MH; JOSHUA NASARI
Ikiwa ni miaka miwili tangu achaguliwe kuwa mbunge kijana kabisa wa jimbo la Arumeru mashariki, mbunge huyu amefanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa 80% kitu kinachowafanya CCM wasiwe na uhakika hata wa kupata kata moja jimbo la Arumeru kwani wananchi wanajiuliza kama kijana akiwa peke yake kwenye halmashauri na ameweza yote haya je siku madiwani wakiwa wa chama chake itakuwaje?
wanaarumeru kwasasa wanajivunia kuwa na mbunge makini kutoka chama makini (Joshua Nassari)
Mashamba aliyoyarudisha kwenye milki ya wananchi ni shamba la Madira lenye ukubwa wa ekari 210, ambalo amelipangia miradi ifuatayo; shule ya sekondari, shule ya msingi, makazi,michezo, shopping mall na stand ya mkoa hii pia kupunguza foleni mjini Arusha. Kwa ujumla mradi huu utaongeza mapato halmashauri ya Meru na pia utatengeneza ajira kwa vijana wengi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Ikumbukwe kuwa eneo la Madira limekuwa linakodishwa kwa watu mbalimbali kwa nyakati tofauti
kwa bei ya juu ila kinachooneshwa halmashauri ni kiasi kidogo sana kama vile shilingi 1,030/= kwa ekari moja wakati ukweli ni kwamba wanakodisha 100,000/= au zaidi kwa eka moja. Pia ikumbukwe kuwa hili ndilo lile eneo lililofyekwa mazao na migomba ya aliyekuwa mbunge wa Vunjo ndugu Aloyce Kimaro mwaka juzi.
Pamoja na kuwa shamba hilo ekari 210 zimerudi kwa wananchi bado serikali kupitia wizara ya kilimo na chakula wamebaki na ekari 100 (kwa ujumla ziko 310) ambazo miaka nenda rudi wanasema ni za utafiti ingawa tunajua kuwa ni eneo endelevu linalozalisha mboga na migomba na linaendeshwa na raia wa nje ya nchi.
Shamba lingine ambalo mheshimiwa mbunge amelirudisha kwa wananchi ni shamba la Valeska lenye ukubwa wa ekari 1500! Halmashauri wamejaribu kumwambia mbunge Nassari kuwa eti wananchi wagawiwe ekari 500 tu na zingine wazifanyie biashara ila mbunge amekataa katakata na kuagiza kuwa eneo lote lipewe wananchi. Hili lilikuwa chini ya ARCU kwa miaka yote.
Kwa sasa mheshimiwa mbunge ana mipango ya kurudisha mashamba ya Mbuguni na Doll Estate kwenye umiliki wa wananchi wake ambao wana matatizo ya ardhi. Kwa nyongeza ni kuwa serikali ya CCM iliwekeana mikataba mibovu ya muda mrefu ila kwa hekima za mbunge Nassari wanarudisha. Mambo haya ni makubwa sana kufanywa na mbunge huyu kwa muda mfupi wa miaka miwili ya ubunge wake huku akiwa hana hata diwani mmoja wa chama chake cha CHADEMA kwani madiwani wote ni wa CCM.
Ziara mbalimbali za kupanga na kushtukiza kwenye miradi mikubwa ya maji yenye thamani ya zaidi ya sh Bilioni 6.9 kwenye vijiji vya patanumbe, ambureni moivaro, nshupu, kikuletwa, majengo, king'ori, kwa ugoro-migandini-maroroni, mbuguni, nk. Jimboni arumeru mashariki
Tuesday, May 6, 2014
MBUNGE JOSHUA NASSARI ATEKELEZA AHADI KWA WANANCHI WAKE .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment