
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam
uliotawalia kwa kiasi kikubwa na Yanga ambao walipoteza nafasi nyingi
katika kipindi cha kwanza na mpaka timu zinaenda mapumziko hakuna timu
iliyoweza kuona lango la mwenzie.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Yanga walionekana
kutafuta bao kwa nguvu, mpaka kufikia dakika ya 50 tayari walishapata
kona tisa ambazo hazikuzaa matunda. Wakati muda ukizidi kuyoyoma na
mashabiki wa Yanga wakiwa wameanza kukata tamaa ya kupata ushindi dhidi
ya waarab, Nadir Haroub Cannavaro aliwainua maelfu ya mashabiki wa Yanga
katika dakika ya 82 baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho ubao wa matokeo ulikuwa
unasomeka 1 kwa upande wa yanga na 0 kwa waarabu. Timu hizi zitarudiana jijini
Cairo wiki mbili zijaz
No comments:
Post a Comment