kuoana.

Baloteli hakutaka Mpenzi wake Fanny Neguisha ajihusishe na kazi ya urembo na mitindo pamoja na muziki .

Baloteli hakutaka Mpenzi wake Fanny Neguisha ajihusishe na kazi ya urembo na mitindo pamoja na muziki .
Fanny alisema hayo kwenye mahojiano ya tele
visheni ambapo alisema kuwa Baloteli alimlazimisha aachane na mitindo , ambapo mrembo huyo alisisitiza kuwa anaipenda kazi yake na ana haki ya kuwa na maisha ya kazi kama ilivyo kwake (Balotelli) jambo ambalo Mario hakukubaliana nalo

No comments:

Post a Comment