Saturday, December 27, 2014

MAN UNITED CHELSEAL, ARSENAL MAN CITY ZAZID KUNG"ARA KWENYE EPL



Olivier Giroud alipewa kadi nyekundi katika ushindi wa arsenal dhidi ya QPR
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa Olivier Giroud alihitaji kupewa kadi nyekundu katika mechi dhidi ya QPR,lakini akathibitisha kuwa mshambuliaji huyo ameomba msamaha baada ya kisa hicho.
Giroud mwenye miaka 28 alionekana akimpiga kichwa Nedum Onuoha katika kipindi cha pili cha ushindi wa 2-1.
Wakati huohuo mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa beki John Terry anacheza kama wakati alivyoiongoza the blues kushinda ligi ya Uingereza miaka kumi iliopita.
Ana motisha chungu nzima. John Terry alifunga bao la kwanza la Chelsea

''Sioni tofauti ya John wa miaka ya 2004,05,06 sioni tofauti yoyote'',alisema Mourinho.
Terry alifunga katika ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham na kuifanya timu hiyo kusalia kileleni mwa ligi hiyo.

Kwengineko mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa ametosheka na uongozi unaotolewa na nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney ambaye alicheza katika safu ya kati na kuisadia timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle katika uwanja wa Old Trafford. Rooney aliifungia Manchester United mabao mawili katika ushindi wa mabo 3-1 dhidi ya Newcastle

Rooney alifunga mabao mawili na kutoa usaidia wa bao la tatu kwa Robin Van Persie.
Nayo Manchester City ilifunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza dhidi ya West Bromwich licha ya barafu iliokuwa ikianguka katika uwanja huo na kusalia nyuma ya Chelsea kwa alama tatu.
Fernando aliifungia City bao la kwanza,baada ya Ben Foster kutoa kross nzuri kutoka kwa Jesus Navas. Yaya Toure alicheka na wavu wa Westbromwich alipopiga mkwaju wa Penalti

Yaya Toure alifunga bao la pili kupitia mkwaju wa Penalty kabla ya David Silva kufunga bao la tatu.

West Brom 1 - 3 Man City West Bromwich walifunga bao la kufutia machozi wakati wa kipindi cha pili.

No comments:

Post a Comment