Saturday, December 27, 2014

MKE WA RAIS WA ZAMANI WA IVORY COAST ASHITAKIWA BI SIMONE GBAGBO


Mke wa aliyekuwa rais wa Ivory Coast laurent Gbagbo,bi Simone Gbagbo amefunguliwa mashtaka ya ghasia za baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast
Mke wa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo, Simone Gbagbo amefikishwa mahakamani kutokana na mashtaka ya kuhusika kwenye ghasia za baada ya uchaguzi ambapo zaidi ya watu 300 waliuwa.
Bi Gbagbo na watu wengine 82 akiwemo waziri mkuu wa zamani wameshtakiwa kwa kuhujumu usalama wa nchi, ukabila na kwa kubuni makundi ya uhalifu.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo ambaye alikataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu miaka minne iliyopita anasubiri kesi yake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kutokana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Zaidi ya watu 3000 waliuawa katika ghasia hizo baada ya rais huyo wa zamani kukataa kushindwa katika ya kura ya awamu ya pili.
Bi Gbagbo ambaye alikuwa anazuiliwa katika kifungo cha nyumbani kwa miaka mitatu ameshtakiwa kwa jaribio la kuhujumu usalama wa taifa hilo.
Aliyekuwa waziri mkuu Gilbert Ake N'Gbo na kiongozi wa chama cha FPI Affi N'Guessan pia wamefunguliwa mashtaka na bi Gbagbo.

No comments:

Post a Comment