Ikiwa ni miezi miwili imepita tangu huduma ya Mtume Lesego Daniel wa
nchini Afrika Kusini ya Rabboni Ministries Centre kuwa maarufu duniani
baada ya waumini wake kula nyasi kama moja ya namna ambavyo roho
mtakatifu alivyowaongoza, sasa waumini hao wamegeukia majani.
Imefahamika kuwa wamekuwa wakitumia njia hiyo kupata uponyaji licha ya watu wengi kupinga ufunuo wa namna hiyo.
Kupitia picha zilizotolewa na huduma hiyo kupitia ukurasa wake wa
facebook, zimeonesha waumini wakikimbilia matawi ya miti na kuanza kula
majani yake, huku mmoja wao aliyefika kanisani hapo kwa mara ya kwawnza
akidai kupona jino lililokuwa likimuuma.
Baadhi ya waumini wakiwa wamezimia baada ya kula majani.
Muumini huyo alisema kwamba alifika kanisani hapo kwa mara ya kwanza
Ijumaa ya wiki iliyopita akiwa na dawa za kutuliza maumivu ambazo
zilikuwa hazimsadii lakini alipokula tu majani yalimponya na kwamba
akirudi nyumbani, mumewe (ambaye pia ni mtumishi) atafurahi sana kwa
uponyaji huo.
Huduma hiyo imekuwa ikipingwa na watu wengi hasa baada ya tukio la
waumini kula nyasi huku pia mtume huyo muda mwingine huwafanyia maombi
waumini wake akiwa amewakanyaga migongoni.
Licha ya kelele kutoka kwa viongozi wa dini na makanisa mbalimbali
kuwakataza waumini wao na wakristo kuwa makini na huduma ya mtumishi
huyo, ndiyo kama wamewaruhusu kwenda huko kwa kuwa inasemekana watu
wamepagawa na baadhi yao huzimia wakati wa kupata maombi hayo katika
huduma hiyo inayoendelea kujikusanyia waumini kila kukicha.
Huduma hiyo ilikuwa ikifanyika katika majengo ya Chuo Kikuu cha
Teknolojia cha Tshwane kwa sasa wamepata eneo lao ambalo wameliita
shamba la Rabboni ambalo wanatarajia kuhamia huko kesho Jumapili.
No comments:
Post a Comment