Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, mkoani Mwanza (Chadema), Salvatory Machemli, ameibwaga serikali baada ya Mahakama kumwachia huru katika kesi ya uchochezi iliyokuwa ikimkabili.
Machemli aliachiwa huru jana na Mahakama ya Wilaya mjini hapa baada ya upande wa mashitaka kukosa ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha shitaka dhidi yake.
Mbunge huyo aliachiwa huru na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe iliyokuwa imefurika umati wa watu, Faustine Kishenyi, baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri na utetezi.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kishenyi alisema kuwa Mahakama imeridhika kuwa mshtakiwa hana hatia baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha shitaka dhidi yake.
Hakimu Kishenyi alisema katika uamuzi wake kuwa mbali ya Jeshi la Polisi kushindwa kuwasilisha vielelezo mahakamani kama ilivyo katika hati ya mashitaka, pia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka haukuwa na hoja wala haujitoshelezi kumtia hatiani mshtakiwa.
Akifafanua, Hakimu Kishenyi alisema kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuwasilisha CD iliyochukuliwa wakati mshtakiwa akitenda kosa huku askari polisi watatu pekee wakijitokeza kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa Hakimu Kishenyi alisema hakuna mtu aliyekwenda kutoa ushahidi kutoka nje ya Jeshi la Polisi kuthibitisha kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la uchochezi.
Hakimu huyo alisema kutokana na waliotoa ushahidi kutoka Jeshi la Polisi pekee wakati nalo linahusika katika kesi hiyo, inaonyesha kuwa kulikuwapo na maslahi ya upande mmoja, hivyo ushahidi huo hauwezi kutumika kumtia hatiani mshtakiwa Machemli.
Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samuel Onyango, kuwa Machemli (39), alitenda kosa la uchochezi Oktoba 23, mwaka 2011 wakati anahutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyamanga kilichopo katika kisiwani Ukara, mashitaka ambayo hata hivyo, mshtakiwa aliyakanusha.
Katika kesi hiyo, ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo kwa makusudi aliwachochea wananchi wazuie shughuli za Jeshi la Polisi na hata kuwashambulia askari watakapokwenda katika maeneo yao kuwasaka wahalifu.
Hata hivyo, Hakimu Kishenyi alisema kwamba upande wa mashitaka unaweza kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia jana.
Source: Nipashe 6/6/2014

No comments:
Post a Comment