Aliyekuwa mmiliki wa timu ya
mpira wa vikapu LA Clippers, ambaye amezongwa na balaa za kisheria,
Donald Sterling, amekubali kuiuza klabu hiyo.
Bwana Sterling ameiuza klabu hiyo kwa aliyekuwa mkuu wa kampuni ya Microsoft Steve Ballmer, kwa dola bilioni 2.
Bwana Sterling amekuwa akikabiliwa na shutuma za ubaguzi wa rangi.
Ametangaza pia kuwa ataondoa kesi aliyowakilisha
dhidi ya shirikisho la mpira wa vikapu nchini Marekani NBA, ya kudai
ridhaa ya dola bilioni moja akisema kuwa shirikisho hilo limekiuka haki
zake za kikatiba.
Shirikisho hilo la NBA limemuwekea marufuku ya
maisha bwana Sterling kutohudhuria mechi zozote za mchezo huo, kufuatia
kanda zilizotolewa akimtusi aliyekuwa mpenzi wake kwa matamshi ya
kibaguzi wa rangi.
Pia bwana Sterlig amepewa hakikisho kuwa NBA
haitamfungulia mashtaka yoyote. Sasa kinachosubiriwa ni asili mia 75
kati ya wamiliki washirikishi 29 waliosalia wa klabu hiyo kuidhinisha
uuzaji huo
No comments:
Post a Comment