Jiwe kubwa likiwa limeanguka kutoka mlimani na kuziba barabara ya Vuga kutoka Mombo kuelekea Korogwe na Lushoto.
Kwa juu ni mlima ambapo jiwe hilo liling'oka na kudondoka hatimaye kuziba barabara hiyo kwa takribani saa sita.
Abiria na madereva wakiwa wamekaa wakisubiri mamlaka zinazohusika wafike ili kutoa msaada wapate kuendelea na safari.
Wanausalama wakiwa eneo la tukio tayari kuweza kulisogeza jiwe hilo ili abiria na watumiaji wa barabara ya Vuga kuendelea na safari.
Hayo ni baadhi ya mawe ambayo yanaonekana kwa juu ya barabara ya Vuga inayounganisha Mombo na Lushoto.
HALI ya usafiri kutoka Mombo-Korogwe kuelekea wilaya ya Lushoto mkoani Tanga ilikuwa tete baada ya jiwe kubwa kuangua barabarani katika eneo la barabara ya Vuga.
Jiwe hilo lilisababisha wasafiri wa barabara hiyo kukwama kwa takribani saa 6 bila magari kupita.
Lakini hatimaye baadae vyombo vya usalama wakishirikiana na wanainchi waliweza kulitoa na hatimaye usafiri wa njia hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida.
No comments:
Post a Comment