Washukiwa wa kundi la wapiganaji
wa kiisilamu nchini Nigeria, Boko Haram, wamewateka nyara wasichana
wengine 8 Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Tukio hili la hivi karibuni la utekaji nyara, lilifanyika Jumapili, katika kijiji cha Warabe katika jimbo la Borno .Mnamo siku ya Jumatatu, kiongozi wa kundi hilo alitishia kuwauza wanafunzi 230 waliotekwa nyara na kundi hilo katika shule ya Chibok tarehe 14 mwezi Aprili.
Kundi la Boko Haram limewaua maelfu tangu mwaka 2009. Lengo lake kuu ni kupinga elimu ya kimagharibi na kutaka utawala wa kiisilamu.
Kwa mujibu wa mhariri wa idhaa ya Hausa Mansur Liman, eneo la Warabe ambako wasichana wanane walitekwa nyara, ni ngome ya kundi hilo la kiisilamu.
Wapiganaji waliwasili katika lori mbili huku wakiiba chakula na mifugo kutoka katika kijiji hicho.
Waandamanaji wamekuwa wakifanya maandamano kuishinikiza serikali kuharakisha juhudi zake za kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara tarehe 14 Aprili.
Kijiji hicho pia kiko akribu na msitu Sambisa ambako kikundi cha kwanza cha wanafunzi waliotekwa nyara walipelekwa.
Kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, alitoa kanda ya video siku ya Jumatatu kudai kuwa kundi hil ndilo liliwateka nyara wanafunzi hao na kwamba linapanga kuwauza.
No comments:
Post a Comment