Monday, November 24, 2014

VIONGOZI WA SUDANI YA KUSINI WAMFUATA KINANA MASASI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye shati la kijani) pamoja na viongozi wa chama cha SPLM kutoka Sudani Kusini wakiwa wameinua mikono juu kama ishara ya umoja na mshikamano,Masasi mkoani Mtwara.
Kutoka Kushoto ni Dkt. Cirino Hiteng,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Bw.Goy Jooyul na Jenerali James Kok.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mazungumzo na viongozi wa chama cha SPLM kutoka Sudani ya kusini waliomfuata Masasi mkoani Mtwara ambapo Katibu Mkuu wa CCM yupo kwenye ziara ya kukijenga na kukiimarisha chama mkoani Mtwara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza  Jenerali James Kok kutoka chama cha SPLM Sudani ya Kusini ambaye yeye pamoja na viongozi wenzake wamefika mpaka Masasi kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM.

No comments:

Post a Comment